Heche ahoji Chongolo kudai Katiba Mpya si hitaji la Wananchi bali Wanasiasa

Paf

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,703
3,304
Akihojiwa na mwandishi wa Dar mpya katika mjadala uliomhusisha Sosop na Heche juu ya kauli ya katibu mkuu CCM kuhusu hitaji la KATIBA MPYA kwamba.

1. Wanaodai Katiba mpya ni wanasiasa wanaotaka madaraka na sio wananchi.

Heche; Amemuuliza Chongolo ni muimbaji wa kwaya?au alitoa kauli hiyo kama mwanasiasa.Nani yupo madarakani kisiasa.

2. Wanaodai Tume huru haiwapelekei wananchi Ugali.

Heche; Wananchi ndiyo wanapeleka Ugali kwa CCM kupitia Tume ya uchaguzi iliyoteuliwa na katiba mbovu,hivyo Chongolo anawapumbaza wananchi.

3. Mliwahi waona wananchi wakionyesha mabango ya kudai Katiba kama sio wanasiasa?

Heche; Wananchi walishatoa maoni yao kupitia Tume ya Warioba ambayo iligharimu pesa nyingi na sheria ilipitishwa na Bunge kwa niaba ya wananchi.
 
Naungana naye katibu mkuu kwa hili hitaji la katiba na tume huru sio la wananchi Ni la wanasiasa

Sababu wanayodai sio hitaji la majority ni la wao kupata katiba ya kuwapa vyeo tu serikali ya umoja sijui wa kitaifa na chaguzi sababu wao wagombea !!!

Hoja za wananchi ziko wazi mfano wa being za miamala zilivyopanda itikio la wananchi limekuwa juu

Wanahitaji ajira na maendeleo nk

Katiba mpya si kitu kwao ni kiti kwa viongozi tu .Mkulima kijijini hata haelewi Katiba mpya ndio dudu gani au takataka gani.Ni hotaji la wanasiasa Tena viongozi wa vyama
 
Kwani wanasiasa hao wanaotaka katiba mpya si wananchi? Au mwananchi mpaka awe mwanaccm tu? By the way Kama wananchi hawataki katiba mpya nyie mlijuaje hawataki?

Na Kama wanasiasa tu wanaotaka katiba mpya si muwache watasutwa na wananchi? La mwisho malengo ya chama siasa kwa mujibu wa katiba ni kushika Dora( madaraka) .

So porojo kuwa Wana uchu wa madaraka, Ni kwa mujibu wa katiba na Sheria. Kwani nyielitaka wawe na uchu na Nini?
 
Naungana naye katibu mkuu kwa hili hitaji la katiba na tume huru sio la wananchi Ni la wanasiasa

Sababu wanayodai sio hitaji la majority ni la wao kupata katiba ya kuwapa vyeo tu serikali ya umoja sijui wa kitaifa na chaguzi sababu wao wagombea...
Ile rasimu ya Warioba ilikua ni kwa kuiweka maktaba?
 
Ile rasimu ya Warioba ilikua ni kwa kuiweka maktaba?
Wafadhili ndio walitaka .Ikawekwa kabatini si unaona wananchi walibaki kimya tu miaka yote pamoja na kulibwaga Hilo li draft li rasimu kabatini
 
Wafadhili ndio walitaka .Ikawekwa kabatini si unaona wananchi walibaki kimya tu miaka yote pamoja na kulibwaga Hilo li draft li rasimu kabatini
Kwahiyo yale maoni ya wananchi yalikusanywa ili kuwafurahisha wafadhili?
 
Chongolo hana hoja, kwani wanasiasa siyo wananchi?

Mbona CCM mwaka 2015 kwenye ilani yao walitaka katiba mpya, ina maana waliacha kuwa wananchi kwa wao kutaka katiba mpya?
 
Chongolo eti wananchi hawataki katiba mpya waliotoa maoni kwenye tume ya Warioba walikuwa tembo ?
 
Naungana naye katibu mkuu kwa hili hitaji la katiba na tume huru sio la wananchi Ni la wanasiasa

Sababu wanayodai sio hitaji la majority ni la wao kupata katiba ya kuwapa vyeo tu serikali ya umoja sijui wa kitaifa na chaguzi sababu wao wagombea...
Wafuasi wa watawala akili mmezikalia.

Wanasiasa ni nani kama si wananchi ?!

Chama kikongwe kama Ccm kukwepa katiba mpya iliyo fair kwa kila mtu. Hata kama ni wachache ni zaidi ya uwendawazimu

Odhis *
 
Back
Top Bottom