Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
Anaandika Deogratius Kisandu kutoka huko FB, nimependa kuwashirikisha,
HAYATI Aboud Jumbe ALIWEKWA VIZUIZINI KWA WIVU WA KIJINGA NA UNAFIKI.
Wapinzani nchini walikuwa wakipiga kelele kuwa Rais wa zamani wa Zanzibar Mh. Aboud Jumbe yuko Kigamboni amewekwa vizuizini tangu utawala wa Mwalimu Nyerere yaani awamu ya kwanza. Kelele hizo hazikusaidia kitu maana Serikali ilikuwa ngumu kujibu tuhuma hiyo ya kweli. Cha kusikitisha alipofariki tu Mzee Jumbe tukatangaziwa kuwa Mzee kafariki huko kwake Kigamboni na mazishi yatafanyika Zanzibar.
Lakini Mzee Jumbe aliacha wosia akisihi Serikali isihusike kwenye mazishi yake na wala kwa lolote. Lakini Rais wetu Mh. John Magufuli alipoenda Zanzibar alidhuru kaburi la ndugu yetu Jumbe.
KWA NINI Jumbe VIZUIZINI?
Mzee Jumbe katika ujana wake alikuwa ni moja ya vijana wenye maono mazuri sana ya kujenga Taifa letu, katika uhalisia walikuwepo wengi tu na wengine waliibuka baadae lakini hapa namzungumzia mmoja wa waasisi wa kutaka tuwe na mfumo wa Serikali tatu.
Jumbe alikuwa na maono mazuri sana ambayo yalisaidia sana kujenga umoja wetu wa Tanganyika na Zanzibar. Kitendo cha yeye kuonekana bora kwa kila idara na kushindwa kumzima, ndipo maadui zake wakatafuta mbinu ya kuzima mshumaa wake.
MAADUI WALICHONGEA NINI?
Maadui wa Jumbe walitengeneza propaganda za kubumba na kumfikishia MWL. Nyerere, katika Uongo huo uliokuwa umesukwa hasa, wakamwambia MWL. Nyerere kuwa Jumbe anataka kuja kupindua Nchi na wengine Jumbe anania mbaya sana na anataka kuvunja muungano na mambo mengine mengi tu. Lakini wao walichofanya ni kupandikiza chuki kwanza kwa jamii ili waamini kinachopandikizwa na walipoona jamii imeamini ndipo wakapeleka uongo wao Ikulu ili awekwe VIZUIZINI. Walichokifanya ni kutafuta sababu ambayo haiepukiki. Yote haya ilikuwa ni wivu kwa kuwa Jumbe alikuwa Jiniazi sana katika mambo mengi. Mwalimu aliiamini timu ya upelelezi ambayo kimsingi ilikuwa ni propaganda na wivu.
KWANINI JUMBE ALIGOMA SERIKALI KUSHIRIKI MAZISHI YAKE?
Hayati Jumbe alikataa kabisa Serikali kushiriki mazishi siku akifa maana alijitahidi sana kueleza ukweli wake mbele ya viongozi wa Serikali lakini hawakutaka kumsikiliza kabisa. Kuna wakati Mwalimu alitaka kumuachia lakini idara husika iligoma kabisa. Yote haya ilikuwa ni wivu kuwa wakimuachia atawazidi nguvu.
KWANINI Rais MAGUFULI alienda kaburini Kwake?
Hapa ndipo unakuja kujua kuwa Jumbe hakuwa na makosa, Rais wa awamu ya Tano pamoja na hayati kuichukia Serikali lakini Rais alionesha kuguswa ama na historia ya Jumbe au msiba wa Mzee Jumbe. Kwa kweli si kila anayeenda jela anahatia, wengi ni mizengwe na kubambikwa tuhuma.
ANGALIZO:
Tuache kufanyiana unyama kisa Fulani Mungu kambariki kwa karama za hekima na maono ya kiuongozi.
Leo hii wachawi wanasema tuweke historia tena ya kumchongea Deo Kisandu ili wampeleke Kigamboni detention. (Wajinga ninyi hamuniwezi labda kama mnataka Mungu alete maafa)
Deogratius Nalimi Kisandu
Mtemi Kiongozi wa ACA tarajiwa.
11 February 2017.
Deogratius N Kisandu | Facebook