Heche anadai Wabunge walilipwa Tsh milioni 272 za pensheni

Kwenye ukweli tuseme ukweli bora Mbowe kuliko mtu mwenye emotions za hovyo kama Heche asiye na staha, asiyefanya uchaguzi kabla ya kutamka, mtu mwenye jazba.

Heche hajui kiinua mgongo kinatoka na ukubwa wa mshahara, niliambiwa Heche ni msomi wa chuo kwa nini anashindwa kuelewa ishu ndogo kama hii.

Wabunge kote duniani hupewa pesa yao ya pensheni wakimaliza kipindi chao cha uongozi vilevile marais kwa nini Heche anashindwa kuelewa ishu ndogo kama hii analinganisha kazi ya miaka 30-40 kwa mishahara kiduchu na yale mamilioni ya kibunge.

USSR
View attachment 2514985
Hujaeleweka..!

Hoja ni ipi in contrast na ya John Heche?

Hoja kuu ya John Heche ni kikotoo cha mafao ya wastaafu cha 33.3% wa nchi hii wengi wao wakiwa ni walimu, manesi, madaktari, mapolisi, wanajeshi nk kwamba hakiwatendei haki kulinganisha na kada ya wanasiasa kama Rais, VP, PM, mawaziri, wabunge, RCs, DCs, wakuu wa taasisi za umma nk..

Katika kulitolea ufafanuzi ili watu waelewe, akasema, inakuwaje mfanyakazi kama mwalimu au daktari au nesi, au polisi mwenye mshahara wa TZS 1,000,000 aliyelitumikia Taifa hili kwa miaka 25 au 30 mwisho wa siku aje aambulie mafao ya mkupuo ya TZS (labda) 45,000,000 huku mtu kama mbunge Kwa miaka mitano tu ya kuwa mbunge analipwa mafao ya TZS 270,000,000???

Usawa uko wapi ktk mazingira haya?

Kumbuka hawahawa wabunge wanaochukua mafao makubwa namna ndiyo wanaokaa chini kutunga na kupitisha sheria za wao kujipendelea kiasi hiki na wakati huohuo wakipitisha sheria za kukandamiza kundi kubwa la watumishi ambao kiukweli si sawa kabisa na wao..!!

Hapa ndipo ilipo hoja ya John Heche. Amekengeuka wapi na wewe hoja yako ni nini kupingana naye??
 
272M na mtu yuko bungeni kwa zaidi ya vipindi 5 (mkuchika) na wenzie alafu umwambie nji hii kuna watu mlo mmoja ni shida atakuelewa??
 
Heche leo kaongeza kufika 2025 Kuna uwezekano wakalipana zaidi ya 400M.

Tupo hapa, kaz inaendelea😄
 
Back
Top Bottom