Hayati Magufuli na Nape Nnauye walipoteza upendo wa Wananchi kwa Bunge lao

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
Miaka ya 2010 hadi 2015 bunge la JMT lilikuwa ni kivutio cha wananchi kulitazama.

Mara baada ya kuingia madarakani kwa utawala wa awamu ya tano wakalivuruga Bunge.

Kitendo cha kufunga bunge lisionyeshwe live ilikuwa ni pigo kubwa na ugonjwa mkubwa uliowafanya wananchi kulipuuza hilo Bunge.

Na hata baada ya kuruhusu bunge lionyeshwe live bado watu wameendelea kulisusia kulitazama.

Hakika kwa hili Jiwe na Nape mnalo jambo la kuwajibu wananchi kwanini mliamua kutufanyia uhuni huo.
 
Hata leo amejikuta mwenyewe hakuna mwenye kutaka msikiliza,lakini alivyofanya awamu ile hakujua mambo yatamgeukia, na ataona atauhitaji tena uhuru wa habari 😂. Laana yake ni kuasisi zile sheria za mwendo kasi na kuhujumu uhuru wa habari, wanahabari na mawasiliano huru ya raia🤔
 
Miaka ya 2010 hadi 2015 bunge la JMT lilikuwa ni kivutio cha wananchi kulitazama.

Mara baada ya kuingia madarakani kwa utawala wa awamu ya tano wakalivuruga bunge.

Kitendo cha kufunga bunge lisionyeshwe live ilikuwa ni pigo kubwa na ugonjwa mkubwa uliowafanya wananchi kulipuuza hilo bunge.

Na hata baada ya kuruhusu bunge lionyeshwe live bado watu wameendelea kulisusia kulitazama.

Hakika kwa hili Jiwe na Nape mnalo jambo la kuwajibu wananchi kwanini mliamua kutufanyia uhuni huo.
nadhani kuna mambo mengi ambayo yamewafanya wananchi kulisusia bunge.moja ni kwa sababu bunge hilo halitokani na ridhaa ya wananchi,pili bunge kutojadili mambo yanayowakera wananchi katika majimbo yao,na ni mpaka hapo bunge litakapotokana na ridhaa ya wananchi ndipo wananchi hao watakaporudisha matumaini ya kuliangalia live.
 
Hata leo amejikuta mwenyewe hakuna mwenye kutaka msikiliza,lakini alivyofanya awamu ile hakujua mambo yatamgeukia,na ataona atauhitaji tena uhuru wa habari
Kipindi kile kama kawaida walikuwa wanafanya kazi ya kumtukuza na kumkubalia mteuzi wao.

Hawakujua kesho yao itakuwaje.
Leo hii bunge lipo live lkn hakuna mwananchi anahangaika kupoteza muda wake kuliangalia
 
nadhani kuna mambo mengi ambayo yamewafanya wananchi kulisusia bunge.moja ni kwa sababu bunge hilo halitokani na ridhaa ya wananchi,pili bunge kutojadili mambo yanayowakera wananchi katika majimbo yao,na ni mpaka hapo bunge litakapotokana na ridhaa ya wananchi ndipo wananchi hao watakaporudisha matumaini ya kuliangalia live.
Naunga mkono hoja yako mkuu nadhani sasa ni muda muafaka kwa wananchi kujaribu tena bila kuchoka kufanya maamuzi yao 2025.
 
Back
Top Bottom