Hekima ya kitume kwa baba zangu maaskofu wa KKKT iko wapi?

Trump2

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
1,553
Reaction score
2,610
Nimesoma Waraka wa MAASKOFU Mara mbili, nikarudiamara ya tatu.Kwanza nianze kwa kukupongezeni kuwa mumetimiza wajibu wenu wa kutumia demokrasia ya uhuru wa kujieleza sawasawa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa namna fulani,ama kwa makusudi au kwa kutokujua kuna mambo muhimu hamjayagusia.

Nafikiri kwamba ilihitajika tafakari fulani kwa upande wenu kabla ya kuutoa ule waraka sawasawa na lile andiko/usemi wa BORITI na KIBANZI.

Kwa maana hiyo sasa naomba nijitolee kutoa ulimu kwa MAASKOFU wangu kama wanavyotoa Elimu ya Ufalme wa Mbinguni kwetu.

Kwanza naomba ifahamike kwamba katu sina madaraka ya kimbingu ya kuweza kuwajibu wapakwa Mafuta wa Bwana Mungu ila hiki ninachofanya hapa ni kuwaelimisha tu kwenye hili eneo ninalolimudu la Kaisari ambako ninyi wenyewe kwa hiari yenu mmeamua kuvuka ng'ambo na kulifuata huku mkijua fika kuwa Ya Mungu tunastahiki kumpa Mungu na ya Kaisari nayo yana wenyewe.

1. Hoja kubwa ambayo mmeizungumza kwa Umakini Ni suala la Katiba Mpya.
Majibu , kwanza mchakato wa katiba mpya ulianzishwa kwa Utashi wa Rais Kikwete ambaye anapaswa kukumbukwa kwa hili Aliona Mbele Sana , Mchakato haukukwamishwa na Serikali ya Magufuli au Kikwete ukweli Ni Huu hapa

" Nakumbuka katika Bunge la Katiba maaskofu walishiriki bunge la katiba ambapo bunge liliamua kwa wingi katiba pendekezwa unapotaka tuachane na maamuzi ya bunge na uhuru wake mbona tena unaenda kinyume na hoja zako bunge lipewe uhuru?? Maamuzi Yale yalifanywa kwa mujibu wa sheria je tunataka kujenga utamaduni wa kutoheshimu katiba na sheria?? Maamuzi Yanapofanywa na wengi hata kama mimi nawewe haturidhiki, ndio demokrasia yenyewe !!! Kwa mujibu wa sheria kilichobakia ni wananchi kupiga kura,na endapo kama wana hoja mbadala basi wasubiri wakati huo badala ya kuturudisha kujadili rasimu ya Warioba as a matter of principle .

2. Hoja Ingine ilikuwa hali ya Siasa.Hoja za MAASKOFU Ni kuminywa kwa Demokrasia , Kumwagika Damu , kushambuliwa kwa Risasi Na watu kuokotwa wakiwa wamekufa .
Majibu , kwa Taifa lenye watu zaidi ya Milioni 50 usitegemee watu wote watafurahi Na kuridhika Na utawala Huu, diversity ni Muhimu Sana katika masuala yanayojenga taifa lakini tunashuhudia Siasa yetu ikianza kuingiliwa Na mataifa ya ulaya kupitia Baadhi ya wanna Siasa wenye ulafi Na tamaa ya fedha Na madaraka , katika hili tusitazame Serikali tu pia twende mbali tutazame mbinu wanazotumia hao watu wa nje wanaotamani rasilimali zetu ,tutazame Mahusiano yao Na wanasiasa wetu, Na mwisho tujifunze kuviachia Kazi vyombo vyetu ambavyo kisheri ndivyo vyenye jukumu la kuchunguza; suala la muda wa uchunguzi Ni muhimu Sana lakini tuvute subira Mana Kanisa la KKKT halina utaalamu Na masuala ya ulinzi Na Usalama.

Katika hii hoja nisema Jambo japo litauma kidogo, hata katika Kanisa la KKKT tumeshuhudia Na nyinyi mkimwaga Damu kule Dayosisi ya Meru mkigombea madaraka au mmesahau jamani?Ikiwa kanisani tu mnafikia mahali mnagombania Wamachame na Wakibosho?Sembuse huku kwa Kaisari kulumbana hapa na pale kwa ajili ya siasa?Anyway huko nidingependa kwenda sana maaskofu wangu.

- Kama ni Ufisadi ambao Magufuli anapambana nao Na nyinyi Msisahau pia kutumbia ufisadi na wizi mkubwa wa Mali za kanisa kupitia hotel ya KKKT Arusha ambayo mpaka sasa imeingiza waumini katika matatizo makubwa ya Kiuchumi Mana zile Ni mali za waumini.Kanisa lijitahidi mno kuishi sawasawa na matarajio ya umma na matakwa ya mwenyezi Mungu.

- Kama ni Polisi kutumia nguvu kubwa katika Jamii, kumbukeni Na nyinyi pia kutumia mgogoro wa kuwaweka ndani wachungaji wa KKKT kule Njombe uliofanywa na askofu Mengele,kufunga milango ya kanisa pale Mafinga na kutaka kumfukuza mkuu wa Jimbo Mch Kipangula , Hali hii imesababisha hadi Leo Jimbo la Mufindi kujitenga na Dayosisi ya Kusini na kuwa nchini ya uangalizi wa Dayosisi ya Iringa , hii inaonyesha Roho ya Vurugu Na Machafuko iliyopo ndani ya Kanisa kilo kwahiyo tunachokiona kwa jamii ni matokeo ya matatizo yaliyoanzia Kanisani tutafakari hapa kidogo.

- Nimesoma Waraka mnalalamika kuhusu fedha za Serikali kutumika kununua madiwani.Jamani MAASKOFU wangu mnajua hii Roho Na pepo la rushwa limeanzia Kanisani kwenu jamani, hivi hebu tuambieni matatizo ya ukabila,ukanda rushwa inayotajwa vilivyotamalaki katika uchaguzi wa kupata mkuu wa KKKT aliyestaafu na huyu wa sasa , hivi mmesahau Kampeni zilizokuwa zinafanywa kama vile mnagombea Ubunge Na udiwani mnakumbuka Kwanini Askofu Alex Gehazi Malasusa alivyopitishwa Kuwa Askofu Mkuu pasipo yeye Kuwa Mgombea?Hi ilitokana Na kushindwa kupatikana kwa Askofu kwa njia za Kidemokrasia baada ya Mapapa Wawili kushindana bila muafaka ndio ikatumika Busara ya kumchagua Baba Askofu Malasusa kuziba Mpasuko.Je hapa tunaruhusiwa kuhisi kwamba sasa Maaskofu mmeichukua hoja za chama fulani cha upinzani na kuzifanya ni za kanisa?Je mnataka sasa sisi watu wa mwilini tuamini hilo la kwamba chama hicho kina uhusiano wa karibu mno na kanisa hilo hasa Dayosisi za Kaskazini?

- Mmezungumzia kuhusu Migogoro ya Wafugaji Na wakulima, Migogoro ya Kisiasa, jamani hebu Na Ninyi Maaskofu Msisahaua kutuambia hali mbaya ya kikanisa huko Mtwara na mgogoro ndani ya Kanisa chini ya Askofu Mbedule ambao umesabaisha Kanisa kufungwa Na kufunguliwa Tena,ila mpaka Sasa bado Kuna changamoto .

- Nimeusoma waraka vizuri,Mimi Ni mluteri maisha yangu yote sijawahi kuona kipindi kigumu katika kanisa kama hiki , unapotazama Changamoto zinazoikabili serikali utaona nyingi zimeanzia Kanisani Na Sasa zimeanza kutoka kwenye jamii.

- Leo ukiuliza baadhi ya Wachungaji wenu wanasema Tumekuwa na viongozi wasaka madaraka na kugombania vyeo ,kumekuwa na rushwa na wizi wa kutisha pamoja na manyanyaso ndani ya Kanisa, Sasa kama hivi viko ndani ya Kanisani unategemea nini huku kwenye jamii maana waumini wenu ndio hao hao wananchi na wana Siasa.

Siku zote naamini Ibada njema inaanzia nyumbani

Pia tusisahau hadithi ya Yesu juu ya Kibanzi vs Boriti

Mwisho nimalizie na mambo mawili.
1. Kwanza kama Kanisa la KKKT lina issue na serikali si waombe kukutana na viongozi wa serikali? Mbona JPM kaenda makanisani kwao kusali si wangemwambia Mheshimiwa subiri tuna maongezi ya faragha baada ya ibada wakaongea??iweje tulumbane hadharani kwa kigezo Cha mnatimiza wajibu wenu kwa kusema , Haki lazima iende Na wajibu .

2. Kuendelea Kutoa Waraka kama huu Ni kuzidisha Mpasuko was Kanisa Na Serikali ambao unanufaisha upande mmoja wa Siasa za Upinzani hivyo Msitarajie Serikali ya chama kingine itakaa kimya , lakini pia inachafua Nchi yetu katika medani za Siasa za Kimataifa Na mashirikiano Mema Na mataifa mengine .

Hivi Enzi za Baba Askofu Mkuu Mstaafu wa KKKT Samson Mushemba hapakuwa Na changamoto kama hizi katika Jamii?Naambiwa zilikuwepo Nyingi Sana ila Askofu Mushemba Alitumia Hekima Kuu katika Utume wake kushughulikia Changamoto hizi katika Hali ambayo ilileta Utengamano wa Kanisa Na Serikali Na ndio Mana hatukuona haya tunayayaona Sasa.

Nakumbuka wao walipambana kuimarisha Huduma za Kiroho Na haswa Injili ambayo ndio msingi Mkuu wa Kanisa la KKKT Na pia kuimarisha Huduma za Kijamii mfano Kuendeleza Na kuanzisha Miradi ya Huduma za Afya ikiwemo KCMC kule Kilimanjaro , Hydom kule Manyara, Kuimarisha Huduma za Elimu Seminary Morogoro, Agape Moshi, Kisarawe Seminary Na Vyuo vya Tumaini Makumira Arusha, Dar es salaam nimetaja vichache .

Lakini katika Enzi hizi Hebu tazama hizi Huduma ziko katika Hali gani leo KCMC Moshi utasikia Kuna Rushwa, Shule za Seminary zinajikongoja, tazama Vyuo vya Tumaini Iringa imeshajitenga haiko tena pamoja Na vingine , utajiuliza kwanini hizi changamoto jibu huenda likawa Viongozi Wanaacha Utume wao Na kutazama Utume wa wana Siasa kina Kaisari.

Changamoto ziko sehemu zote , serikalini na katika Kanisa Cha msingi Huu sio wakati wa kuandikiana Manyaraka Bali Ni wakati wa kila taasisi kupambana katika kutatua changamoto zake pasipo kumnyooshea mwingine kidole.

Ombi:Kanisa lenu siku zote lijitahidi kulinda sifa yake halisi ya Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania(KKKT),na kamwe lisikurupuke na kukimbilia mambo yasiyowahusu.La sivyo hiyo KKKT tuijuayo inaweza kuleta maana tofauti na ile iliyozieleka.Watu lazima wajue kutofautisha kati ya KKKT ya Kanisa na hizi KKKT zingine zikiwemo Kichwa Kidogo Kuliko Tumbo au Kataa Kutumiwa Kijinga Tafadhali.Maana Hizo zote hizo ni KKKT.

*Niwatakie Pasaka Njema Wote, kila mtu Na atimize Wajibu wake*.

Ni Mimi Eliamlingi John Kanyoselo,
PHD Candidate/Mwanafunzi wa Masomo ya Uzamivu,
Taras Shevchenko National University,Kiev.
Russia
 
Acha ukuda wewe!! Tangu lini ukaitwa Kanyoselo?? Tangu ulienda Urusi?? Mbona huna uwezo wa kusoma PhD??
 
PhD zimevamiwa na matahiri miaka hii kama huyu mleta mada
 
Tanzania tunashindwa kuendelea kwa sababu ya watu wenye akili za kipuuzi kama zako wewe mtoa mada. Toa waraka wako tuone utakachoandika.
Na usisahau kuelezea serikali yako inavyotaka kulazimishwa kupendwa.
Watanzania wa sasa sio kama wa zamani. Nimefurahishwa na maaskofu kwa sababu wamefunua kilichopo kwenye jamii, kazi kwenu mnaolazimisha watu wawapende
 
Hekima ya Kitume? Huko Congo DRC maaskofu walikuwa na hekima ya kitume mpaka walipoona hali inakuwa mbaya hawakuwashawishi wananchi wala kuandika waraka ambao wewe umeuchukia sana. Bali wao wenyewe waliingia barabarani kuupinga utawala wa Kabila na ubabe (udicteta) wa kutaka kusalia madarakani.

So sipendi tufike huko hata siku moja. Lakini watu tutambue safari ni hatua. Hatua tulipofika sasa kwamba kila dhehebu linaipinga serikali ni hatua mbaya. Tusishangae kuona wahubiri wakihubiri wazi wazi kuwashawishi wananchi.

Bado serikali ina wajibu wa kukaa vizuri na viongozi wa dini. Kwa madhehebu mengine sawa. Lakini kwa Maaskofu wa Kikatoliki kusema yale ni kwamba hali imekuwa mbaya. Tena wanampinga Kijana wao Muumini wao.
 
ASKOFU SHOO: VIONGOZI WA DINI WASIZIBWE MDOMO KUTEKELEZA WAJIBU WAO

askofu-shoo-300x149.jpg

Na Upendo Mosha, Moshi

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo ameonya kwamba asitokee kiongozi yeyote nchini wa kisiasa au serikali ambaye atajaribu kuwazuia na kuwaziba midomo viongozi wa dini kutekeleza wajibu wao wa kukemea na kuonya juu ya maovu yanayoendelea hapa nchini.

Dk. Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, pia amesema kamwe kanisa halitanyamaza kimya kwa wanasiasa wenye tabia ya kutumia nafasi zao kuligawa taifa vipande vipande.

Akizungumza kwenye ibada maalumu ya kusataafu kwa aliyekuwa Mchungaji wa Usharika wa Masama Kati, John Mshau wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

“Wajibu wa viongozi wa dini ni kuonya na kukemea yale mabaya yanayoendelea nchini na si vinginevyo na kwamba asijaribu kutokea mtu yeyote kuwazuia viongozi wa dini kufanya wajibu huo kwani ni sawa na kupingana na Mungu.

“Wajibu wetu ni kuonya, kushauri, kukemea na tunatenda hivyo, asijaribu kuja mtu yeyote kutuzuia kufanya hivyo kwani neno la Mungu linasema bwana hutegemeza wenye upole na huangusha chini wenye hila, hivyo sisi kama viongozi wa dini hatutakubali kunyamaza tutasema na kukemea maovu,” amesema

Pamoja na mambo mengine, Dk. Shoo amewaonya viongozi wote wa kisiasa nchini kuacha kutumia vyama vyao kuligawa taifa na kwamba suala hilo halitaweza kuvumiliwa na viongozi wa dini na wataendelea kusema na kuonya.

Akitolea ufafanuzi waraka ulioandaliwa na Baraza la Maaskofu 27 wa KKKT, Machi 15 Jijini Arusha ambapo walifunga na kuomba Mungu kwa lengo la kupata ujumbe sahihi ili wautoe kwa waumini wa kanisa hilo na Taifa kwa ujumla na kwamba hawakukurupuka kutoa ujumbe huo.

Nimesoma Waraka wa MAASKOFU Mara mbili, nikarudiamara ya tatu.Kwanza nianze kwa kukupongezeni kuwa mumetimiza wajibu wenu wa kutumia demokrasia ya uhuru wa kujieleza sawasawa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa namna fulani,ama kwa makusudi au kwa kutokujua kuna mambo muhimu hamjayagusia.

Nafikiri kwamba ilihitajika tafakari fulani kwa upande wenu kabla ya kuutoa ule waraka sawasawa na lile andiko/usemi wa BORITI na KIBANZI.

Kwa maana hiyo sasa naomba nijitolee kutoa ulimu kwa MAASKOFU wangu kama wanavyotoa Elimu ya Ufalme wa Mbinguni kwetu.

Kwanza naomba ifahamike kwamba katu sina madaraka ya kimbingu ya kuweza kuwajibu wapakwa Mafuta wa Bwana Mungu ila hiki ninachofanya hapa ni kuwaelimisha tu kwenye hili eneo ninalolimudu la Kaisari ambako ninyi wenyewe kwa hiari yenu mmeamua kuvuka ng'ambo na kulifuata huku mkijua fika kuwa Ya Mungu tunastahiki kumpa Mungu na ya Kaisari nayo yana wenyewe.

1. Hoja kubwa ambayo mmeizungumza kwa Umakini Ni suala la Katiba Mpya.
Majibu , kwanza mchakato wa katiba mpya ulianzishwa kwa Utashi wa Rais Kikwete ambaye anapaswa kukumbukwa kwa hili Aliona Mbele Sana , Mchakato haukukwamishwa na Serikali ya Magufuli au Kikwete ukweli Ni Huu hapa

" Nakumbuka katika Bunge la Katiba maaskofu walishiriki bunge la katiba ambapo bunge liliamua kwa wingi katiba pendekezwa unapotaka tuachane na maamuzi ya bunge na uhuru wake mbona tena unaenda kinyume na hoja zako bunge lipewe uhuru?? Maamuzi Yale yalifanywa kwa mujibu wa sheria je tunataka kujenga utamaduni wa kutoheshimu katiba na sheria?? Maamuzi Yanapofanywa na wengi hata kama mimi nawewe haturidhiki, ndio demokrasia yenyewe !!! Kwa mujibu wa sheria kilichobakia ni wananchi kupiga kura,na endapo kama wana hoja mbadala basi wasubiri wakati huo badala ya kuturudisha kujadili rasimu ya Warioba as a matter of principle .

2. Hoja Ingine ilikuwa hali ya Siasa.Hoja za MAASKOFU Ni kuminywa kwa Demokrasia , Kumwagika Damu , kushambuliwa kwa Risasi Na watu kuokotwa wakiwa wamekufa .
Majibu , kwa Taifa lenye watu zaidi ya Milioni 50 usitegemee watu wote watafurahi Na kuridhika Na utawala Huu, diversity ni Muhimu Sana katika masuala yanayojenga taifa lakini tunashuhudia Siasa yetu ikianza kuingiliwa Na mataifa ya ulaya kupitia Baadhi ya wanna Siasa wenye ulafi Na tamaa ya fedha Na madaraka , katika hili tusitazame Serikali tu pia twende mbali tutazame mbinu wanazotumia hao watu wa nje wanaotamani rasilimali zetu ,tutazame Mahusiano yao Na wanasiasa wetu, Na mwisho tujifunze kuviachia Kazi vyombo vyetu ambavyo kisheri ndivyo vyenye jukumu la kuchunguza; suala la muda wa uchunguzi Ni muhimu Sana lakini tuvute subira Mana Kanisa la KKKT halina utaalamu Na masuala ya ulinzi Na Usalama.

Katika hii hoja nisema Jambo japo litauma kidogo, hata katika Kanisa la KKKT tumeshuhudia Na nyinyi mkimwaga Damu kule Dayosisi ya Meru mkigombea madaraka au mmesahau jamani?Ikiwa kanisani tu mnafikia mahali mnagombania Wamachame na Wakibosho?Sembuse huku kwa Kaisari kulumbana hapa na pale kwa ajili ya siasa?Anyway huko nidingependa kwenda sana maaskofu wangu.

- Kama ni Ufisadi ambao Magufuli anapambana nao Na nyinyi Msisahau pia kutumbia ufisadi na wizi mkubwa wa Mali za kanisa kupitia hotel ya KKKT Arusha ambayo mpaka sasa imeingiza waumini katika matatizo makubwa ya Kiuchumi Mana zile Ni mali za waumini.Kanisa lijitahidi mno kuishi sawasawa na matarajio ya umma na matakwa ya mwenyezi Mungu.

- Kama ni Polisi kutumia nguvu kubwa katika Jamii, kumbukeni Na nyinyi pia kutumia mgogoro wa kuwaweka ndani wachungaji wa KKKT kule Njombe uliofanywa na askofu Mengele,kufunga milango ya kanisa pale Mafinga na kutaka kumfukuza mkuu wa Jimbo Mch Kipangula , Hali hii imesababisha hadi Leo Jimbo la Mufindi kujitenga na Dayosisi ya Kusini na kuwa nchini ya uangalizi wa Dayosisi ya Iringa , hii inaonyesha Roho ya Vurugu Na Machafuko iliyopo ndani ya Kanisa kilo kwahiyo tunachokiona kwa jamii ni matokeo ya matatizo yaliyoanzia Kanisani tutafakari hapa kidogo.

- Nimesoma Waraka mnalalamika kuhusu fedha za Serikali kutumika kununua madiwani.Jamani MAASKOFU wangu mnajua hii Roho Na pepo la rushwa limeanzia Kanisani kwenu jamani, hivi hebu tuambieni matatizo ya ukabila,ukanda rushwa inayotajwa vilivyotamalaki katika uchaguzi wa kupata mkuu wa KKKT aliyestaafu na huyu wa sasa , hivi mmesahau Kampeni zilizokuwa zinafanywa kama vile mnagombea Ubunge Na udiwani mnakumbuka Kwanini Askofu Alex Gehazi Malasusa alivyopitishwa Kuwa Askofu Mkuu pasipo yeye Kuwa Mgombea?Hi ilitokana Na kushindwa kupatikana kwa Askofu kwa njia za Kidemokrasia baada ya Mapapa Wawili kushindana bila muafaka ndio ikatumika Busara ya kumchagua Baba Askofu Malasusa kuziba Mpasuko.Je hapa tunaruhusiwa kuhisi kwamba sasa Maaskofu mmeichukua hoja za chama fulani cha upinzani na kuzifanya ni za kanisa?Je mnataka sasa sisi watu wa mwilini tuamini hilo la kwamba chama hicho kina uhusiano wa karibu mno na kanisa hilo hasa Dayosisi za Kaskazini?

- Mmezungumzia kuhusu Migogoro ya Wafugaji Na wakulima, Migogoro ya Kisiasa, jamani hebu Na Ninyi Maaskofu Msisahaua kutuambia hali mbaya ya kikanisa huko Mtwara na mgogoro ndani ya Kanisa chini ya Askofu Mbedule ambao umesabaisha Kanisa kufungwa Na kufunguliwa Tena,ila mpaka Sasa bado Kuna changamoto .

- Nimeusoma waraka vizuri,Mimi Ni mluteri maisha yangu yote sijawahi kuona kipindi kigumu katika kanisa kama hiki , unapotazama Changamoto zinazoikabili serikali utaona nyingi zimeanzia Kanisani Na Sasa zimeanza kutoka kwenye jamii.

- Leo ukiuliza baadhi ya Wachungaji wenu wanasema Tumekuwa na viongozi wasaka madaraka na kugombania vyeo ,kumekuwa na rushwa na wizi wa kutisha pamoja na manyanyaso ndani ya Kanisa, Sasa kama hivi viko ndani ya Kanisani unategemea nini huku kwenye jamii maana waumini wenu ndio hao hao wananchi na wana Siasa.

Siku zote naamini Ibada njema inaanzia nyumbani

Pia tusisahau hadithi ya Yesu juu ya Kibanzi vs Boriti

Mwisho nimalizie na mambo mawili.
1. Kwanza kama Kanisa la KKKT lina issue na serikali si waombe kukutana na viongozi wa serikali? Mbona JPM kaenda makanisani kwao kusali si wangemwambia Mheshimiwa subiri tuna maongezi ya faragha baada ya ibada wakaongea??iweje tulumbane hadharani kwa kigezo Cha mnatimiza wajibu wenu kwa kusema , Haki lazima iende Na wajibu .

2. Kuendelea Kutoa Waraka kama huu Ni kuzidisha Mpasuko was Kanisa Na Serikali ambao unanufaisha upande mmoja wa Siasa za Upinzani hivyo Msitarajie Serikali ya chama kingine itakaa kimya , lakini pia inachafua Nchi yetu katika medani za Siasa za Kimataifa Na mashirikiano Mema Na mataifa mengine .

Hivi Enzi za Baba Askofu Mkuu Mstaafu wa KKKT Samson Mushemba hapakuwa Na changamoto kama hizi katika Jamii?Naambiwa zilikuwepo Nyingi Sana ila Askofu Mushemba Alitumia Hekima Kuu katika Utume wake kushughulikia Changamoto hizi katika Hali ambayo ilileta Utengamano wa Kanisa Na Serikali Na ndio Mana hatukuona haya tunayayaona Sasa.

Nakumbuka wao walipambana kuimarisha Huduma za Kiroho Na haswa Injili ambayo ndio msingi Mkuu wa Kanisa la KKKT Na pia kuimarisha Huduma za Kijamii mfano Kuendeleza Na kuanzisha Miradi ya Huduma za Afya ikiwemo KCMC kule Kilimanjaro , Hydom kule Manyara, Kuimarisha Huduma za Elimu Seminary Morogoro, Agape Moshi, Kisarawe Seminary Na Vyuo vya Tumaini Makumira Arusha, Dar es salaam nimetaja vichache .

Lakini katika Enzi hizi Hebu tazama hizi Huduma ziko katika Hali gani leo KCMC Moshi utasikia Kuna Rushwa, Shule za Seminary zinajikongoja, tazama Vyuo vya Tumaini Iringa imeshajitenga haiko tena pamoja Na vingine , utajiuliza kwanini hizi changamoto jibu huenda likawa Viongozi Wanaacha Utume wao Na kutazama Utume wa wana Siasa kina Kaisari.

Changamoto ziko sehemu zote , serikalini na katika Kanisa Cha msingi Huu sio wakati wa kuandikiana Manyaraka Bali Ni wakati wa kila taasisi kupambana katika kutatua changamoto zake pasipo kumnyooshea mwingine kidole.

Ombi:Kanisa lenu siku zote lijitahidi kulinda sifa yake halisi ya Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania(KKKT),na kamwe lisikurupuke na kukimbilia mambo yasiyowahusu.La sivyo hiyo KKKT tuijuayo inaweza kuleta maana tofauti na ile iliyozieleka.Watu lazima wajue kutofautisha kati ya KKKT ya Kanisa na hizi KKKT zingine zikiwemo Kichwa Kidogo Kuliko Tumbo au Kataa Kutumiwa Kijinga Tafadhali.Maana Hizo zote hizo ni KKKT.

*Niwatakie Pasaka Njema Wote, kila mtu Na atimize Wajibu wake*.

Ni Mimi Eliamlingi John Kanyoselo,
PHD Candidate/Mwanafunzi wa Masomo ya Uzamivu,
Taras Shevchenko National University,Kiev.
Russia
 
ASKOFU SHOO: VIONGOZI WA DINI WASIZIBWE MDOMO KUTEKELEZA WAJIBU WAO

askofu-shoo-300x149.jpg

Na Upendo Mosha, Moshi

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo ameonya kwamba asitokee kiongozi yeyote nchini wa kisiasa au serikali ambaye atajaribu kuwazuia na kuwaziba midomo viongozi wa dini kutekeleza wajibu wao wa kukemea na kuonya juu ya maovu yanayoendelea hapa nchini.

Dk. Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, pia amesema kamwe kanisa halitanyamaza kimya kwa wanasiasa wenye tabia ya kutumia nafasi zao kuligawa taifa vipande vipande.

Akizungumza kwenye ibada maalumu ya kusataafu kwa aliyekuwa Mchungaji wa Usharika wa Masama Kati, John Mshau wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

“Wajibu wa viongozi wa dini ni kuonya na kukemea yale mabaya yanayoendelea nchini na si vinginevyo na kwamba asijaribu kutokea mtu yeyote kuwazuia viongozi wa dini kufanya wajibu huo kwani ni sawa na kupingana na Mungu.

“Wajibu wetu ni kuonya, kushauri, kukemea na tunatenda hivyo, asijaribu kuja mtu yeyote kutuzuia kufanya hivyo kwani neno la Mungu linasema bwana hutegemeza wenye upole na huangusha chini wenye hila, hivyo sisi kama viongozi wa dini hatutakubali kunyamaza tutasema na kukemea maovu,” amesema

Pamoja na mambo mengine, Dk. Shoo amewaonya viongozi wote wa kisiasa nchini kuacha kutumia vyama vyao kuligawa taifa na kwamba suala hilo halitaweza kuvumiliwa na viongozi wa dini na wataendelea kusema na kuonya.

Akitolea ufafanuzi waraka ulioandaliwa na Baraza la Maaskofu 27 wa KKKT, Machi 15 Jijini Arusha ambapo walifunga na kuomba Mungu kwa lengo la kupata ujumbe sahihi ili wautoe kwa waumini wa kanisa hilo na Taifa kwa ujumla na kwamba hawakukurupuka kutoa ujumbe huo.
Hakika WACHAGA mmeamua kwa Udi na Uvumba kuleta mchafuko na kuharibu Amani hapa Nchini.
Ila Mungu ni wa Watanzania wote. Hakika mtashindwa katika Chuki, uadui, Roho mbaya, hila, ufedhuli, ubazazi, ujambazi, UNYANG'AU, Uhaini, wizi wa Mali za umma, kufarakanisha watu, Majungu, n.k.

Laana ya kumwaga Damu kila mwisho mwaka inawatafuna taratibu. Mwisho wenu ni mbaya sana.
 
Acha uoumbavu na ukabila wewe. Si kila mtu ambaye anamlaani huyu dhalimu ni mchagga. Na wachagga wameharibu vipi amani ya nchi na kuleta machafuko nchini!? Wachagga wamemteka nani, kumtesa na kumuua? Wachagga lini wamedharau katiba, mahakama, Bunge, sheria za nchi, kuminya uhuru wa Watanzania na vyombo vya habari? Acha ujuha wako humu kama huna cha maana cha kuandika kaa kimya badala ya kuandika upuuzi humu.

Kaa kimya ngumbaru wewe! Mliyofanya kwa Taifa hili yanatosha. WACHAGA mnajiona kama mna Hati miliki na Tanzania hii. Shame on you! Na ndio maana mnanyooshwa na kukimbilia katika karata ya UDINI. Maana huko kwingine kote mlishashindwa kitambo tu. SHAME ON YOU NA KIZAZI CHAKO CHOTE.
PATHETIC!
 
Naona mnahangaika tu kazi kuandika pumba. Jamaa wamewapa dozi mntapapa tu. Bado 26 April tuliamshe dude naona mntakufa kwa HBP.
 
1. Kwanza kama Kanisa la KKKT lina issue na serikali si waombe kukutana na viongozi wa serikali? Mbona JPM kaenda makanisani kwao kusali si wangemwambia Mheshimiwa subiri tuna maongezi ya faragha baada ya ibada wakaongea??
Aisee! PHD candidate... Kazi kweli kweli.
 
Shida yako ulitaka tujue kama upo unasomea PHD tena Russia mkuu. Hivi nasikia huko ni mkwanja tu unatunukiwa Ma PHD ndo maana wabongo ambao mambo si shwari upstairs hukimbilia huko kujipatia ganda la ndizi, tudhibitishie hili kwanza hao maaskofu wamedhibitisha tayari mambo waliyo yaona.
 
Back
Top Bottom