Helikopta na malori ya Urusi yateketea Syria

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,377
8,075
ImageUploadedByJamiiForums1464095780.472917.jpg

Helikopta 4 na malori 20 ya Urusi yateketea nchini Syria

Picha za satellite zilitolewa kwa BBC zinaonyesha kuwa ndege nne za Urusi aina ya helkopta na malori 20 viliteketea moto ndani ya kambi moja ya kijeshi iliyo kati kati mwa Syria wiki iliyopita.

Kampuni moja ya ujasusi ya Marekani, Stratfor, iliyotoa picha hizo, inasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa Islamic State walihusika na uharibifu huo.

Islamic state hawajasema kuwa ni wao walihusika lakini taarifa kutoka kwa kundi hilo zinasema kuwa helikopta na malori yaliteketea.

Baadhi ya wataalamu wanasema kuwa huenda moto ulisambaa kutoka kwa tangi la mafuta ambalo lilipuka. Urusi bado haijazungumzia kisa hicho.
 
Yanarudi yale yale yakudai eti cruise missiles nne za Urusi zilianguka nchini IRAN baada ya kushindwa kufika kwenye target zake huko Syria! Habari yenyewe ikaja gundurika ni ya uongo na uzushi mtupu, nchi za magharibi wameshindwa ku contain kikundi hatarishi cha ISIS, badala ya nchi hizo kuja na mikakati yenye mshiko ya ku deal na magaidi wao wanakimbilia kutangaza propaganda/uzushi ili Dunia iamini kwamba Warusi wameshindwa kuwadhibiti ISIS nchini Syria!!

Jeshi gani linaweza kupark Helicopters karibu na mantanki ya mafuta, jeshi la anga la Urusi ndio lipo nchini Syria hakuna hata platoon moja ya infantry hayo malori watayaitaji kwa shughuli gani?

Mimi nilicho ona leo ni malori, magari na matenki ya mafuta yaliyo shambuliwa na kulipuliwa na jeshi la anga la Urusi wakishirikiana na airforce ya Syria, hizo habari za kudai zimetangazwa na BBC zimetoka source gani na tangu lini BBC ikawa na satellite za upekelezi kwenye orbit - lini?
 
hizo habari za kudai zimetangazwa na BBC zimetoka source gani na tangu lini BBC ikawa na satellite za upekelezi kwenye orbit - lini?

kusoma unajua tatizo lako kuelewa unayoyasoma, ni wapi katika habari hii pameandikwa bbc wana satelite za upelelezi kwenye orbit?!
ebu soma kipande cha habari mara 5 utaelewa tu:-
'Picha za satellite zilitolewa kwa BBC zinaonyesha kuwa ndege nne za Urusi aina ya helkopta na malori 20 viliteketea moto ndani ya kambi moja ya kijeshi iliyo kati kati mwa Syria wiki iliyopita.
Kampuni moja ya ujasusi ya Marekani, Stratfor, iliyotoa picha hizo, inasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa Islamic State walihusika na uharibifu huo.'
umeelewa?
 
Hii vita imejaa propaganda sana.. Ukifuatilia kwa karibu utaona mashambulizi wanayofanya ISIS syria hakuna nchi ya Magaharibi inayolaani hata kidogo. Lakini ikitokea Iran ama syria wameshambulia ISIS kama wanavyofanya sasa mji wa aleppo mara moja utasikia Kerry na timu yake wanalaani vikali.. Naamini kama ingekuwa imetokea kweli ISIS Tayari wangesharusha video na vyombo vya magharibi vyote ingekuwa breaking news masaa 24..
 
Back
Top Bottom