Hili suala linakiathiri kuliko unavyofikiria. CDM ilipaswa kulizima mapema ili kuzuia CCM kulitumia kisiasa. Na tayari wanalitumia kupakazia chama kizima wakati nyie mnajifanya hamuoni.
Hamna mvutano maana kila mtu anajua Team Lissu ilishinda uchaguzi. Hao unaowaita Team Mbowe hawana mamlaka yeyote ndani ya Chadema. Ni wajibu wa Team Lissu kuwaonyesha kuwa pamoja na wao kushinda uchaguzi, wale walioshindwa bado wana nafasi na heshima katika chama. Kuwananga ni siasa mbovu.
Tangu lini kuwa Team Mbowe imekuwa dhambi? Mlitaka wote wawe Team Lissu? Kama kigezo cha kumuamini mtu ni kumkubali Lissu basi tatizo ni kubwa. Wanaokiharibu chama chenu sio CCM bali ni wale wanaotaka kutumia nafasi zao au ukaribu wao na viongozi kulipa visasi. Sagrida sio mnafik. Anachotaka ni heshima wanayostahili kama viongozi. Aidha, anakataa kubagaza mchango mkubwa wa Mbowe kwa chama chake. Kufanya hivyo sio kukataa kuutambua uongozi wa sasa.
Kama mna imani hiyo hapatakuwa na kuponya vidonda. Hivi unadhani Mbowe angetaka kuendelea kama Mwenyekiti angeshindwa? Amesaidia kufanikisha uchaguzi uliokuwa huru na haki na amempisha Mwenyekiti mpya aongoze chama. Tofauti na unavyosema, ni Team Lissu ndio inaelekea haikutegemea kushinda maana wanajua ni vigumu wa viongozi wa vyama vya siasa nyumbani kukubali kushindwa. Walijua Mbowe atatumia hata mbinu chafu kubaki madarakani. Alipoendesha uchaguzi ambao kila mtu ameusifia na kukubali kushindwa iliwastua. Kinachosikitisha ni kuwa badala ya kuhakikisha chama kinabakia kimoja, baadhi yao wanaendekeza siasa za visasi na kuchafuana.
Approach ya Mbowe na Lissu ni tofauti. Hata hivyo hamna kampeni ya chama ambayo Mbowe hakujihusisha kikamilifu.
Sio dhambi kujitayarisha kugombea ili kama uongozi ukibadili mawazo au mabadiliko ya maana yakifanyika wawe katika nafasi nzuri ya kushinda nafasi za kutosha. Ni kuwaonea kuwashutumu kuwa watakuwa tayari kutumika ili mradi tu wapate ushindi. Mtazamo huo ndio unaharibia chama chenu. CCM haishindwi kuweka mtu ambae hata sio mwanachama wa CDM kugombea. Aidha, wanaweza kuhakikisha wagombea kutoka vyama vingine vitakavyoshiriki kwenye uchaguzi vinashinda. Kama ilivyofanywa kwa Chaumma. Vyama kama CUF, NCCR Mageuzi hata ACT-WAZALENDO havitajivunga nafasi hiyo ikitokea.
Amandla...