Hekima, busara na uongozi bora wa CCM na Magufuli ndizo zitatuvusha hapa. CCM na Rais Magufuli ni hazina, tunu na rasilimali muhimu kwa Tanzania.

Nakubaliana sana na wewe .
Uchumi wa makada na watawala wa CCM unakua kwa kazi sana mifukoni mwao .

Nimejaribu kuangalia misafara yao na aina ya magari wanayotembelea na umaskini wa nchi ya Tanzania ,hakika wamedhamiria kabisa kuishi maisha ya anasa na starehe kwenye nchi hii maskini.

Nilichogundua ni kuwa Wanaoumia ni wengi lakini wachache wameamua kuirithi nchi kwa nguvu ndio maana hawataki ushindani wa haki wa kisiasa.
Kama wanafanya mambo mazuri basi wasimamie haki kwa wote sio kubaki na maneno majukwaani huku umaskini ukiwa mkubwa kwa wengi na wachache wakistawi kwa kodi za wananchi na kujisifu kuwa uchumi umekua kiasi cha kuongeza michepuko .
Hayo ndio maendeleo ndani ya mifuko yao .
 
Umepoa sana....
IMG-20190501-WA0017.jpg
 
Hekima ni uwezo wa kutumia maarifa uliyonayo kwa ajili ya kuzalisha matokeo chanya katika jamii. Biblia na Quran vinasema kuwa hekima inatoka kwa Mungu mwenyewe. Katika Biblia, kitabu cha Yakobo 1:5 inasema’ lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu wala hakemei;naye atapewa’. Katika Biblia, tunaona chanzo cha hekima yote ya mwanadamu ni Mungu mwenyewe na akimuomba MUNGU anapewa. Rais Magufuli ana hofu ya Mungu, na mtu mwenye hofu ya Mungu ana hekima.

Watu wenye hofu ya Mungu, busara na hekima ndio waliowaongoza wana wa Israel kwenda nchi ya ahadi. Joshua alikuwa na hofu ya Mungu, hekima na busara na Mungu alimwambia hivi’ Musa mtumishi wangu amekufa,sasa jitayarishe, vuka mto Yordani pamoja na watu hawa wote , mwingie katika nchi ambayo ninawap’ ( yoshua 1:1,2). Hapo tunaona kwamba Mungu alimchagua Yoshua, baada ya kifo cha mtu wake ili awavushe watu wake. Leo hii jukumu hilo anapewa Rais Magufuli la kutuvusha katika haya. Hakika tutavuka.

Huo ni mtazamo wa biblia katika kuelewa ni namna gani kiongozi mwenye hofu ya Mungu, mwenye hekima na busara anapewa jukumu la kuwavusha wengine na ndiyo maana nina mtazamo kama huo kwa Rais wetu wa kutuvusha kama Joshua alivyopewa jukumu hilo.

Tuangazie mtazamo wa kibinadamu, ni kivipi Rais Magufuli atatuvusha.

Rais Magufuli ni kiongozi mwenye maono, na kupitia kwa maono hayo na utekezaji wake ni kutimia kwa ndoto ya kuwa uchumi wa kati kufikia 2025. Si rahisi hata kidogo lakini matumaini yapo na yatatimia. Dhoruba ni nyingi lakini tanga lipo imara, ngarawa haiyumbi inatembea. Kupitia kwa maono hayo tutavuka, hakika tutavuka.

Uongozi wa mfano wa Rais Magufuli na CCM. CCM ni chama chenye kuonesha dira na muelekeo wa muda mrefu. Uongozi bora wa CCM umekuwa kama dira kwa taifa hili. Mipango, mikakati na sera za kichumi iliyopo chini ya CCM ni Imani tutavuka. CCM kimebeba matumaini ya watanzania na moja ya tumaini hilo ni kuhakikisha nchi inakuwa na uchumi wa kati kwa kutekeleza kwa nguvu sera na mipango. Hakika uongozi bora wa CCM utatuvusha hapa tulipo.

CCM na Rais Magufuli ni tunu, hazina kubwa kwa Tanzania kuelekea uchumi wa kati. Rais Magufuli ni kiongozi mwenye maono na mzalendo, ambapo maono hayo ni rasilimali muhimu ya kutuvusha na kuvuka na CCM ni chama chenye uongozi bora ambao unatumika kuandaa viongozi bora kama Magufuli kwa hiyo mchanganyiko wa CCM na Rais Magufuli ni kutimia na kutekelezeka kwa ahadi ya UCHUMI WA KATI. Hekima na busara zikiwemo kwa kiongozi, zinamsaidia kufanya mambo makubwa na kwa kuwa Rais wetu anavyo, tutegemee mambo makubwa kwa Tanzania.

Ukome kuitaja Quran kwenye vitu vya kijinga
 
Back
Top Bottom