Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokradsi na Maendeleo (CHADEMA), John Heche akizunguma leo Novemba 19, 2025 amesema Tume ya kufanya uchunguzi wa uvunjifu wa amani wa vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025 iliyoundwa na Rais Samia siyo chombo huru kwani wajumbe wengi wa Tume hiyo waliwahi kuwa wafanyakazi wa Serikali ya chama tawala na pia ni wanachama wa CCM.
Aidha, Heche ameeleza kuwa haiwezekani Serikali inayotuhumiwa kufanya mauaji ndiyo inayounda tume kuichunguza, hivyo haki haiwezi kupatikana.
Pia Soma: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025
==
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuuarifu umma wa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kwamba haiitambui Tume ya Uchunguzi iliyoteuliwa na Ndg. Samia Suluhu Hassan, aliyejisimika madarakani bila ridhaa ya wananchi inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed Chande Othman, akiielekeza kuchunguza “matukio ya uvunjifu wa amani” yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
La kwanza na la msingi zaidi, msimamo wetu unatokana na ukweli kwamba mteuzi wa tume hiyo Ndugu Samia Suluhu Hassan hana uhalali wa kisiasa, kisheria na kimaadili.
Alijipachika Urais kupitia mchakato usio huru, usio wa haki, usio wazi na usiokidhi viwango vya kidemokrasia kama ambavyo walivyosema Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Afrika (UA) na wale wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Ndugu Samia hana mamlaka ya kimaadili wala kisiasa kuunda chombo cha kuchunguza uhalifu mkubwa uliofanywa na utawala wake dhidi ya raia waliokuwa wakidai haki zao za kidemokrasia na kikatiba.
Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi (Commissions of Inquiry Act, 2002: Chapter 32), tume ya aina hii ni chombo cha Rais, kinachofanya kazi kwa matakwa na maelekezo yake. Hata ripoti ya Tume, Rais ana mamlaka ya kuamua ichapishwe au isichapishwe, iwasilishwe hadharani au ifichwe.
Kwa mantiki hiyo, si chombo huru, na hakiwezi kutoa ukweli wala haki katika mazingira ambapo serikali ndiyo mtuhumiwa mkuu. Zaidi ya hapo, haiwezekani mtuhumiwa akajichunguza mwenyewe halafu tutarajie haki.
Serikali ya Samia ndiyo iliyoasisi, kuratibu na kutekeleza mauaji, utekaji, mateso, ubakaji, unyanyasaji na ukiukwaji mpana wa haki za binadamu. Wote walioteuliwa ndani ya tume hiyo waliwahi kuwa au ni watumishi wa Serikali na pia ni Wanachama wa chama anachokiongoza Ndugu Samia (CCM) jambo ambalo kimsingi linakiuka kanuni ya msingi kwamba tume huru haipaswi kuwa na uhusiano wowote na Serikali wala chama tawala.
Hawa wajumbe wakati wote wamekuwa sehemu muhimu ya kuiingiza nchi yetu kwenye maafa haya, na baadhi yao ni watuhumiwa wa kupanga na/au kutekeleza ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu wakiwa madarakani.
Hii si tume huru; ni njama ya kuficha ukweli, kufuta ushahidi na kuendelea kuwaumiza waathirika. Kinachoitwa “kuchunguza uvunjifu wa amani” ni mbinu ya kuwageuza waathirika kuwa wahalifu na kuwasafisha wahalifu halisi. Lengo ni kuendeleza ukandamizaji wa sauti huru na kuhalalisha utawala wa mabavu unaotekelezwa na serikali isiyo na ridhaa ya wananchi.
Kwa msingi huo, Chadema inasisitiza kwamba; iundwe Tume Huru ya Kimataifa, yenye uwezo, weledi, mamlaka na uaminifu wa kuchunguza kwa uhuru na umakini mauaji, makosa dhidi ya binadamu na ukiukwaji mkubwa wa haki za msingi za raia uliofanywa chini ya utawala wa Samia Suluhu Hassan. Serikali inapaswa kuruhusu uchunguzi huo usimamiewe na Tume Huru ya Kimataifa ambayo itafanya kazi bila uoga, vitisho wala kuingiliwa.
Tunatoa wito kwa taasisi za kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa na Baraza lake la Usalama (UNSC), Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Mauaji ya Halaiki, Makosa Dhidi ya Binadamu na Makosa ya Kivita (ICC), kamisheni za haki za binadamu za kikanda na kimataifa, mataifa rafiki na wadau wote wa demokrasia kuchukua hatua za haraka kuishinikiza Serikali ya Samia na CCM kuruhusu uchunguzi huru wa kimataifa.
Ujumbe wetu uko wazi na thabiti:
• Hakuna amani bila haki.
• Hakuna uhalali bila ridhaa ya wananchi.
• Mtuhumiwa hawezi kuwa mwamuzi wa uhalifu alioufanya.
Chadema itaendelea kusimama imara na wananchi wa Tanzania hadi haki itendeke na wahalifu dhidi ya ubinadamu wawajibishwe kama inavyostahili. Tunawaomba waTanzania na jumuiya yote ya kimataifa kutuunga mkono katika msimamo wetu huu.
Imetolewa leo Jumatano, tarehe 19 Novemba, 2025 na;
JOHN HECHE
Makamu Mwenyekiti Bara