Heche: Ongezeko la bei ya mafuta na miamala inatokana na wabunge wa serikali

Huko ni kulidhalilisha Bunge la JMT,nadhani ungetumia maneno ya staha ujumbe wako ungefika pia.Mh. Rais aliwahi kusema tuwakosoe kwa heshima na siyo kuwatukana.
Usitetee ujinga, wewe na wabunge wako hao kafie nao huko
mbele
 
Hakuna mtu aliyetamani kujenga mabarabara, madarasa na hizo huduma za afya kama magufuli lakini mbona hakuleta haya mauzauza ya tozo? Hawa hizi hela kuna sehemu wanazipeleka na sio huko wanapojaribu kutuaminisha na ndio maana wanatumia nguvu kubwa sana kueneza hizo propaganda zao kuhusu haya makato.
 
"Wabunge waliochaguliwa na wananchi hawawezi kukaa kwenye bunge linalowaongezea wananachi gharama kila siku. Wabunge wa wananchi siku zote wanajitahidi kuibana serikali ipunguze gharama za maisha kwa wananchi. Ongezeko la bei ya mafuta na miamala inatokana na wabunge wa serikali.

Unamtumia mama yako pesa kijijini wanakata tozo, mama ambae hana kazi anakwenda kutoa pesa ili anunue sababu nae wanamkata tozo.

Hili ndio bunge ambalo zaidi ya nusu ya wabunge wake hawakuchaguliwa na wananchi, bunge linalopunguza bei ya bia na kuongeza bei ya mafuta." - Mh John Heche
Hao ni watu wanaokusanyika na kugawana kodi zetu kwa manufaa ya matumbo yao na familia zao kln sio kulisaidia taifa
 
Back
Top Bottom