Elections 2010 Helikopta ya Slaa yapata tabu kutua Mpwapwa

jambo1

JF-Expert Member
Jul 5, 2009
241
29
Helikopta ya Slaa yapata tabu kutua Mpwapwa

Thursday, 02 September 2010
Salim Said, Mpwapwa

HELIKOPTA ya mgombea urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chadema, Dk Willbrod Slaa, juzi ilipata tabu kutua katika vijiji vya Wilaya ya Mpwapwa, kufuatia kutoonekana vyema kwa vijiji hivyo ambavyo nyumba za watu wake, zimeezekwa kwa matope.

Katika baadhi ya maeneo, helikopta hiyo iliyokuwa imembeba Dk Slaa ililazimika kurudia katika sehemu za vijiji ambavyo ilivipita kwa sababu ya kutoonekana vizuri.

Hata hivyo akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Winza, katika Jimbo la Kibakwe, wilayani Mpwapwa, Dk Slaa aliwaomba radhi wananchi kwa kuchelewa kufika, kwa sababu rubani wake alipata tabu ya kutafuta kijiji hicho.

"Ndugu zangu rubani wangu alipata tabu sana kukitafuta kijiji chenu, sisi tulidhania ni kutokana na hali ya hewa, kumbe vijiji vyenu havionekani ukiwa angani kwa sababu nyumba zenu zimeezekwa kwa matope, hivyo tunawaomba radhi kwa kuchelewa lakini muwe wavumilivu," alisema Dk Slaa.

"Lakini wakati nyinyi mnakaa ndani ya nyumba zilizoezekwa kwa matope, mbunge wenu, George Simba Chawene, anatembea na Sh7 milioni za mshahara wa kila mwezi na marupurupu ya Sh180,000 ,bungeni hata kama hakufanya lolote," alisisitiza.

Mwandishi wa habari hizi, pia ilishuhudia asilimia kubwa ya nyumba za watu katika kijiji hicho, zikiwa zimeezekewa kwa kutumia matope, hali inayoashiria ugumu wa maisha ya watu wa eneo hilo .

Dk Slaa alisema pamoja na dhiki hiyo, wananchi hao wengi wakiwa ni wachimbaji wadogo, hivi karibuni walivamiwa na polisina kuhamishwa kwa nguvu katika machimbo yao .

"Ndugu zangu poleni sana kwa kuhamishwa kwa nguvu katika machimbo yenu ya rubi na kupigwa risasi. Lakini hata fidia hamkulipwa, nashangaa kwa sababu tumepitisha sheria ya rubi kwamba ichimbwe na wachimbaji wadogo wadogo," alisema Dk Slaa.

"Nawahakikisha ndugu zangu mambo haya yatamalizwa na serikali ya Chadema ndani ya siku 100 kwa sababu sheria ipo," alisema Dk Slaa.

Alisema kitendo hicho kinaashiria kuwa Watanzania hawajajikomboa katika ardhi yao wenyewe.

"Kumbukeni kuwa Watanzania waliwafukuza wazungu si kwa sababu ya ubaya wao au kuwapiga Watanzania, ila kwa ajili ya kupata uhuru wa kujitawala na kujiamulia," alisitiza.

Katika mkutano huo, mwananchi mmoja alimweleza Dk Slaa kwamba wafanyabiashara watatu ambao ni raia wa Tanzania wanaoishi nje, waliwapora mawe yao ya rubi yenye thamani ya Sh400 milioni.

Source:Mwananchi 02/09/2010
 
“Lakini wakati nyinyi mnakaa ndani ya nyumba zilizoezekwa kwa matope, mbunge wenu, George Simba Chawene, anatembea na Sh7 milioni za mshahara wa kila mwezi na marupurupu ya Sh180,000 ,bungeni hata kama hakufanya lolote," alisisitiza.

“Nawahakikisha ndugu zangu mambo haya yatamalizwa na serikali ya Chadema ndani ya siku 100 kwa sababu sheria ipo,” alisema Dk Slaa.

Katika mkutano huo, mwananchi mmoja alimweleza Dk Slaa kwamba wafanyabiashara watatu ambao ni raia wa Tanzania wanaoishi nje, waliwapora mawe yao ya rubi yenye thamani ya Sh400 milioni

Source: Mwananchi
 
AISEEE!!!:eek2:
 
Helikopta ya Slaa yapata tabu kutua Mpwapwa

Thursday, 02 September 2010
Salim Said, Mpwapwa

HELIKOPTA ya mgombea urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chadema, Dk Willbrod Slaa, juzi ilipata tabu kutua katika vijiji vya Wilaya ya Mpwapwa, kufuatia kutoonekana vyema kwa vijiji hivyo ambavyo nyumba za watu wake, zimeezekwa kwa matope.

Katika baadhi ya maeneo, helikopta hiyo iliyokuwa imembeba Dk Slaa ililazimika kurudia katika sehemu za vijiji ambavyo ilivipita kwa sababu ya kutoonekana vizuri.

Hata hivyo akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Winza, katika Jimbo la Kibakwe, wilayani Mpwapwa, Dk Slaa aliwaomba radhi wananchi kwa kuchelewa kufika, kwa sababu rubani wake alipata tabu ya kutafuta kijiji hicho.

"Ndugu zangu rubani wangu alipata tabu sana kukitafuta kijiji chenu, sisi tulidhania ni kutokana na hali ya hewa, kumbe vijiji vyenu havionekani ukiwa angani kwa sababu nyumba zenu zimeezekwa kwa matope, hivyo tunawaomba radhi kwa kuchelewa lakini muwe wavumilivu," alisema Dk Slaa.

"Lakini wakati nyinyi mnakaa ndani ya nyumba zilizoezekwa kwa matope, mbunge wenu, George Simba Chawene, anatembea na Sh7 milioni za mshahara wa kila mwezi na marupurupu ya Sh180,000 ,bungeni hata kama hakufanya lolote," alisisitiza.

Mwandishi wa habari hizi, pia ilishuhudia asilimia kubwa ya nyumba za watu katika kijiji hicho, zikiwa zimeezekewa kwa kutumia matope, hali inayoashiria ugumu wa maisha ya watu wa eneo hilo .

Dk Slaa alisema pamoja na dhiki hiyo, wananchi hao wengi wakiwa ni wachimbaji wadogo, hivi karibuni walivamiwa na polisina kuhamishwa kwa nguvu katika machimbo yao .

"Ndugu zangu poleni sana kwa kuhamishwa kwa nguvu katika machimbo yenu ya rubi na kupigwa risasi. Lakini hata fidia hamkulipwa, nashangaa kwa sababu tumepitisha sheria ya rubi kwamba ichimbwe na wachimbaji wadogo wadogo," alisema Dk Slaa.

"Nawahakikisha ndugu zangu mambo haya yatamalizwa na serikali ya Chadema ndani ya siku 100 kwa sababu sheria ipo," alisema Dk Slaa.

Alisema kitendo hicho kinaashiria kuwa Watanzania hawajajikomboa katika ardhi yao wenyewe.

"Kumbukeni kuwa Watanzania waliwafukuza wazungu si kwa sababu ya ubaya wao au kuwapiga Watanzania, ila kwa ajili ya kupata uhuru wa kujitawala na kujiamulia," alisitiza.

Katika mkutano huo, mwananchi mmoja alimweleza Dk Slaa kwamba wafanyabiashara watatu ambao ni raia wa Tanzania wanaoishi nje, waliwapora mawe yao ya rubi yenye thamani ya Sh400 milioni.

Source:Mwananchi 02/09/2010

Tatizo kubwa la Watz ni hesabu.

Imekuwa ngumu sana watu kukokotoa hii formula x = y + z

where x -- Utawala wa CCM
y -- Umaskini wangu
z -- Umaskini wa taifa langu

Na hii formula inaaply kwa kila binadamu asiye fisadi anayeishi Tanzania
 
Back
Top Bottom