Hear out my story/ sikia historia yangu

Hear out my story/ sikia historia yangu

Joined
Oct 24, 2014
Posts
7
Reaction score
1
Katika maisha kuna vitu tunavipitia ambavyo wakati mwingine huvunja moyo na kukatisha tamaa. Naomba uandike wakati mgumu unao pitia/uliowahi kupitia ili tutiane moyo na kushauriana. Pia story yaweza kumsaidia mwingine anepita ktk wakati kama huo. In the world we are living there are some ppo whom their live are misserable just becoz they lack someone to talk to, and some one who can give them HOPE...LETS SHARE OUR LIFE EXPERINCE
 
hiyo stori yako mbona hukuiandika??? umeandika.heading sikia stori yangu iko wapi
 
Samahanini wana jamvi nilibanwa kidogo na majukumu nikashindwa kumalizia lakini simulizi ninayoenda kutoa si yangu bali ni ya rafiki yangu kwani imenigusa sana na nikatamani kushiriki nanyi.
Ni msichana wa miaka 24 aliyemaliza masomo yake ya shahada ya sheria mwaka huu, japo katika changamoto nyingi.
Kila kitu kilianza alipokua mwaka wa kwanza ambapo baba yake mzazi ambae alikua ndio tegemeo kubwa la familia mwili wake ulipooza (alipata strock) ambayo ilimpelekea asiweze kuendelea na kazi. Kutokana na hilo hakuweza kuendelea kumlipia binti huyu ada ya shule na ndugu zake wakashinikiza aache masomo hadi hali iatakapo kua nzuri. Lakini binti huyu alimuamini Mungu kuwa hata kama familia imeshindwa kumsomesha Mungu atainua watu watakao jitolea kumsaidia kulipa ada.
Maisha yalianza kuwa magumu japo aliendelea kujipa moyo na kuomba kwani alikua akitioa sana katika kumtumikia Mungu. Baadhi ya watu walijitolea kumsaidia kwa kidogo walichokua nacho.
Alipata rafiki amabe pia alikua akipitia ktk hali ngumu kama yeye na wote walimpenda Mungu na walizidi kutiana moyo kua ipo siku mambo yatakua sawa.
Mtu mmoja alijitolea kuwalipia chumba cha kuishi na kuwapa jiko la kupikia. Lakini maisha yalikua magumu ukitegemea ni wasichana na wana mahitaji muhimu kama wasichana wengine na ingewezekana kabisa kujitolea kufanya mambo ya aibu ili wapate kipato kwani walikua ni wazuri wa sura na umbo pia lakini walimuheshimu Mungu na kujiheshimu sana.
Walijitahidi kuonyesha nyuso za furaha ili isiwe rahisi kwa watu kujua magumu waliyokua wanapitia lakini kwa wachache tuliokua tunajua tulielewa kinachoendelea kwani maisha ya mlo mmoja(yaani waliweza kula usiku tu na wakati mwingine asubh kama cha usiku kilibaki) ndiyo yalikua maisha yao ya kila siku. Kwa sisi narafiki zao jambo hili lilituumiza na tulijitahdi kwa kila tulipoweza kwenda nao lunch kwasababu walizoea kubaki darasani wakijifanya wanasoma wakati ukweli ni kwamba hawakuwa na hela ya chakula.
Hali iliendelea hivi hivi na tulipofika mwaka wa tatu binti ambae ninasimulia story yake baba yake hali ilizidi kuwa mbaya na ndugu wakashinikiza apelekwe kwa mganga wa kienyeji jambo ambalo binti huyu na mama yake hawakuliafiki kwani walimuamini Mungu. Siku moja ndugu zake walimchukua baba yake wakidai wanampeleka hospitali lakini badala yake wakampeleka kwa mganga wa kienyeji bila familia kujua.
Ilichukua muda hadi kufahamu kuwa baba yake alipelekwa kwa mganga wa kienyeji ambako jitihada za kumrudisha ziliznza kufanyika lakini mganga alikataa kumruhusu kwani kuna deni ambalo wale ndugu hawakulilipa kwa yule mganga.
Binti huyu akisaidiana na mama yake walijitahid kutafuta huku na kule na wakafanikiwa kulipa lile deni la TSH.70,000 na kufanikiwa kumtoa baba yao akiwa amedhoofu sana kutokana na ukksefu wa chakula bora na matunzo.
Wakati hili linapita tayari tukikua mwaka wa tatu na mitihani ilikarbia sana, binti huyu alipatwa na vidonda vya tumbo ambavyo niliamini kua vilitokana na msongo wa mawazo na kutokula. Tulikaa kama Fellowship(kikundi cha dini tulipokua tunaabudu pamoja) pale chuoni na tukajadikiana kuwa kama ni Mungu huyu tunaemwabudu sio sawa mwenzetu afe kwa njaa katikati yetu. Tulichanga fedha kwa kika kidogo tulichokua nach na kuweza kumpatia ili ziwasaidie ktk matumizi ya chakula na mengine madogo madogo.
Lakini zalipobaki wimi mbili tuanze mitihani binti huyu alinifuata na kuieleza jambo ambalo lilinishtua sana. Aliniambia kua alikua na deni analodaiwa kwenye ada TSH. 3,000,000 na aliniomba nimshauri nini cha kufanya kwani aliamini kabisa kuwa Mungu aliemsaidia siku zote atamsaidia hata sasa na atafanya mitihan yake kama watu wengine. Nilimshauri na kwa jinsi ilivyonigusa niliahidi kumuombea na nikajitolea sehemu ya pesa yangu ya matumizi ili kumsaidia na kumuelekeza kwa watu kadhaa ambao niliamini wangeweza kumsaidia.
Kama fellowship tuliomba kwaajili yake na kumtia moyo, pia kumsaidia ili kupunguza deni lake. Na jambo hili lilimgusa kila mtu kwani alijitoa sana ktk kumpenda Mungu na kumtumikia ktk fellowship na alipenda kumshukuru Mungu mara nyingi kila wakati alieleza ji si Mungu alivyo mwema kwake.
Mpaka inafika muda wa mtihani alimfuata kila mtu ambae alihisi angeweza kunsaidia na deni lilipungua na kubaki TSH. 1,900,000 . Chuo kilikataa kumpa namba ya mtihani ili kumruhusu kufanya mtihani kutokana na deni lake lakini alinipigia simu na kunieleza kua imaniayake ni kua atafanya mtihani nami nilimtia myo lakini yalikua yamebakia masaa machache sana tuingie kwenye chumba cha mtihan. Tulichukua hatua ya kumfuata mkuu wa kitivo na kumueleza tulipofikia kwani alilijua tatizo lake tangu mwanzo. Mkuu wa kitivo alijitolea kumdhamini afanye mtihani kutokana na kwamba kuna watu waliokuwa wameahidi kumsaidia kwa siku zilizofuata.
Baada ya kumaliza mitihani alimshukuru Mungu sana na alianza shughuli za kufuatilia waliomuahidi japo sio wote waliomsaidia. Kaka yake aliahidi kumsaidia kwani akikua amepata kazi na alitegemea kwa mshahara wake angeweza kumaliza deni lote lililobaki kwahiyo binti huyu alipata matumaini makubwa. Lakini kabla ya mwisho wa mwezi kaka yake alifukuzwa kazi na kushindwa kumsaidia tena.
Binti huyu alivunjika moyo na kukata tamaa na swali kubwa kwake lilikua, KWA NINI MIMI?
Baadae alipata watu wa kumtia moyo na wengine walimsaidia na kwa sasa ninavyotoa simulizi hii amebakiza deni la laki saba na sitini na tano elfu. Ameapply sehemu nyingi ili kuomba nafasi ya kazi ili aweze kupata fedha za kumalizia deni lake na kuisaidia familia yake lakini bado wanahitaji vyeti na matokeo yake ya chuo ambayo hawezi kupata hadi atakapomaliza deni.
Imani yake ni kwamba atahitimu na wanafunzi wengine katika mahafali yatakayofanyika siku chache zijazo na hajakata tamaa. Anaamini Mungu aliye ianzisha safari yake ataimaliza...
KWA MSICHANA YEYOTE ANAEPITIA HALI KAMA HII, USIKATE TAMAA KWANI MUNGU ANAJUA KILA UNACHOPITIA....
 
Duh!!! Mungu n mkubwa na mjuzi wa wajuzi
 
Maisha yanamikasa ya kila aina,lakini mwisho wake ni ushindi.
 
me ctosahau nlvyopgwa na kund la watu mtaan then wao wakawah polc ikawa bonge la kec kwangu.nkkumbuka nachoka kabsa
 
Duh...kumbe kuna watu wana matatizo zaidi yangu...Asante Mungu, nashukuru kwa mitihani unayonipa...sitokaa nikukufuru...
 
Back
Top Bottom