Hela Zinazoibwa na Wanasiasa wa Tanzania Zinakwenda Wapi?

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
17,369
33,015
Kinyungu nimekaa chini nikatafakari kiasi cha pesa kinachoibwa ama kukwapuliwa na Wanasiasa wa Tanzania na kugundua ni kiasi kikubwa sana. Cha ajabu pesa hizi sioni impact yake yoyote kwenye mazingira yanayotuzunguka Wananchi wa kawaida.

Wizi wa pesa za umma kwa wanasiasa si jambo geni, Kenya ni mfano mzuri wa nchi yenye wanasiasa wezi. Lakini angalau wanasiasa wa Kenya wanacho cha kuonesha. Kule Kenya ukiambiwa utaambiwa wazi Majumba fulani ya Real Estate ni Waziri fulani, Hotel fulani ni Waziri fulani, Kiwanda fulani ni Waziri yule, Kampuni fulani ni mwanasiasa au kiongozi fulani wa serikali, Kampuni hii ni Waziri huyu....lakini kwa Tanzania hali ni tofauti kabisa, wanasiasa wanaiba kila kukicha lakini hatuoni hela hizi zikirudi kwenye mzunguko wa uchumi!

Wanasiasa wa Tanzania mkiiba hela mnapeleka wapi? Au mnakimbizia Uswisi na South Africa?
 
Back
Top Bottom