Heko Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Hongera kwa kusimamia uwekwaji wa viashiria vya daraja pale Darajani, Old Bagamoyo Road karibu na MayFair Plaza.
Hili ni moja ya mambo yenye yaliangaziwa na wananchi wa Mikocheni kwenye mkutano wao na mbunge na diwani.
Sijui kama barabara ile inasimamiwa na TANROADS au halmashauri, lakini najua wamehusika katika utekelezwaji. Sasa daraja limewekewa reflectors za nguzo katika kona zote nne na zinaonekana tangu umbali wa mita 200.
Kipindi cha nyuma daraja halikuwa na kingo wala viashiria, hivyo kupelekea ajali nyingi hasa wakati wa mvua kubwa, ukizingatia daraja lenyewe ni jembamba.
Hongera wahusika!
 
Kama hivyo viashiria vimo ndani ya hifadhi ya barabara, Magufuli ataving'oa sasa hivi!
 
Back
Top Bottom