Hebu Ipe Akili Yako Uhuru wa Kufikiri !

Hebu Ipe Akili Yako Uhuru wa Kufikiri !

Judgement

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2011
Posts
10,326
Reaction score
4,789
Huko kale tuliamini matambiko!
Then tukapata dini tukawa Waislamu & Wakristo .

Tulikua na chama kimoja tu, cha siasa!
Then tukapata multparty.

Elimu ya msingi tulikomea darasa la 4 !
Then tukapata darasa la 7.

Michezo tulianza na FAT !
Then tukapata TFF. Aidha
Tulianza na National Stadium (Old usio na sifa za kimataifa)
Then tukapata new National Stadium (ukubalikao kimataifa)

Mawasiliano tulianza na POSTA & SIMU ==> TCCL!
Then tukapata VODA , AIRTEL, TIGO , ZANTEL .

Habari tulikua na Radio 1 tu , RTD TV hatukua nayo kabisa!
Magazeti yalikua mawili UHURU & MZALENDO!
Then tukapata Radio kibao, na Magazeti lukuki.

Burudani tulikua na video za mikanda!
Then DVD, VCD.
Aidha tukatoka kwenye mafaili tukaja kwenye COMPUTER , INTERNET !

Tulikua na Telegram Money Oder!
Tukaja kwenye M'PESA , ATM.

Tumebakiza kitu kimoja tu!
Nini hicho?

CHAMA.
Chama gani?

C . C . M !
Hiki kinasubiri nini?

Wakati
CHADEMA
Hii hapa? TAFAKARI !
Ipe Akili yako Uhuru Wa Kufikiri!
 
Lilianza agano la kale likaja agano jipya wakasema lile la kale ni kuukuu lakini limeshindikana kutupwa kwa kuwa hekima yote ya maneno ya Mungu yapo kulee kwenye agano la kale. ccm ni agano la kale copy chama
 
Last edited by a moderator:
Lilianza agano la kale likaja agano jipya wakasema lile la kale ni kuukuu lakini limeshindikana kutupwa kwa kuwa hekima yote ya maneno ya Mungu yapo kulee kwenye agano la kale. ccm ni agano la kale copy chama

Uko tayari kubadilika Mamndenyi? Tuipeleke sisieka walipo nduguze KANU na UNIP.
 
Last edited by a moderator:
Hapana mie ni wa ccm tu,
soma madhumuni ya chama chetu
then uweke ya chama chenu ili tukompee;
MADHUMUNI
Malengo na Madhumuni ya CCM yatakuwa yafuatayo:-
1) Kushinda katika Uchaguzi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa Tanzania Bara na Zanzibar ili kuunda na kushika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande mmoja na Zanzibar kwa upande wa pili.

2) Kulinda na kudumisha Uhuru wa Nchi yetu na raia wake.

3) Kuhimiza ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea kwa mujibu wa Azimio la Arusha.

4) Kusimamia utekelezaji wa Siasa ya CCM pamoja na kuendeleza fikra za viongozi waasisi wa vyama vya TANU na ASP, kama zilivyofafanuliwa katika maandiko mbali mbali ya Vyama hivyo

5) Kuona kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika Jamii hifadhi ya maisha yake na mali yake kwa mujibu wa sheria.

6) Kuona kwamba katika Nchi yetu kila mtu aliye na uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi; na kazi maana yake ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu riziki yake.

7) Kusimamia haki na maendeleo ya Wakulima, Wafanyakazi na wananchi wengine wenye shughuli halali za kujitegemea; na hasa kuona kwamba kila mtu ana haki ya kupata malipo yanayostahili kutokana na kazi yake.

8) Kuona kwamba kwa kutumia Vikao vilivyowekwa, raia anayo haki ya kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi wa mambo ya Taifa na yanayomhusu, na kwamba anao uhuru wa kutoa mawazo yake, wa kwenda anakotaka, wa kuamini Dini anayotaka na kukutana na watu wengine,maadamu havunji Sheria au Taratibu zilizowekwa.

9) Kuona kwamba Nchi yetu inatawaliwa kwa misingi ya kidemokrasia na ya kijamaa.

10) Kuhifadhi, kukuza na kudumisha imani na moyo wa kimapinduzi miongoni mwa Watanzania pamoja na ushirikiano na wanamapinduzi wenzetu kokote waliko.

11) Kuweka na kudumisha heshima ya binadamu kwa kufuata barabara Kanuni za Tangazo la Dunia la Haki za Binadamu.

12) Kuona kwamba Dola inakuwa Mhimili wa Uchumi wa Taifa.

13) Kuona kwamba Serikali na Vyombo vyote vya Umma vinasaidia kwa vitendo kuanzishwa na kuendeleza shughuli za Ushirika na za ujamaa, na shughuli nyinginezo halali za wananchi za kujitegemea.

14) Kuona kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya Wananchi na hasa jitihada za kuondosha umasikini, Ujinga na Maradhi.

15) Kuona kwamba Serikali na vyombo vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wanawake na wanaume bila kujali rangi, kabila, Dini, au hali ya mtu.

16) Kuona kwamba katika nchi yetu hakuna aina yoyote ya dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu na/au upendeleo.

17) Kuendelea kupiga vita Ukoloni Mamboleo, Ubeberu na Ubaguzi wa aina yoyote.

18) Kuimarisha uhusiano mwema na Vyama vyote vya Siasa vya Nchi nyingine vyenye itikadi kama ya CCM ambavyo kweli vinapinga Ukoloni, Ukoloni Mamboleo, Ubeberu na Ubaguzi wa aina yoyote.

19) Kushirikiana na Vyama vingine katika Afrika, kwa madhumuni ya kuleta Umoja wa Afrika, na kuona kwamba Serikali inaendeleza na uimarisha ujirani mwema.
copy: chama





Uko tayari kubadilika Mamndenyi? Tuipeleke sisieka walipo nduguze KANU na UNIP.
 
Last edited by a moderator:
Lilianza agano la kale likaja agano jipya wakasema lile la kale ni kuukuu lakini limeshindikana kutupwa kwa kuwa hekima yote ya maneno ya Mungu yapo kulee kwenye agano la kale. ccm ni agano la kale copy chama
Mamndenyi
Maneno yamejaa hekima nyingi asiyetaka kuelewa mwache na ujuha wake!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom