MAJINA ya watu saba walionusurika kufa baada ya helikopta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliyokuwa wakisafiria kuanguka, yamefahamika.
Helikopta hiyo ilianguka na kuwaka moto juzi kwenye Ziwa Natron mkoani Arusha.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Matei Basilio, alisema ajali hiyo mbaya ilitokea juzi asubuhi majira ya saa 3:30, baada ya helikopta hiyo, ambayo namba zake za usajili hazijafahamika, kuruka na dakika chache baadaye ikiwa angani kutoa moshi mzito mweusi, kabla ya kuanguka ndani ya Ziwa Natron.
Kamanda Basilio alitaja walionusurika kifo na nchi wanazotoka kwenye mabano kuwa ni pamoja na Jeffrey Sibbery (Canada), Forest Sowyer (Marekani), Ben Herberston (Australia) na Mark Berker (Uingereza), mkazi wa Kisongo wilayani Arumeru, ambaye inasadikiwa kuwa mwenyeji wa watalii hao.
Watanzania walionusurika katika ajali hiyo ni pamoja na rubani wa helikopta hiyo ya jeshi, Luteni Kanali Mayenga, ambaye amevunjika mguu na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi, msaidizi wake, Luteni Edward, fundi wa helikopta, Gabriel Majala na mwongoza watalii, Issaya ole Poruo.
Aidha, kamanda huyo alisema kuwa Jeffrey na Forest wamepelekwa Kenya kwa ndege ya kukodi kwa matibabu zaidi baada ya hali zao kuonekana haziridhishi.
Akisimulia ajali hiyo, Kamanda Matei alisema mara baada ya helikopta hiyo kuanguka, wakazi wa Kijiji cha Engusero, waliwahi eneo la tukio na kufanikiwa kuwaoka abiria hao, waliokuwa katika helikopta hiyo kabla hawajapata madhara ya moto uliolipuka.
Watalii hao walikwenda katika eneo hilo kwa lengo la kupiga picha maeneo ya vivutio vya utalii, likiwemo Ziwa Natron na Mlima Oldonyo Lengai, ambao una sifa ya kutoa volkano hai na unaosifika kwa kulipuka mara kwa mara.
Wakati huo huo, Alli Waziri (45), alifariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea jana katika eneo la Ndemwa ndani ya hifadhi ya Ngorongoro baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Land Cruiser, lenye namba za usajili T 241 ATC, kupinduka.
Kamanda Basilio alisema gari hiyo ilipinduka baada ya gurudumu la mbele upande wa kushoto kupasuka wakati gari ikiwa katika mwendo mkali. Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Gerald Msaki (45).
Govt chopper for sale
-Helicopters have of late become a popular means of transport for local politicians during election campaigns, enabling candidates to reach remote areas and also serving as a crowd-puller
Dar es Salaam
THE government has put one of its helicopters, along with various spare parts, up for sale and interested bidders given a deadline of mid-next month to submit offers.
The pending sale of the government chopper was advertised for the first time earlier this year with the initial deadline set for April 5. However, the Ministerial Tender Board in the ministry of finance has now re-advertised the tender and set November 15 this year as the new deadline for submission of tenders.
According to the specifications of Tender No. 1 of 2006/07 as advertised through a weekly regional newspaper last week, the government is inviting bids for the purchase of a boarded helicopter and spare parts on as is, where is basis.
It says details of the helicopter plus a list of the spare parts available and further information can be found on the official website of the ministry of finance.
However, when visited yesterday, the ministrys website showed only the tender notice as printed in the newspaper but did not provide any of the stated additional information.
While reasons for the sale of the government chopper and details of the tender documents remain sketchy, THISDAY understands that the government currently has a fleet of around three Agusta Bell helicopters.
One of them, model Bell 206, is owned by the police force and has traditionally been the only such aircraft owned by the government.
Apart from normal police operations, the machine has been put to use in various rescue missions and to fly top government leaders to remote locations in the country.
The Ministry of Defence and National Service recently bought four Agusta Bell helicopters model 412 EP for the Tanzania Peoples Defence Forces (TPDF). It is understood that two of these aircraft are currently in service.
Investigations by THISDAY have established that the helicopters bought for the TPDF are soft-skin, civilian choppers that are not suitable for specialised military operations.
A private company, Khaisa Enterprises Limited, has already filed a 17bn/- suit against the defence ministry for breach of contract in connection with the supply of helicopters to the TPDF.
The firm is seeking compensation amounting to 10 million euros (approx. 16.8bn/-) from the ministry for unlawfully dishonouring an agreement between the two parties over the supply of the choppers.
In the ongoing civil case number 74 of 2007 being handled by the High Court in Dar es Salaam, the Attorney General ? in his position as the governments chief legal advisor - has also been named as respondent alongside the ministrys permanent secretary.
According to details of the plaint obtained by THISDAY, Khaisa Enterprises claims that the defence ministry went against a valid contract in which the company was to supply six units of COUGAR AS 532 helicopters manufactured by Frances Eurocopters company at a total cost of 125 million euros (approx. 210bn/-).
It is alleged that the Augusta Bell choppers eventually purchased for the TPDF had already been rejected by the defendants (defence ministry), on the basis that the same were of inferior quality and were civilian helicopters, while defendants required helicopters for military use.
It is further alleged that the defence ministry purchased helicopters at a higher cost of $9.263m each, contrary to the ones proposed by the plaintiff (Khaisa Enterprises Ltd) which were relatively cheaper at $4.7m each, thus making the nation suffer a loss of $4.563m for each helicopter purchased.
Our sources say a local company, Merlin International Limited, was the agent used to supply the Agusta Bell helicopters to the government at vastly inflated prices.
Merlin International, registered in the name of local businessmen Shailesh Vithlani and Tanil Somaiya, has also been linked to the controversial 28 million pounds sterling (approx. 70bn/-) military radar system purchase, the governments purchase of a $40m (50.7bn/-) Gulfstream presidential jet, the supply of over 600 IVECO military trucks to TPDF and various other dubious deals.
Helicopters have of late become a popular means of transport for some local politicians during election campaigns, enabling candidates to reach remote areas and at the same time serving as a crowd puller
Ninachojua mimi msafara huu haukuwa wa watalii, kulikuwepo na watu kutoka ofisi ya raisi ambao walikuwa wameruka the day before ambao walitumwa kufuatilia utata unaoendelea sasa hivi kuhusu ujenzi wa soda ash factory ambao umeshindwa kuendelea baada ya Enviromental Impact Assesment report kuonyesha kwamba mradi is not sustainable na ungeharibu kabisa breeding site ya flamingo.
kiwanda hiki cha chumvi kinaitwa TATA kutoka India. Roumour has it that EL anataka sana hiki kiwanda kiendelee lakini watu wengi hasa conservation activist wameupiga vita kabisa na wengi bado wanaendelea kuupiga vita.
Inasemekana JK alituma vijana wake wakatafuta na wataalamu wanaolijua eneo ili kumsaidia kufanya decision kama TATA ifanye kazi au la.
Rumour has it that EL anataka sana hiki kiwanda kiendelee lakini watu wengi hasa conservation activist wameupiga vita kabisa na wengi bado wanaendelea kuupiga vita.
Inasemekana JK alituma vijana wake wakatafuta na wataalamu wanaolijua eneo ili kumsaidia kufanya decision kama TATA ifanye kazi au la.
Wajamaa wa serikali walikuwa wafanya trip the day before, hao waliopata ajali walienda kama wataalamu, huyo muaustralia alikuwa mpiga picha na huyo jamaa wa uingereza anayeishi arusha alichukuliwa kwa sababu ni mtaalamu wa mimea na ndege na ameshafanya kazi katika maeneo hayo.
hao wengine sina uhakika walikwenda kama nani.
RAIA MWEMA said:Maliasili, Ulinzi, Ikulu watofautiana
Waandishi Wetu
Ajali ya Watalii Arusha
WAKATI kuna hisia kwamba helikopta ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ilikodishwa kwa watalii ambao walipatwa nayo ajali wiki iliyopita Arusha, kulikuwa na hali ya kujiumauma katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Wizara ya Utalii na Ikulu, ili kuelezea sakata hilo.
Gazeti hili katika kufuatilia ajali hiyo, ambayo watalii wanne wa kigeni walinusirika kifo, lilipigwa ‘danadana' sehemu zote hizo bila kujua ‘wageni' hao walikuwa wa nani hasa na kwa nini walitumia helikopta hiyo.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Athumani Kapuya na naibu wake, Omar Yussuf Mzee, hawakuwa na majibu ya kutosheleza juzi walipoulizwa kuhusu mazingira ya helikopta hiyo ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kubeba watalii wa kigeni.
Wakati Kapuya alisema yuko likizoni Kaliua, Tabora, na hajui chochote kuhusiana na suala hilo, alilitaka Raia Mwema kumtafuta Mkuu wa Majeshi atoe ufafanuzi wa suala hilo.
"Hivi sasa nipo Kaliua. Niko likizo…Mimi sijui kinachoendelea huko. Mtafute CDF (Mkuu wa Majeshi) ili akupe taarifa hizo," alisema Profesa Kapuya.
Raia Mwema lilipowasiliana na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Omar Yussuf Mzee, alisema kwamba hakuwa na taarifa za kina kwa kuwa alikuwa safarini, na kwamba alikuwa ameagiza apewe taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo.
Naibu Waziri alisema tayari ameomba apatiwe taarifa za suala hilo kutoka uongozi wa JWTZ kuhusu nani walikuwamo, helikopta hiyo ilikuwa inafanya nini huko na sababu za ajali yake.[/B]
Kama ilivyokuwa kwa Kapuya, naye pia alilitaka gazeti hili kupata maelezo kutoka JWTZ kwenyewe, na kumtaka mwandishi awasiliane na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi kwa maelezo.
"Nimeomba nipewe taarifa za ajali hiyo. Ninataka kujua helikopta hiyo ilikuwa ikifanya kazi gani huko, nani walikuwamo na nini kilisababisha ajali.
"Kwa sasa unaweza kuwasiliana na Chief of Staff (Mnadhimu Mkuu). Atakuwa amekusanya taarifa hizo kwa sababu nimeagiza nipewe. Wasiliana naye," alisema Mzee.
Juhudi za kuwapata mkuu wa Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Luteni Jenerali Abdulraham Shimbo hazikuweza kufanikiwa.
Lakini, Raia Mwema iliwasiliana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, ambaye alikiri kuwa wageni waliokuwa katika helikopta hiyo walikuwa ni wageni wa serikali, na kwamba walikuwa hapa nchini kwa ajili ya kutengeneza filamu ya vivutio vya utalii nchini.
Profesa Maghembe alisema: "Wageni hao walikuwa ni wa serikali. Walikuwa wakitoka Travel Channel, na walikuja nchini ili kusaidia kutengeneza documentary (filamu) ili kusaidia kukuza utalii hapa nchini.
Watalii waliokuwamo katika helikopta hiyo, na ambao walinusurika katika ajali hiyo ni Jeffrey Sibbery anayetoka Canada, Forest Sowyer wa Marekani, Ben Herberston wa Australia na Mark Berker wa Uingereza. Pamoja nao, alikuwapo mkazi wa Kisongo wilayani Arumeru, Issaya ole Poruo, ambaye ilielezwa ya kuwa alikuwamo katika helikopta hiyo kwa ajili ya kuwaongoza watalii hao.
Alipoulizwa ilikuwaje wizara yake ikatumia chombo cha JWTZ kwa masuala ya kitalii, alisema: "Huu ulikuwa ni mpango wa serikali, na ulikuwa ni utaratibu wa State House (Ikulu). Halikuwa tatizo kubwa kupata helikopta ya jeshi.
"Tulishirikiana na Ikulu… Hawa walikuwa pia wageni wa Commander-in- Chief (Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete). Kwa hiyo halikuwa tatizo kwetu kupata helikopta ya jeshi. Tulihakikisha tunatumia vyombo vyote vya serikali ili kufanikisha kazi hiyo.
"Kama tungetumia vyombo vingine ingebidi tukodi. Na kama tungetumia vile vya nje ya nchi, basi tungepambana na washindani wetu (wa mambo ya utalii) jambo ambalo lisingefaa," alisema Waziri.
Hata hivyo, mwandishi wa habari wa Rais, Premmy Kibanga, alipoulizwa kuhusu Ikulu kuhusika na suala la kutoa kibali cha kutumia helikopta hiyo, alisema kwamba Wizara ya Maliasili na Utalii ndiyo iliyopaswa kutoa ufafanuzi wote jinsi walivyoweza kupata helikopta hiyo ya jeshi. "Wao walitakiwa kutoa taarifa zote. Waeleze ni nani alitoa kibali cha matumizi ya helikopta, na huyo ndiye angepaswa kueleza sababu za kuitumia… Kama wizara ilikosa ndege za kukodi, angeeleza," alisema Kibanga.
Hata hivyo, utata mwingine unaojitokeza hapa ni ushiriki wa mtu binafsi kuongoza watalii ambao walikuwa wageni wa serikali, kwani inafahamika kuwa serikali ina maofisa wake wanaohusika na uongozaji wa watalii.Waziri Maghembe alisema kwamba wageni hao walikuwa wamekuja kufanya kazi hiyo kama msaada kwa serikali, na kwamba kama ingekuwa wanalipwa basi kazi hiyo ingegharimu dola za Kimarekani milioni tano.
Alisema wageni hao tayari walikuwa wametunga filamu zao 5 ambaza zilikuwa zimeshinda Tuzo ya Oscar, na kwamba hata ya kwetu, kama ingekamilika, basi ingeweza kushinda tuzo hiyo.
Kwa mujibu wa Waziri wa Utalii, kabla ya ajali hiyo, wageni hao walikuwa wamefanya kazi Zanzibar na kisha wakaenda Mlima Oldonyolengai na hatimaye Ziwa Natron, ambako walipata ajali wakati wakifanya kazi.
"Kwenye Ziwa Natron kuanzia mwezi Oktoba kunakuwa na flamingo (korongo) wengi kutoka sehemu mbali mbali za Afrika. Wanakuja pale kwa ajili ya kuzaana. Kwa hiyo, hali inavutia sana na ndiyo maana wageni walikwenda kupiga picha pale.
"Bahati mbaya helkopta ilipoingia ndani ya ziwa iliangukia ndani. Bahati nzuri ilikuwa katika speed (kasi) ndogo, na milango ilikuwa wazi kwa sababu ya kupiga picha.
"Tunashukuru wenyeji wa eneo lile waliweza kuingia ndani ya ziwa kuwaokoa… Walitengeneza stretcher (machela) kwa kutumia nguo zao. Baadaye tulipopata taarifa tulituma flying doctors (madaktari wasiokuwa na mipaka) Jumatano iliyopita helikopta inayomilikiwa na JWTZ ilianguka na kushika moto Ziwa Natron mkoani Arusha, asubuhi majira ya saa 3:30, baada ya helikopta hiyo, ambayo namba zake za usajili hazikufahamika, kuruka na dakika chache baadaye ikiwa angani kutoa moshi mzito mweusi, kabla ya kuanguka ndani ya Ziwa Natron.
Watanzania walionusurika katika ajali hiyo ni pamoja na rubani wa helikopta hiyo ya jeshi, Luteni Kanali Mayenga, ambaye alivunjika mguu na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi, msaidizi wake, Luteni Edward, fundi wa helikopta, Gabriel Majala na mwongoza watalii, Issaya ole Poruo.
Watalii Jeffrey na Forest walipelekwa Kenya kwa ndege ya kukodi kwa matibabu zaidi baada ya hali zao kuonekana haziridhishi.
Mara baada ya helikopta hiyo kuanguka, wakazi wa Kijiji cha Engusero, waliwahi eneo la tukio na kufanikiwa kuwaoka abiria hao, kabla ya kupata madhara ya moto uliolipuka.
Ninachojua mimi msafara huu haukuwa wa watalii, kulikuwepo na watu kutoka ofisi ya raisi ambao walikuwa wameruka the day before ambao walitumwa kufuatilia utata unaoendelea sasa hivi kuhusu ujenzi wa soda ash factory ambao umeshindwa kuendelea baada ya Enviromental Impact Assesment report kuonyesha kwamba mradi is not sustainable na ungeharibu kabisa breeding site ya flamingo.
kiwanda hiki cha chumvi kinaitwa TATA kutoka India. Roumour has it that EL anataka sana hiki kiwanda kiendelee lakini watu wengi hasa conservation activist wameupiga vita kabisa na wengi bado wanaendelea kuupiga vita.
Inasemekana JK alituma vijana wake wakatafuta na wataalamu wanaolijua eneo ili kumsaidia kufanya decision kama TATA ifanye kazi au la.