Hayati Magufuli ndiye aliyeimalizia kuiua CCM hadi kufikia sio tu kuogopa uchaguzi bali hadi kuogopa kivuli tuu cha CHADEMA

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Dunia nzima kwa sasa hakuna serikali inayo weza kutawala nchi bila ushirikiano na wapinzani labda iwe ya kidikteta halisi au kidikteta uchwara. Nchi nyingi zinatumia mfumo wa serikali za mseto kulingana na uwiano wa uwakilishi wa viongozi walio chaguliwa ktk vyama mbalimbali.

Faida ya kuwa na serikali ya umoja ni kwanza kuheshimu demokrasia na ya pili ni kupunguza minyukano na misuguano baina ya viongozi au wananchi hususani ktk vyama vinavyo onekana kupata idadi kubwa ya kura na uwakilishi wa wananchi.

Ccm kwa sasa haina tena mvuto kwa wananchi inatumia polisi na wizi wa kura kusalia madarakani na ni jambo baya na hatari kwa ccm yenyewe kuliko wapinzani. Hii ingekuwa turufu yake ya mwisho ili kuwaonesha wananchi kuwa wao hawana uchu wa madaraka na pia ingekuwa ni njia nyingine kwa wananchi kuwasoma wapinzani uwezo wao na udhaifu wao.

Ccm msijidanganye kuwa mnakubalika hata kama mngekuwa mnawatendea watu mambo mazuri sana kupita kiasi bado binadamu huwa anahitaji uhuru na shauku ya kuchagua au kupenda kitu tofauti na kile alicho nacho.

Kama Mungu alimpa Adam na Eva bustani iliyo sheheni kila kitu lakini wakatamani kula tunda la mti mmoja tuu ambalo wamezuiwa wasile sembuse ninyi ma ccm majizi na makatili wakubwa watu wawapende kwa lipi hasa mnalo jiona ni la kipekee kwenu wakoloni Makabulu ninyi?

Maji hayapimwi kwa miguu Mwenda zake aliwahadaa kwa kuogopa matokeo ya uchaguzi ambayo kivuli chake bado kinaishi. Kama cccm mmefikia hatua ya kuogopa BANGO tuu linalo onesha CHADEMA wamezindua mradi kwa nguvu ya wananchi mna hali ngumu. Kama bango la chadema linaogopwa kwa kiasi hiki je Chadema yenyewe? Uchaguzi je mnaogopa je? Tunapata sasa majibu kwa nini mliengua wagombea wa upinzani na kuvuruga Uchaguzi mkuu uliopita.

Nyerere aliwahi sema hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo. Chadema ipo tena na wananchi ina nguvu na inapendwa. Karne hii hamuwezi tena kuishi kwa propaganda za kutishana na uzushi. Watu wanataka Uhuru haki demokrasia na maendeleo ya watu. KATIBA MPYA NI SASA.
Na maendeleo hayana vyamaa.
 
Alipata 86% ya kura za Urais , akasaidia kupata 99.2 ya wabunge wa kuchaguliwa 88% ya wabunge wa viti maalumu na akasaidia kupata 92 ya viti vya udiwani na hapa simzungumzii Yeyote ila ni Hayati Magufuli. Apewe maua yake
 
Alipata 86% ya kura za Urais , akasaidia kupata 99.2 ya wabunge wa kuchaguliwa 88% ya wabunge wa viti maalumu na akasaidia kupata 92 ya viti vya udiwani na hapa simzungumzii Yeyote ila ni Hayati Magufuli. Apewe maua yake
Shetani anapewaje maua zaidi ya moto wa jehanamu ??
 
Alipata 86% ya kura za Urais , akasaidia kupata 99.2 ya wabunge wa kuchaguliwa 88% ya wabunge wa viti maalumu na akasaidia kupata 92 ya viti vya udiwani na hapa simzungumzii Yeyote ila ni Hayati Magufuli. Apewe maua yake
Ule ulikuwa uchaguzi kwa akili zako au umesimuliwa na wazee wa bao la mkono?
 
Back
Top Bottom