Hekima za Mzee Kikwete

Hekima za Mzee Kikwete

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,953
Reaction score
40,634
"Sisi tuliostaafu tunapata muda mwingi wa kutalii kwenye mitandao ya kijamii kuona kinaongelewa nini kuhusu nchi yetu. Juzi baada ya hotuba yako fupi uliyoitoa baada ya kula kiapo nilipitia kuona wananchi wanaongea nini kuhusu hotuba hiyo? Nakuhakikishia, wananchi wameipokea vizuri sana."

Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete akimsimulia Rais Samia Suluhu Hassan namna wananchi walivyoipokea positively hotuba yake baada ya kuapa.

Je, kuna kitu JK alitaka SSH akipate ambacho anaamini hakikuwepo wakati wa mtangulizi wake na sasa yeye SSH amekisema? Au hekima yake imemtuma kusifu tu na hakuna cha ziada kwenye wosia wake?
 
JK ni zaidi ya mwanasiasa.

Kwanza kuna principle ya never speak ill of the dead, kaitumia vizuri principle hii.

Ni kweli inabidi ampongeze Mama Samia kwanza kumpongeza kwa kulipita sekeseke lililotaka kujitokeza nyuma ya pazia kutaka kuvunja katiba VP asiwe rais.

Na pili kumpa moyo kuwa hata kwa maoni aliyoyaona mitandaoni, watu wamefurahia katiba kufuatwa na Mama Samia kuwa Rais.

Hawa watu aina ya Kikwete sasa ni nadra kuwapata chamani na kwa kueleza mambo kwa umahiri mkubwa.
 
Kikwete karudi chawla kwenye line ya uongozi
Atumie spana zake ili arudishe hali ya uwezo wa watanzania kujitafutia na kujiingizia kipato iliyo tolewa na wenye niambaya na wendazake
 
Mambo matatu ni "takes"hapo kwa Mhe. Rais
1. Asijenge uadui na mitandao ya kijamii kama mtangulizi wake kwa maana wanaoitumia si watu wa hovyohovyo pekee bali hata wao washeshimiwa wanaitumia, tena wastaafu ambao wana lens nzuri ya kuona na kushauri juu ya mambo ya nchi.

2. Asipuuze yasemwayo katika mitandao ya kijamii au nguvu ya mitandao hiyo katika zama hizi kwa kuwa wako watu wakubwa, werevu na makundi mtambuka wanavinjari humo.

3. Asiwaangushe wananchi walioweka matumaini makubwa sana kwake ukilinganisha na mtangulizi wake kwa jinsi ya kinachojadiliwa humo juu yake.

Tukumbuke huyu ni muasisi wa ule msemo maarufu "za kuambiwa changanya na za kwako". Huyo ndio JK, all time father of our modern politics
 
Mambo matatu ni "takes"hapo kwa Mhe. Rais
1. Asijenge uadui na mitandao ya kijamii kama mtangulizi wake kwa maana wanaoitumia si watu wa hovyohovyo pekee bali hata wao washeshimiwa wanaitumia....
Umeshauri vema, asante mkuu.
 
Mambo matatu ni "takes"hapo kwa Mhe. Rais
1. Asijenge uadui na mitandao ya kijamii kama mtangulizi wake kwa maana wanaoitumia si watu wa hovyohovyo pekee bali hata wao washeshimiwa wanaitumia...
Nikuulize machache utusaidie;
1.Ni kipi kati ya aliyoongea mama SSH siku ya kuapishwa kilichopokelewa chanya na wananchi?

2.Je, ni hichohicho kilichomfanya Kikwete naye afurahie hotuba hiyo.

3.Je, hicho kilichofurahisha wananchi hakikuwepo kabla?
 
1. Sijafuatilia kwenye mitandao na kufanya utafiti kujua kama hotuba yake ilipokelewa positively na if yes, ni nini kilifanya ipokelewe hivyo ila kwa MUJIBU wa JK anasema ilipokelewa positively.
2. Swali na. 2 na 3 linaweza kupata majibu kutoka katika jibu na. 1. Thanks
 
Hiki: (1)Tushikane mikono (2)tuangalie mbele tunakokwenda na si kuangalia(indirect message: some things were running wrong),(3)Tanzania ipo salama.Alionekana kutokuwa na mbwembwe na kutulia sana ktk speech yake.
Nikuulize machache utusaidie;
1.Ni kipi kati ya aliyoongea mama SSH siku ya kuapishwa kilichopokelewa chanya na wananchi?
2.Je, ni hichohicho kilichomfanya Kikwete naye afurahie hotuba hiyo.
3.Je, hicho kilichofurahisha wananchi hakikuwepo kabla?
 
Tuzidi kumuombea azidi kuishi mzee wetu maana kwa sasa ndiyo tegemeo letu wa kukemea mapepo
Kweli kabisa. Sioni waziri mkuu mstaaafu mwenye nguvu ndani ya chama, Ali mwinyi kachoka, wazee wengi ndani ya chama ni njaaa tu. 90% ya tunaowaita vijana ndani yachama na wanataka uongozi wa juu ni wapigaji tu.
 
Sahihi kabisa mkuu
 
Back
Top Bottom