Kweli nakubaliana na wadau kuwa hekima na busara yana maana zinazokaribiana sana. Unaweza kuyatumia kama "synonyms"-(naomba neno lake la kiswahili kama unajua). Ingawa wapo wanaodhani kuwa hekima mara nyingi mtu huzaliwa nayo ilihali busara mtu hujifunza kutokana na mazingira anayoishi. Inawezekana ikawa kweli lakini bado haitoshi (nionavyo mimi) kuwa tofauti kubwa sana.