ChekoFagia
Senior Member
- Sep 20, 2025
- 115
- 339
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche ameitaka serikali kuchukua hatua za haraka ili kuepusha nchi kuingia kwenye matatizo makubwa yanayoweza kuathiri amani na usalama wa wananchi.
Heche alisema kuwa hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya waliouwa watu na wale waliyoagiza kupigwa risasi, huku akisisitiza pia kuondolewa kwa kesi za kisiasa zinazochochea migogoro.
“Hakuna taifa la nje limechochea, nyie ndio mmechochea hayo,” alisema Heche, akisisitiza kuwa hatua hizo ni muhimu kuhakikisha haki inatendeka na wananchi wanakuwa salama.
Aidha, Heche aliongeza kuwa serikali inapaswa kuhakikisha kesi za kisiasa ziondolewe haraka na wahusika wa ukiukaji wa sheria wachukuliwe hatua bila kuchelewesha, ili kudumisha amani na utulivu wa nchi.