Heche apangua Hoja zote za mwandishi wa StarTV

Mhe. John Heche Yuko live StarTV. Huyu jamaa ni Jembe na ni kichwa.
Amepangua hoja zote kuhusiana na tuhuma dhidi ya CHADEMA kuhusu Mwenyekiti Mbowe na kufukuzwa kwa Wabunge waliokaidi agizo la chama kujitenga Bungeni.

Saafi sana Mhe. Heche.
Hii nayo ni thread sio?
 
Odemba aweke Full Interview kwenye Youtube Channel hii ya Leo wamemkatisha katisha sana kwahiyo hajatolea maelezo ya kina ila ni kweli kapangua maswali yote ya Odemba.

Nimeitafuta sana hiyo Interview kwene StarTV -Y.Tube Channel hawajai- upload....!! Nachelea hawataiweka maana kina Mr. Slowslow wa CCM wakiiona wanaweza pata wazimu!
 
Sina uhakika unachoamini ni nini ila maandiko yako yanathibitisha kwamba "hujui kama hujui". Kwa mfano, Heche wenu anadai pesa zinazojenga " vitu" ni za walipa kodi, hivyo CCM haipaswi kujivuna. Je, huoni kuwa Serikali ya CCM ina viongozi waadilifu wanaosimamia matumizi mazuri ya fedha ya walipa kodi tofauti na viongozi wenzake CHADEMA?

Hiyo ndiyo tofauti kubwa kati ya CCM na CHADEMA yenye viongozi vuvuzela ambao kwa gharama yoyote wako tayari kumtetea Mbowe hata kama atawaamuru kulamba miguu yao. Viongozi wanaojitambua, wanahama. Kama hawa wabunge.

Ulitaka kuja vizuri mjadala wako lakini umeharibu kwa kutoa huo mfano eti wa " viongozi wanaojitambua!"
Inaelekea sio mfuatiliaji mzuri wa matukio ya kisiasa ya nchini mwako hivyo no rahisi kuchotwa na propaganda zozote. Chunguza mambo kabla hujayafanya agenda yako. Hizo taka usirudie kufanya mifano yako zinakuchafulia points katika hoja zako
 
Nimeitafuta sana hiyo Interview kwene StarTV -Y.Tube Channel hawajai- upload....!! Nachelea hawataiweka maana kina Mr. Slowslow wa CCM wakiiona wanaweza pata wazimu!

Acha tu StarTV inabidi waendane na Tech ya Sasa , VIindi vingi vikisharushwa vinawekwa Youtube sasa sijui wao wanakwama wapi.
 
Mhe.Heche ni moja ya vijana ambao ni hazina kwa chama lkn na kwa nchi pia...mbeleni anaweza kuja kuwa Mwenyekiti wa chadema Taifa..kifupi anafaa
 
Ulitaka kuja vizuri mjadala wako lakini umeharibu kwa kutoa huo mfano eti wa " viongozi wanaojitambua!"
Inaelekea sio mfuatiliaji mzuri wa matukio ya kisiasa ya nchini mwako hivyo no rahisi kuchotwa na propaganda zozote. Chunguza mambo kabla hujayafanya agenda yako. Hizo taka usirudie kufanya mifano yako zinakuchafulia points katika hoja zako

Katika haya yafuatayo, toa maoni yako kwa dhati:
1) Sifa za kiongozi bora wa kisiasa.
2) Maana ya "utashi wa kisiasa"

Baada ya hapo nitarudi kujibu hoja yako, nanukuu: usirudie kufanya mifano yako zinakuchafulia points katika hoja zako
 
Amedhirisha madai kuwa viongozi wa CHADEMA hawathamini na kuheshimu Jatiba yao, sembuse ya JMT. Amethibitisha pia kuwa mamuzi ya CHADEMA ni ya Mbowe, hivyo tyhuma dhidi yake zina ukweli.

Sentensi moja tu inathibitisha hoja yangu pale alipokiri kuwa moja ya msingi wa Demokrasia ni kukubali maamuzi ya wengi (collective respinsibility). Ati ni kwa sababu hiyo hao Wabunge wamefukuzwa kwa kukiuka maamuzi ya wengi.

Vitendo vya kususia Bunge, kwa nyakati mbalimbali, ikiwa ni moja ya kufunga midomo huku wakisusia kikao cha bunge, kwa hoja yake ya "collective respobsibility" walipaswa na wao kufukuzwa bungeni moja kwa moja.
Kwa kawaida hasa wale walienda shule isipokuwa na jibu sahihi la swala unaacha kujibu kuliko kupoteza muda wa wasahishaji na wino wa maswali unayoyajua sawa sawa.
Kiongozi ni hayo tu kwa leo
 
Mr Heche! watanzania tukubali huyu ni hazina ya Taifa. kwa hoja, maono na kujiamin katika anachoamin. nasikitika kuona hatunaye ccm akashirikiana na rais!
 
Amedhirisha madai kuwa viongozi wa CHADEMA hawathamini na kuheshimu Jatiba yao, sembuse ya JMT. Amethibitisha pia kuwa mamuzi ya CHADEMA ni ya Mbowe, hivyo tyhuma dhidi yake zina ukweli.

Sentensi moja tu inathibitisha hoja yangu pale alipokiri kuwa moja ya msingi wa Demokrasia ni kukubali maamuzi ya wengi (collective respinsibility). Ati ni kwa sababu hiyo hao Wabunge wamefukuzwa kwa kukiuka maamuzi ya wengi.

Vitendo vya kususia Bunge, kwa nyakati mbalimbali, ikiwa ni moja ya kufunga midomo huku wakisusia kikao cha bunge, kwa hoja yake ya "collective respobsibility" walipaswa na wao kufukuzwa bungeni moja kwa moja.
Tatizo uamua kuchagua upande mkuu ndo maana key point hujazikamata vizuri
 
Mhe. John Heche Yuko live StarTV. Huyu jamaa ni Jembe na ni kichwa.
Amepangua hoja zote kuhusiana na tuhuma dhidi ya CHADEMA kuhusu Mwenyekiti Mbowe na kufukuzwa kwa Wabunge waliokaidi agizo la chama kujitenga Bungeni.

Saafi sana Mhe. Heche.
Hajapangua amejibu
 
Back
Top Bottom