Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Akisisitiza kuwa hakuna kutetereka wala kuogopa, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema John Heche akiambatana na Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika, ameeleza kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Tundu Lissu, amefurahia sana wingi wa wananchi waliojitokeza leo Mei 19, 2025 kusikiliza shauri la Lissu lililotajwa kwenye Mahakama ya Kisutu Dar Es salaam.
Heche katika maelezo yake, amehimiza pia wanachama wa Chama hicho kujitokeza kwa wingi Juni 02, 2025 kwenye Mahakama ya Kisutu, kwenye muendelezo wa usikilizwaji wa shauri la Lissu.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Heche pia amebainisha kuwa Wiki hii wataketi kama Kamati kuu na baada ya hapo watendelea na ziara za No Reforms, No election, akibainisha kuwa bado msimamo wa chama hicho ni kwamba hawakatai uchaguzi bali watashiriki uchaguzi pale tu ambapo yatafanyika mabadiliko ya sheria na mifumo ya uchaguzi, itakayoweka mizania sawa kwa vyama vya siasa n wanasiasa wanaoshiriki chaguzi.
Wakati akimaliza kuzungumza, wanachama na wananchi waliokuwa wakimsikiliza kando ya kuandamana naye wakilisindikiza gari lake, wamechanga fedha kadhaa kama sehemu ya utamaduni wao wa siku za karibuni kupitia kampeni ya Tone tone.