Hazina Muone haya, ni dhambi hii

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
4,162
794
Source ya hii taarifa si mtu baki ni Mimi mwenyewe.

Nashangazwa sana, nini kiliwalazimisha kufanya mlichofanya wkt huu wa sikukuu?.

Inawezekana hata January itakuwa hivi kwa kuwanaongozwa na mihemuko watu wa hazina kabla ya kukata mishahara ya watu kwa nini wasiwasiliane na idara husika. Pamoja na madeni ya huko nyuma sasa tuna deni hazina, upyaaa
..

Hatujala Xmas je mmeridhika? Ninawasihi kabla ya tarehe moja tupate pesa zetu.

walau kila wilaya nchini inawatu walionyimwa pesa mwez Nov,Dec nk. huu sio uungwana

oneni haya, mnaongozwa na nini katika maamuzi yenu?
 
Kama ni kweli kuwa watumishi wamesitishiwa mishahara, Mawaziri husika jiulizeni lengo ni nini, maana naona dalili za kuwafukuzisha watu kazi kutokana na kutoweza kufika kazini kwasababu hao wahanga hawatakuwa na nauli za kuendea kazini lakini pia uhai wao upo mashakani, je hazina haikuona ni busara kuwasiliana na wahusika kwa simu badala ya kuwaingiza matatizoni watumishi hao wa umma? nashauri.jambo hili litazamwe kwa namna tofauti vinginevyo athari zake zitakuwa mbaya
 
hawa jamaa hela zetu wanalipana hovyohovyo tu,overtime all,na alowance nyingi kibao.mpango tunaomba sitisha malipo yote nje ya mshahara.
 
Kama ni kweli kuwa watumishi wamesitishiwa mishahara, Mawaziri husika jiulizeni lengo ni nini, maana naona dalili za kuwafukuzisha watu kazi kutokana na kutoweza kufika kazini kwasababu hao wahanga hawatakuwa na nauli za kuendea kazini lakini pia uhai wao upo mashakani, je hazina haikuona ni busara kuwasiliana na wahusika kwa simu badala ya kuwaingiza matatizoni watumishi hao wa umma? nashauri.jambo hili litazamwe kwa namna tofauti vinginevyo athari zake zitakuwa mbaya

hii ishu imekaa kana kwamba haipo, tena dec krismas, na Jan ada za watoto. imekaa vibaya sana
 
Tatizo lipo kwa maafisa utumish husika ama hazina?

Kilichotokea ile history sheet ya mtumishi ina tarehe ambayo si sahihi ya kustaafu. Matatizo makubwa ni maafisa
utumishi, hawajui kazi zao, ku-apdate historia za wafanyakaz
na kuituma hazina. Sasa wamesababisha usumbuf mkubwa

kwa mfano ulizaliwa 1960+60=2020

Sasa ama hazina au utumishi hawakutekebisha

Wakati wanatoa mishahara huandaa salari slip na kwa kuwa hazina hawana hii taarifa wao wametoa history kwamba

Mtumishi atastaafu 1960 ambayo wameupata ama kwa kujumlisha 1900+60 au vyovyote walivyofanya.

Sasa wafanyakaz hawa wanaonekana washastaafu.

Hicho ndicho chanzo cha kuzuia pesa za Manesi,Walimu,Madaktar,Mabwanashamba nk. kila halmashauri si chini ya watu 200 swali ni kwamba walikuwa wapi siku zote?

Wanamfanyiana sabotage magufuli aonekane hafai
 
Je wew unayelalamika mwajili wako anajua? Na unapolalamikia Hazina usikute tatizo liko utumishi
 
Back
Top Bottom