Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 2,235
- 4,382
Kwenu Wanajema,
****
Picha ya George Soros
Huu ni uzi mchungu kwa wanaCCM wengi vitatange, kwa sababu nagusia anguko la CCM ambalo nimelichambua na kuliona.
****
Picha ya George Soros
Kwa wafuatiliaji wa medani za nchi za magharibi na watu wake, George Soros sio jina geni kulisikia. Ni mmoja wa watu waliobahatika kuugusa usukani wa kuendesha matukio makubwa kwenye nchi za magharibi na ulimwenguni kwa karibu karne moja iliyopita, akijumuishwa kwenye ulingo wa akina John D. Rockefeller, John Peirpont Morgan na wengineo wa kariba yao kama kina, Rupert Murdoch na Michael Bloomberg ambao walianzisha vyombo vya habari vya kueneza propaganda ulimwenguni, mtakumbuka ile habari ya shilingi ya Tanzania kuitwa 'World's worst currency' ambayo ilichapishwa na gazeti la Bloomberg.
Ukiachilia kuwa Hedge Fund Manager mwenye record nzuri Wall Street, akipata umaarufu mkubwa mwaka 1992 baada ya Hedge Fund yake ya Quantum Fund kupata faida zaidi ya $1 Billion ndani ya siku moja; Soros ni mchumi hodari sana kwa kiwango cha Phd, ni mwanafalsafa mfuasi wa mwanazuoni nguli Karl Popper (mwanafalsafa wa ki Austrian ambaye alikuwa mpinzani mkali wa tawala za ki communist kupitia maandiko yake - andiko lake maarufu likiwa ni kitabu cha Open Society and Its Enemies alichokitoa mwaka 1945, miaka 3 kabla ya UN Human Rights Charter, ambayo ni moja ya maagano Tanzania imeingia na dunia)
Ni kupitia maandiko ya Karl Popper ndipo George Soros alianzisha Open Society Foundation ambayo ilikuwa inafadhiliwa na utajiri wake mkubwa uliotokana na faida za Hedge Fund yake ya Quantum Fund. Na lengo kubwa la Soros kuanzisha hii foundation ilikuwa ni kwa ajili ya kuvunja misingi ya ki-communist katika nchi za ulaya mashariki ambazo zilikuwa bado ni closed societies kwa miaka ya 1980s na 1990s na lengo lake lilikuwa ni kuvunja hiyo mifumo ili ku transform hizo nchi kuwa Open Societies.
Huu ndo ulikuwa mwanzo wa Soros kushirikiana na globalists wenzake na hata intelligence systems kama CIA kuanza kufadhili mapinduzi na kutengeneza mapinduzi kwa kutumia mbinu mbadala au hata chafu pale inapobidi. (Na ndio hii ilitengeneza ile conspiracy kwamba George Soros anatumika kuangusha serikali za dunia zinazopingana na Marekani, zenye mirengo ya ki-communist, na serikali za mabavu na kidikteta).
George Soros na utabiri wa anguko la kampuni, mfumo wa utawala wa nchi etc
Katika moja ya maandiko ya Soros, aliweza kuja na Theory yake inayoitwa 'Theory of Reflexivity' ambayo kwa mara ya kwanza iliweza kumsaidia kupata faida kubwa akiwa Hedge Fund manager kwani aliweza ku-apply hii theory kutabiri anguko la makampuni na hii ikamfanya kuwa mbele ya muda na kufanya maamuzi sahihi ambayo yalimpatia faida kubwa baadae kupitia kuuza na kununua hisa.
Baadae kabisa wakati anajiingiza kikamilifu kwenye kupambana na serikali korofi zenye mirengo ya kikomunist na kidikteta, aliweza kuitumia Theory of Reflexivity kutabiri anguko la mfumo wa utawala wa nchi, hivyo kumuweka mbele ya muda wa kujua ni wakati gani sahihi wa kuanzisha harakati zitazopelelea anguko la mfumo mzima wa utawala.
Dhana pana ya Theory of Reflexivity ni kwamba kuna muunganiko wa matukio mengi katika kutokea tukio moja kubwa. Mfano; kuanguka kwa kampuni sio tukio la kama embe kuanguka juu ya mti, ukichunguza utakuta kuna matukio mengi kabla ya kuanguka kwa kampuni yanayotokea hata miezi 24 kabla, waweza kuta mashine zimezeeka, viongozi wa kampuni wabovu, wafanyakazi wavivu, ubora mbovu wa bidhaa sokoni etc etc. Kwa kutumia uchambuzi yakinifu, ukiweza kudadisi hayo mambo madogo madogo, yaweza kuwa rahisi kujua hii kampuni itaweza kufa ndani ya muda gani au itaweza kuinuka baada ya muda gani, hivyo utajikuta kwenye kunufaika ikiwa wewe ni mwekezaji katika ulimwengu wa hisa.
Vivo hivo kwa mfumo wa utawala wa nchi, haudondoki kama embe liangukavyo juu ya mti, anguko la mfumo wa utawala ni muunganiko wa matukio meengi madogo madogo ambayo yanaweza kujionesha hata miaka mitano kabla ya anguko rasmi kutokea. Na matukio hayo madogo madogo yakiwa timilivu, anguko huwa halikwepeki.
Baada ya kuzichambua hekaya za George Soros; kwa kutumia Theory of Reflexivity nikajikuta nauchambua mfumo wa siasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na nikagundua ya kwamba CCM ni chama ambacho kipo kwenye hatua za mwisho kabisa kukaribia anguko kwasababu kuna mambo kadhaa yameshajidhihirisha tayari na ni ngumu kwa CCM kukwepa kikombe cha anguko.
Nimefanyia tafiti sababu 6 kubwa (haimaanishi zipo 6 tu) bali kwa macho yangu ya kiuchambuzi, nimeziona 6 muhimu kwa sasa
1. Hakuna Strategists katika ngazi kubwa ya uongozi, strategists ambao ni nguzo ya kufanya maamuzi ya manufaa kwa kuangalia trend ya matukio hata miezi 24 ijayo.
Hata bila kukubali, ni wazi CCM wamevurugwa na 'no reforms, no election', ni mtego mbaya sana kwao, lakini ukijiuliza vema, wangeliweza vizuri kuukwepa mtego huu kwa kuwahadaa wapinzani kwa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 huku wakiangalia kuiba uchaguzi wa 2025, ikiwa wangegawa demokrasia kidogo. Unavyoona akili zilizotumika 2024 za ku 'Take All' badala ya 'Trade Off' inakuambia kabisa kwamba hakuna strategist wa kusoma nyakati zinataka nini. Labda mimi nakosea pia, yawezekana CCM kuna strategists, ila sio watoto wa mjini kama kina Abdulrahman Kinana au Edward Lowasa ambao wao lugha ya 'Trade Off' yaani - mwachie mwenzako naye ale kidogo ili na wewe uweze kula kwa amani, ni msingi ambao wanaitambua vema kwasababu huwezi kufanikiwa mjini ukiwa mbinafsi na mchoyo kwa wengine. Baada ya ujio wa Magufuli na kujiweka pembeni kwa watoto wa mjini kina Kinana et al, ni wazi kabisa kwamba strategists wa CCM yawezekana kabisa imetawaliwa na washamba wa kijijini ambao wao, ushindi maana yake ni 'Chukua Chote Kilichopo' kwasababu saikolojia ya mshamba imeathiriwa na ugumu wa maisha ya kijijini, hivo yeye, lugha ya kugawa kidogo haipo kichwani mwake
2. CCM ya sasa haina King Makers kwenye majukwaa ya kisiasa. Hii haihitaji mfano halisi zaidi ya alichokuwa anaongea CPA Amos Makalla kwamba Chadema wanapanga kuleta Ebola nchini, ilinichekesha sana. Huwezi kuzishinda hoja za upinzani kwa hoja nyepesi hivi. Ni kiashiria pia cha kwanini CCM imekuwa inapata shida sana kipindi cha kampeni, kuanzia 2010 mpaka 2020, uwezo wa CCM kusimama majukwaani ni kama umezorota kwa kiwango kikubwa. Na haiwezi kuwa tofauti hata sasa 2025, ikiwa una viongozi waandamizi kama kina CPA Makalla wanashambulia jukwaa kwa hoja za kiwango cha ndondo cup wakati wapo ligi kuu. Kukosa Kingmakers majukwaani, maana yake ni kwamba CCM imekuwa inakosa watu wa ku match tempo ya wapinzani hodari wa majukwaa kama kina Lissu. Hii maana yake ni kwamba, CCM imejikuta wakati wote ikiwa kama follower badala ya leader, na hii inawafanya CCM kujikuta wakikimbiza upepo wa Chadema kila wakati. Hii ina fit very well narrative ya CCM gradual decay. Hakina King Makers majukwaani, hakina tena ushawishi kwa watanzania.
3. Youth wing ya chama - UVCCM ambayo pia ingepaswa kuwa lifeblood ya chama, yaani kiwanda cha kutengeneza hoja mpya, imetengenezwa kiuchawa bila kujali competency, democratic and meritocratic process.
Kwa miaka ya karibuni, UVCCM imejikuta kwenye mkondo wa uraibu wa kuwa na viongozi waliopatikana kwa busara za majina ya mfukoni ya wakubwa wa chama. Hii imewanyima UVCCM fursa ya kuenjoy magical power of democracy ambayo ingeweza kuwasaidia wao kupata uongozi wenye meritocracy, kwani kuna msemo, 'macho ya wengi ni jicho la Mungu'. Hii maana yake ni nini? Kwakuwa UVCCM ina uongozi usiotokana na demokrasia na meritocracy process, maana yake hata wao wamejikuta wakikosa strategists na king makers wa majukwaa, kama ilivyo kwa wakubwa wao wa chama. Maana yake ni kwamba hata vijana wa CCM wamejikuta upande wa kuwa second rated dhidi ya vijana wa Chadema. Mathalani ukiangalia uwezo wa vijana wa Chadema wanapozijenga hoja na kuziongea, unaona utofauti ambao ni umbali wa mbingu na ardhi. Utofauti huu wa uwezo wa vijana wa CCM na Chadema, umekuwa ukiniogopesha sana kwasababu, mbali ya kwamba unaashiria kwamba CCM haina mustakabali wa kudumu, lakini kwa namna moja kunaashiria pia uwepo wa mstari mwembamba sana kati ya vitendo vya kuteka wapinzani na harakati za vijana wa CCM. Kwasababu kama huwakuti kwenye majukwaa ya kisiasa, na hawana uwezo wa kujenga hoja dhidi ya wapinzani, maana yake watabuni kila mbinu ya kuwafanya wawe relevant kwa viongozi waliowateua. Kwa logical thinking ya namna hiyo, maana yake huwezi kutenganisha UVCCM na vitendo viovu vya utekaji, kwasababu, uongozi wao haujatokana na meritocracy, na bila meritocracy hakuna sustainable system, hivo ni sahihi kuiweka hii kama kiashiria cha anguko la CCM.
4. Uongozi hauishi uhalisia wa utanzania na wanaCCM asilia,
Maisha ya viongozi wa sasa wa CCM sio aina ya viongozi wa CCM ya miaka ya 80 au 70, tofauti kabisa. Kama maisha yako yamejitenga na wao, unawezaje kusema wewe ni mmoja wao? Maana yake mfumo wa utawala wa CCM umetengeneza gap kubwa sana kati ya watawala na watawaliwa. Hii ina maana ya kwamba, CCM imepoteza mguso na wananchi walio wengi. Na unaweza kabisa kulithibitisha hili, pindi viongozi wa CCM wanapoenda kufanya ziara huko mikoani, yaani ile kufuru ya idadi ya magari ya kifahari na ile hali ya raia wananchi wa hayo maeneo, huwa inaniweka kwenye mshangao na majiulizo - maana raia ni wamechakaa na makobazi machafu vumbii, nguo ndo usiseme chafuu vumbi.
5. Too Big To Manage
CCM ina wanachama wengi na mali nyingi ambazo hazizalishi. Naweza kusema kwa hisia za ukweli kwamba, ukiondoa Kanisa Katoliki, yawezekana CCM ikawa taasisi ya pili kuwa na mali nyingi Tanzania. Mali za CCM ni mabilioni kwa mabilioni, lakini inahuzunisha kwamba mali hizo zimekuwa zikiwanufaisha wachache, hili watalitetea zaidi waliopo ndani ya CCM.
CCM pia ina mkusanyiko wa wanachama wengi ambao wamekuwa hawapo CCM kwa maana ya kuipambania agenda ya CCM bali wapo CCM kwa nia ya kuitumia CCM kama collateral na kinga dhidi ya uovu wao. Imejeuka kuwa kichaka cha kujificha waovu na wavunja sheria. Na watu hao hao ndo mara nyingi huitumia bendera ya CCM ndivyo sivyo. Bendera ya CCM sikuhizi imekuwa mbadala wa kibali cha ujenzi, unakuta mtu amejenga kiholela bila kufuata utaratibu, lakini unakuta ameotesha mlingoti wa bendera ya CCM.
Hii imeifanya CCM kuwa tafsiri halisi ya shamba la bibi. Kwa maana ya kwamba wanachama wa CCM wengi wapo hapo sio kwa mapenzi na CCM kama chama, bali kama chombo cha kufanya mambo yao binafsi yaende.
Hii hoja inaungana vema na hoja nne hapo juu, kwasababu wana CCM wengi wapo CCM kwa ajili ya masilahi yao binafsi, ni wazi kwamba, hawana mda wa kufikiria kuhusu strategy, kufikiria kuwa king makers wa majukwaa ya kisiasa, hawana interest ya ku practice democracy kwenye chaguzi za ndani, na hawawezi kuwa na uhalisia na raia wa chini. Na hii hoja namba 5 yaweza kabisa kuwa root cause ya hizo hoja nyingine 4 za juu.
6. Nguvu ya mitandao ya kijamii na ongezeko kubwa la idadi ya watu
Hii ni external force ambayo ndo inaenda kuizika CCM rasmi, hizo sababu 5 hapo juu ni internal forces ndani ya CCM. Kila hila na uovu wa CCM kwasasa imekuwa rahisi kuibuliwa na kujulikana kwa nguvu ya mitandao, hii inamaanisha hakuna kichaka cha kujificha kwa CCM kufanya hila zozote bila kujulikana.
Watabiri wanasema, baada ya miaka 15 ijayo, Tanzania itakuwa na watu kati ya milioni 100 mpaka milioni 120. Kwa wingi huo ambao wengi watakuwa ni vijana, aina ya mfumo huu wa utawala wa CCM hauwezi ku exist tena.
Mfumo huo utaweza ku exist at the expense of peace, kama tunavyoona nchi kama Pakistani ambayo ina idadi kubwa ya watu lakini hakuna amani ya kudumu.
Hitimisho
Kwa kutazama 'Theory of Reflexivity' ambayo nimeikopa kwa George Soros, sioni kama CCM ni chama chenye maisha marefu, japo sina ushahidi wa ni lini haswa anguko litatokea, ila ni vema kuweka kumbukumbu sawa. Japo imani yangu ni kwamba, miaka 15 ijayo itakuwa very rough years kwa CCM na sitoshangaa anguko likitokea ndani ya hicho kipindi.
Wasalaam
Mikopo Consultant.