PostGE2025 Heche: Watu wanahoji maridhiano, unaridhiana na nani? CHADEMA siyo tuvyama hutu twa mfukoni

PostGE2025 Heche: Watu wanahoji maridhiano, unaridhiana na nani? CHADEMA siyo tuvyama hutu twa mfukoni

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amesema watu wengi wanahoji kuhusu masuala ya maridhiano, akiuliza, “Unakaa na nani? Nakaa na mtu ambaye amemkamata mwenyekiti wako kwa kesi ya uongo.” Kauli hiyo ameitoa akielezea msimamo wa chama chake kuhusu wito wa maridhiano ya kisiasa nchini.

Heche ameongeza kuwa wananchi wanafahamu kuwa Tundu Lissu si mhaini bali ni mwanasiasa anayefanya siasa za upinzani dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Amesema Lissu hana nguvu ya kifedha wala mamlaka ya dola ya kupambana na vyombo vya usalama au kuipindua serikali, lakini bado amekamatwa na kuwekwa ndani. Aidha, amedai kuwa viongozi wengine wa chama hicho wamekamatwa, kufunguliwa kesi, na chama chao kuzuiwa kufanya shughuli za kisiasa ikiwemo mikutano na vikao.

Kutokana na hali hiyo, Heche amehoji uwezekano wa kufanyika kwa maridhiano ya kweli, akisema ni vigumu kufanya mazungumzo na watu wasiokubali kuwa wanawaonea au hata kuruhusu mikutano ya wazi. Amesisitiza kuwa CHADEMA siyo tuvyama hutu twa mfukoni, bali ni taasisi kamili yenye wanachama na wafuasi kuanzia ngazi ya kitongoji hadi taifa zima.

Video: Mwananchi Digital
 
Chadema haitakiwi meza ya maridhiano,inatakiwa kufutwa na viongozi wake kuhamishiwa jela
 
Back
Top Bottom