Heka heka za JKT

Ukaridayo

JF-Expert Member
Oct 8, 2012
508
470
Zikiwa zimebaki siku 2 tu zoezi la uwasilishwaji wa maombi ya kujiunga na mafunzo haya ya JKT 2016 Kufungwa rasmi kwa mujibu wa fununu ktk wilaya ya kinondoni..

Leo nikiwa maeneo hayo ktk hekaheka zangu za kupigania nafasi hizo, tukiwa kwenye foleni nilipata kusikia story mob za hapa na pale kutoka kwa maraia tuliokuwa nao mahali hapo. Yupo raia mmoja ambaye daaa aliyekuwa anaelezea habari za huko mithili ya mtu aliyepata kushiriki huko, hatujui either kahadithiwa ama kaona Cd za mafunzo hayo...

Ilifika kipindi unajiuliza hivi kuna tofauti ya haya mafunzo ya sisi ambao tunajitolea (target) na yale ya wale vijana wa form six kwenda chuo???

Sijajua kama kwenye mikusanyiko kama hiyo kunakuwaga na watu waliowekwa kama huyu jamaa kwa ajili ya kuwaweka watu kwenye tension kali kiasi hicho!!!

Anachokizungumza jamaa huyu kuhusu hali ya mafunzo na changamoto za huko (zinatisha)... Unakuta mtu unatoka na mindset nyingine kabisa na kama ni kipaji cha kumfanya mtu ajipime mara 2x2 juu ya uamuzi wako basi jamaa anacho.

Wale vijana mliopata kushiriki haya fungukeni kwenye hili mana jamaa pamoja na kutuweka ktk tension ya juu naye alikuwa kwenye hekaheka zile zile za kuhangaikia maombi.
 
Mimi nilipangiwaga kambi arusha kiukweli kuna ka ugumu lakini kila kitu kitakuwa sawa na na Hakuna matatizo yoyote
 
kawaida sana na yote yatapita tu ndugu yangu. usianza kukata tamaa mapema kiasi hicho wakati hata kuchaguliwa bado.
 
Yanawezekana fungua moyo ,kunywa maji ,penda kaz za watu na mwisho mdomo wako ukusaidie kula nimetoka juz jkt na ninajilia vyangu 821 oyeeeeeee
 
ivi usaili wilaya ya kinondoni tayari wamemaliza jamani ? mi nataka niende j3
 
Kama umedhamiria kwenda JKT nakushauri usiogopeshwe na maneno ya watu. Kuna watu wanaeleza ukweli lakini pia kuna watu ambao upenda kukuza mambo. Mbona watu maelfu wamekwenda huko huko JKT na hatimae wakamaliza salama hayo mafunzo? Hao waliomaliza salama wana nini na wewe ushindwe una nini?

Mimi ni mmoja wa waliotishwa sana kwa maneno kuhusu JKT kipindi kile mafunzo yakiwa bado yanachukua mwaka mmoja kwa wale tuliokuwa tukijiunga kwa mujibu wa sheria baada ya kumaliza kidato cha sita. Sikujali. Nilikwenda, nikajionea niliyojionea, nikayakabili kama wengine na hatimaye tukamaliza salama. Pamoja na yaliyokuwa yakisemwa na pia yale niliyokabiliana nayo lakini bado kwa upande wangu JKT ni sehemu ambayo nili enjoy sana na kupata marafiki wengi ambao hata baada ya kutoka huko tumeendelea kusaidiana katika mambo makubwa kabisa ya kimaisha uraiani. Ni mwaka juzi tu nilifunga safari ya makusudi kabisa nikaenda kutembelea hiyo kambi yangu nilipomalizia mafunzo hayo, nikajieleza na nikakaribishwa kwa furaha kubwa na mkuu wa kambi pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa kambi hiyo na kisha kutembezwa hapo kambini kwa kufurahishwa na uzalendo niliouonyesha kwani sikuonyesha kuwa na chuki yoyote na JKT.

Kwa hiyo kwa ujumla ndugu yangu nakushauri u focus zaidi kwenye dhamira yako na usisikilize maneno ya watu ambao wanaweza kuwa na nia ya kukatisha tamaa wenzao.
 
Back
Top Bottom