Bob Lee Swagger
JF-Expert Member
- Oct 21, 2011
- 1,362
- 519
Bujibuji nashukuru sana kwa bandiko zuri ila mimi naomba nionezee kidgo sana jambo hapa.
jamani najua kabisa sio mara zote ama wanaume wote wata kaa na kudumu na wake zao, la hasha, najua kwamba kuna kutoka nje ama kuna kucheat. Lakini sasa inapotokea basi wewe mwanamke ukawa unatoka na mume wa mtu basi jiheshimu. Heshimu nafasi uliyopewa wala usimdharau anayemmiliki. usilete jeuri na kuona kwamba wewe u babu kubwa zaid kuiko mke wake nyumban.
huwa nawashangaa sana wanawake wa aina hii manake laiti wanagalijua kwamba ukiwa unatoka na mume wa mtu, kisha ukamheshimu na kuiheshimu familia yake, mara nyingine ukamsaidia hata kumfanya aipende familia yake ni kwamba utakuwa na chance kubwa sana ya kufaidi penzi la huyo mtu bila ugomvi.
wanaume wana siri moja wanapenda sana kujaliwa, na kuheshimiwa hisia zao sasa ukimjali na kuheshimu hizia zake kwa familia yake ni kwamba unamfanya awe mtu wa kukupenda sana wewe kuliko kitu chochote. wewe ni hawara siku moja moja mwambie huyo bwana hebu leo twende shopping ama nipe hela nikanunue nguo basi akikupa unanunua moja yako na nyingine ya bi mkubwa akija unampa unamwambia kabisaa sio kila siku navaa mm na mwenzangu pia. ukweli huyu mwanaume atakuwa na heshima sana kwako.
pia muda mwingine anakuja kwako kagombana na mkewe basi wewe usianze uonyesha kwamba mkewe ni mkosa ila mwonyeshe jinsi ambavuo katika lile kosa hakuitumia vyema nafasi yake ya ubaba uone tena ujitahd kuhakikisha kwamba hata home anatengeneza amani irudi na mkewe. mtingishie kiberiti kwamba kama huna amani kwako basi kwangu usije manake nataka uje ukiwa na raha tufurahie maisha. huyu mwanaume lazima atadumu na wewe hawara milele.
NB naomba ieleweke kwamba siufagilii umalaya ila hapa najaribu kuonyesha uhalisia kabisa ambao unatakiwa kuwepo wakati ambapo hii dhahama imesha ingia. kwa vyvyote vile ndoa na iheshimiwe na watu wote.
Dada gfsonwin, naona sasa umeanza kumfunda Da Sophy ili adumu daima!
Binafsi naona hii comment yako inatakiwa kuanzishiwa thread yake yenyewe kabisa...!! :yo:
Title iwe "Mwanamke, fanya haya ili kuwa hawara atakayedumu milele" itafaa nadhani, hahahah hahahah
Last edited by a moderator: