Mifumo mingi ya IT inayotumika nchini ni mibovu, eGA mnaikagua hii mifumo kabla haijaanza kutumika?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Tanzania imeingia kwa kasi kwenye e-service lakini imekosea kufanya miradi hii bila kuwateua wasimamizi wazuri.

Ipo mifumo tunayotumia ambayo ukiiangalia tu wakati unaanza kuomba huduma au ukipitia mchakato wa kupata huduma utagundua watengenezaji wa mifumo hii si wataalam wa mifumo au walifanya kazi chini ya kiwango.

Natamani kufahamu mfumo wa Dawasco, mfumo wa lostcase wa polisi, mfumo wa pasipoti wa uhamiaji na visa, mfumo wa NIdA, mfumo wa TRA, websites za idara na wizara za serikali zinakaguliwa kabla Taarifa au hazijaanza kutoa huduma?

Jaribuni kuomba huduma kwenye mifumo hii au pitieni websites za seriakali utabaini hakuna watu serious wanaosimamia mitumo hi na hata ikiwa haifanyi kazi hakuna anayejua.

Ila Sasa najiuliza, Kama Mimi mwomba huduma naona mapengo mengi kiasi hiki kwa miaka mingi je huko ndani ya mfumo hakuna uwezekano wakudukuliwa? Tukumbuke hii mifumo ipo worldwide na si ya ndani humu.

Mfano ukitaka kuungia Tanzania unakuta visa inasema kuna mipaka sijui mitatu au minne na yote Ni lazima uje kwa ndege ila nonavyojua Mimi nchi hii hata ukitaka kuingia kwa maji au mipaka ya ardhini inawezekana, je watalii tunaowazungumzia hapa hatuwadanganyi?

Mtu yupo Kenya anataka kupita kwa bus anaambiwa na mfumo ashuke KiA au Daresalaam kwa ndege kweli? Watengeneza mifumo ya aina hii na wasimamizi wanafanya Nini ofisini? Wanaweza kuzuia wasidukuliwe Kama haya hawayaoni?

Dawsco Wana mfumo unapeleka bili za mamilioni kwa wateja kila kukicha, unafika ofisini wanakuambia lipa kiasi hiki ilo Deni tutalitoa, najiuliza watu wa hesabu wanawezaje kuziba pengo la bili hewa Kama mfumo unatoa taarifa zisizo sahihi? Hatupigwi?

Nida mfumo unahudumia wateja hawapati namba na kila saa mfumo upo down kuanzi kwa wateja na wananchi. Watu wanasajili lini halama za vidole hazionekani

Websites zinataarifa za mwaka juzi nyingine zikiwa Ni websites za taasisi za kibiashara. Namba zakupata huduma zilizowekwa kwenye websites ni landlines ambazo hazipatikani most of time, kwanini ttcl wasitoa mobile namba kwa taasisi na ziwekwe vocha wafanye biashara? Leo hii kweli landline ndo main number kwenye websites?

Landlines zenyewe unapiga anayepokea akujibu anakuambia subiri akuunganishe na boss....kwanini kusiwepo na madawati ya huduma na hizo namba zao ziwekwe kwenye websites?

Inshort serikali imeingia kwenye e-service ikiwa na watu wenye mentality za manual systems na hakuna anayeshtuka. Hapa pakifanyiwa study upo uwezekano serikali ikawa imepigwa fedha nyingi sana kuanzia kwenye ukandarasi wa mifumo, utoaji wa tenda, utoaji elimu kwa watumiaji, ununuzi wa vifaa na usimamizi wa mifumo yenyewe.

Nchi za wenzetu Kati ya eneo linalokodolewa macho ni hili kwa sababu watu wanapiga sana pesa. Nashawishi serikali ifanye ukaguzi maalum itagundua tumeibiwa fedha nyingi sana katika eneo hili.

Lakini pia hazina wajaribu kuangalia Kama hii mifumo inatumika kulipa ipasavyo fedha za serikali? Maana kwa mfano tu wa dawsco system naamini Kuna matundu yakupiga yametengenezwa huko kwenye control number na yawezekana huko nje wapo watu wanatukua bila sisi kujua.

Nawasilisha kwa Waziri mwenye dhamana afanye kiti eneo hili atanishukuru siku moja ....tusisherekee technology
 
Zaidi ya yote, hivi zile contact info kwenye site zao huwa wanaweka za nini?

Unatuma email leo unajibiwa baada ya wiki mbili hadi tatu na zingine hujibiwi kabisa.

Unapiga simu namba haipatikani, ikipatikana inaita tu hakuna wa kupokea, ikipokelewa anayepokea hana ujuzi wowote na mambo IT anakuambia nitumie taarifa zako au subiri kidogo ukimuuliza maswali bado majibu ni ya kisiasiasa tu.

Mambo ya technology kwetu TUMELAZIMISHWA kutokana na mabadiliko ya ulimwengu na technology in general hivyo tunatekeleza japo bado uwezo na uzoefu hatuna na hata wataalamu wenyewe ni wazee wa copy and paste kutoka project zingine, we are good in editing asikuambie mtu.

Kuna ofisi moja bosi anatoa ripoti kupitia iPad na kuwakabidhi wafanyakazi iPads ili iwe rahisi kufuatilia ripoti wao waliona kama wamedharauliwa kwanini boss asi print ripoti akawapa hardcopy??
 
Umewaza vyema sana kuhusu mitumo ya serikali, kwa kweli websites nyingi za serikali zimedumaa kwa sababu wafanyakazi wenye wenye age above 35 awajui chochote kuhusu technology
Websites nyingi ndiyo milango yakuomba huduma na zikigoma Basi uwezi kupata huduma.

Lakini pia malipo mengi yanafanyika kwa njia ya mtandao, lakini sidhani Kama Kuna utafiti au auditing inafanyika kuonyesha kwamba fedha zinaingia serikalini.

Ila tunalotatizo pia la wateule wa Mhe, kushindwa kumsoma mteuzi wake hasa katika eneo la Tehama. Wengi wa wateule naamini Leo hii wakihojiwa kuhusu mifumo wanayoisimamia awatakuwa na lakujibu.

Eneo la Tehama naamini linaweza kuwa lango kuu lakupigia fedha za serikali, computer inauzwa usd 500 sokoni ila inaandikiwa usd 1000,

Vifaa vingi tunapigwa kwa sababu hatuajui bei.

Mifumo mingi tunapigwa kwa sababu wanaosimamia mifumo hiyo Awana uchungu nayo na Wala siyo wataalamu ni watu wamepewa tu kwa sababu ya ukubwa wao.

Nina kiu yakuona eneo la Tahama linafanyiwa auditing tuone tunavyopigwa na weusi wenzetu kwa kujificha kwenye taalum hii
 
Hata barabara zenyewe ni mbovu, na hata utendaji wa serikali ni wasifa na ulimbukeni
 
Back
Top Bottom