PreGE2025 Heche apeleka 'No reforms No election' Chato asisitiza uhitaji tume huru ya uchaguzi

PreGE2025 Heche apeleka 'No reforms No election' Chato asisitiza uhitaji tume huru ya uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), John Heche amefika Wilaya ya Chato, nyumbani kwa Rais wa Awamu ya Tano hayati John Magufuli, kupeleka kampeni ya chama hicho ya No reforms, No election.

Heche anayeongoza timu ya chama hicho katika ziara ya Kanda ya Victoria, ameingia Chato leo Mei 10, 2025 na kuhutubia mkutano wa kwanza katika Kijiji cha Muganza.

Katika mkutano huo amewataka wakazi wa eneo hilo na Watanzania wote kuunga mkono kampeni ya kudai mabadiliko ya sheria na mfumo wa uchaguzi unaorejesha mamlaka kwa umma.

Amesema mapambano ya Chadema ya kudai mabadiliko yanalenga kujenga Taifa ambalo mamlaka yote ya nchi yako mikononi mwa wananchi na viongozi wawajibike kwa umma, tofauti na sasa ambapo alidai viongozi wanafanya watakalo bila hofu.

"Hapa Muganza mna Ziwa Victoria lakini hamnufaiki ipasavyo kutokana na kukosekana kwa sera na mipango ya kuwainua wananchi kiuchumi, wananchi tuungeni mkono kudai mabadiliko tubadilishe mfumo huu," amesema Heche.

Akifafanua, kiongozi huyo amesema sheria na mfumo uliopo hauweki sawa uwanja wa ushindani kisiasa, kwa sababu mchakato wote wa uchaguzi unasimamiwa na kuendeshwa na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

"Mfano hai ni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ambayo miongoni mwa wajumbe watano, mmoja si tu kada wa CCM, bali pia alikuwa kiongozi wa juu wa chama hicho," amesema Heche.
Amesema Chadema inachopigania ni haki na usawa kwa wagombea na vyama vyote vya siasa.
 
Back
Top Bottom