Heche amtaka Raisi kupeleka mabadiliko ya Katiba bungeni kuruhusu marais Mkapa,Kikwete wachunguzwe

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Mbunge wa Jimbo Tarime Vijijini kupitia Chadema John Heche amtaka Raisi John Pombe Magufuli kupeleka mabadiliko ya Katiba bungeni ili kuruhusu maraisi Benjamini Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete wachunguzwe kuhusiana na mikataba ya madini .
Mbunge huyo amesema wananchi hawataruhusu ndege kutua North Mara kuchukua madini kwa sababu kampuni hiyo imebainika kuiibia nchi.
Mbunge huyo amesema atawahamasisha wananchi kuvamia mgodi wa North Mara baada ya ripoti kuonyesha unaiibia nchi.
tmp_23769-IMG_20170613_111141-1834689759.jpg
 
CCM ya Mkapa na Kikwete iseme wazi kwa nini iliacha kuisimamia serikali na kuacha wizi huu uliolipotezea taifa Trilioni karibu 180?kwa ni waliacha kuisimamia serikali kama alivyowahi himiza Katibu mkuu Kinana?.
 
Mbunge wa Jimbo Tarime kupitia Chadema John Heche amtaka Raisi John Pombe Magufuli kupeleka mabadiliko ya Katiba bungeni ili kuruhusu maraisi Benjamini Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete wachunguzwe kuhusiana na mikataba ya madini .
Pia mbunge huyo amesema wananchi hawataruhusu ndege kutua North Mara kuchukua madini kwa sababu kampuni hiyo imebainika kuiibia nchi.
View attachment 523194

bunge wa Tarime Vijijini, John Heche amesema atawahamasisha wananchi kuvamia mgodi wa North Mara baada ya ripoti kuonyesha unaiibia nchi. Mwananchi Newspapers (@MwananchiNews) | Twitter
 
Apo sasa ndio tutapata moyo na imani kwamba Rasi naye ana damu na anafanya haya kwa kuwahurumia watanzania maskini. Wachunguzwe tu maana sasa hatuna namna.
 
Mh.W
Mbunge wa Jimbo Tarime kupitia Chadema John Heche amtaka Raisi John Pombe Magufuli kupeleka mabadiliko ya Katiba bungeni ili kuruhusu maraisi Benjamini Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete wachunguzwe kuhusiana na mikataba ya madini .
View attachment 523194

Mh.Heche ulichosema ni hakika kikifanyika "Vita hii ya Uchumi" itafanikiwa. Kwani, nionavyo mimi wale wote waliotajwa kwenye ripoti ya 2 ya Kamati ya Rais juu ya makanikia hawatahojiwa kivile kama bado Sheria ya Kinga kwa marais itaendelea kuwepo au kutorekebishwa. Mathalan, chini ya sheria hii nd na waheshimiwa waliotajwa watakapohojiwa wakawa na neno moja tu, "Niliagizwa na rais." Je! Hapo kutakuwa na haja ya kuendelea kuchunguza? Utaendelea kuchunguza ili iweje?

Miye naona, Mh.rais Magufuli aiondoe nchi kwenye mikatasba yote ya kimataifa ya uwekezaji kwenye madini, gesi na mafuta kisha aifute mikataba yote ya uchimbaji madini, mafuta na gesi. Halafu, ile sheria ya madini na uwekezaji ya 1997, 1998 na zote zilifuata zifutwe tutunge sheria nyingine kabisa, au tuondoe vipengele vya kinyonyaji kwenye sheria zilizopo.

Vinginevyo, Mh.Rais kama hawezi kufanya hivyo anyamaze kimyaaaaaa!
 
  • Thanks
Reactions: bht
Haha hapo patamu,, vile vile suala la uwajibikaji kwa viongozi.. Ifike wakati tuwe na adhabu kama China,, Enough is Enough,, sisi wanyonge tumeonewa vya kutosha wakati kuna watanzania wenzetu wanaishi kama hawatakufa.. Umoja wetu ndio nguvu yetu.. Vijana ni nguvu ya Taifa katika kulijenga, kulilinda na kuliendeleza.. Tumuunge mkono Raisi wetu kwa ajili ya maslahi ya watanzania wote..
 
Kama ni hivo na wafuatao wawe kwenye list...Lowasa na sumaye maana hao ndo walikua mawazir wakuu enzi hizo
 
Msingi wa mwanzo baada ya Uhuru ndo chimbuko la haya. Haki tena haukuwa mzuri.!
 
Mbona Msimamo wa Rais Uko wazi kuwa hapangiwi?

Heche ni nani? Kwanini hajaanza Kumshauri Mbowe juu ya Kuschia ngazi uwenyekiti wa kudumu wa CHADEMA?

Upumbavu wenu wa kuleta ushabiki wa kiccm kwenye hoja zenye maslahi mapana kwa taifa letu ndiyo umetuletea hasara kwenye nchi hii. Wakati wapinzani wanapinga kupitishwa sheria ya madini kwa hati ya dharula mliwatukana sana na kuwazomea.Sheria mlizopitisha kwa mbwembwe na kuwazodoa wapinzani ndiyo hizi zimeleta mikataba inayotutafuna, na kwa akili hizo hizo za kushikiwa nawe uanaponda hoja ya Heche. Kweli aliyewaroga CCM ameshakufa.
 
Back
Top Bottom