Haya utayakuta Tanzania tu, sio mahali pengine

sakapambo

JF-Expert Member
May 10, 2015
502
150
KWANINI TFF WANATAKA KUMHUJUMU
SAMATTA??


By Malisa GJ,

Hii nchi kuna watu wanapaswa kufungwa au
kupewa adhabu kali iwe fundisho. Miongoni
mwao ni Rais wa TFF Jamal Malinzi na safu
yake ya uongozi. Ningekua na mamlaka
Malinzi leo angelala "Keko au Segerea"..

Mbwana Samatta ameleta HESHIMA KUBWA
sana Tanzania ambayo viongozi wa kisiasa
wameshindwa kutuletea kwa miaka zaidi ya
50. Ushindi wa tuzo ya Mwanasoka bora wa
Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za
ndani ni ushindi mkubwa sana kwa taifa letu.
Samatta ameitangaza nchi yetu kwa kiwango
kikubwa sana. Waliokua hawaijui Tanzania sasa wataijua bila kupenda.

Brother Anthony Mtaka ambaye ni mwanasiasa hodari, msomi na miongoni mwa watu wachache ndani ya CCM wanaonivutia
kisiasa; amesema kuwa Samatta ametangaza
Tanzania vizuri kuliko viongozi wa Serikali
waliotumia mabilioni ya fedha kwa miaka
kumi mfululizo (2005 -2015) kutangaza vivutio
vya utalii na wakashindwa.

Ni wazi kuwa heshima aliyotupa Sammata ni
kubwa sana na tunapaswa kuheshimu
mchango wake hasa ukizingatia kwamba amefika hapo kwa juhudi binafsi. Sio TFF wala Serikali zilizochangia mafanikio ya
Sammata. Ni yeye mwenyewe na Mungu wake.

So ilitakiwa TFF waweke utaratibu mzuri wa
kumpokea Samatta kwa heshima. Ikiwezekana
watu wafanye maandamano ya amani kuanzia
pale Airport hadi mahali watakapokusanyika.
Kama tunaandamana kwa sababu za kisiasa
kwanini tusiandamane kumpongeza
mtanzania mwenzetu aliyeitangaza vema nchi
yetu kimataifa?

Tena ingepaswa tuwe na Media Campaign
maalum ya kumpongeza Samatta. Na tufanye
"hashtag" kwenye mitandao ya kijamii kama
FB, Tweeter, Instagram etc. Tujenge
ushawishi watu wajitokeze kwa wingi uwanja
wa ndege wa JNIA hadi Samatta mwenyewe
asikie fahari na ajivunie kuwa Mtanzania.

Lakini cha ajabu TFF kwa kushirikiana na
CAF wameamua kumhujumu Samatta. Na
serikali imekaa kimya as if nothing is gojng
on. Rais wa TFF Jamal Malinzi ameandika
kupitia ukurasa wake wa Tweeter kuwa
Samatta atatua nchini saa 8 za usiku kesho
jumamosi. Seriously?? Saa 8 usiku??
Apokelewe na "wanga" au??
Rafiki yangu Ezekiel Kamwaga amehoji
kwanini isitafutwe ndege ya saa 4 asubuhi
kesho ili watu waweze kujitokeza kwa wingi
kumpokea? Hivi kweli hatuwezi kum-market
shujaa wetu?? Kama tulishindwa kumsaidia
kufika hapo alipofika, hata kumfanyia
marketing tunashindwa? Hivi mnadhani
Samatta angekua Mkenya angepokelewa saa 8
za usiku?? TFF kuweni serious kidogo, acheni
ujinga.!

Saa 8 za usiku watu wanakoroma vitandani,
wengine wako club wameshalewa "ndovu
baridi" ndio mmeona ni muda mzuri wa
kumpokea Sammata? Wanaopokelewa usiku
wa manane ni "majambazi na wanga" sio
shujaa kama Samatta.

Halafu Malinzi kwa kujishtukia anajaribu
kupunguza ukali wa maneno na kusema eti
Samatta atatua kesho "saa 8 alfajiri". Hakuna
kitu kinachoitwa "saa 8 alfajiri" kwenye
Kiswahili. Ni saa 8 usiku. Alfajiri inaanza saa
11. Sasa hiyo alfajiri ya Malinzi ya saa 8 usiku
ameitoa wapi?
Pia utetezi wa Malinzi ni wa "kitoto sana". Sio
utetezi wa kiongozi tena wa taasisi kubwa
kama TFF. Malinzi anasema saa 8 usiku ndio
muda ambao Samatta amekatiwa ticket na
Shirikisho ls Soka Afrika (CAF ) ambao ndio
waandaaji wa tuzo hizo. Hivi kwani kila
wanachofanya CAF lazima tukubaliane nacho
bila kuhoji?
Ilipaswa TFF wajiulize kwanini CAF
wamemkatia Samatta ndege ya usiku wakati
ndege za asubuhi au mchana zipo.?? Jibu ni
rahisi tu kwamba CAF wanaendeleza juhudi
zao za kuhujumu nchi za Afrika Mashariki.

Hawapendi kabisa kuona nchi zetu za Afrika
Mashariki zikifanikiwa kisoka. Ndio maana
hata kwenye michuano ya kimataifa wamekua
wakitupanga na timu ngumu kama "Ghana,
Senegal, Cameroon, Algeria, Misri, Nigeria"
etc ili tusifike mbali.

Kwahiyo hili la kumpangia Sammata kurudi
saa 8 usiku sio bahati mbaya. Itz a planned
and organized matter. Lengo lao tushindwe
kumpa Samatta mapokezi mazuri na ya
heshima. Kwahiyo ilitakiwa viongozi wa TFF
waione hujuma hii na waikatae.
Sifa ya kiongozi ni kuona pale ambapo
wengine hawawezi kuona (A Leader must be
able to see where others cannot see). So TFF
walitakiwa waone kuwa muda aliopangiwa
Sammata (saa 8 usiku) ni hujuma za CAF,
then wafikirie mbinu mbadala ya kukataa
hujuma hiyo. Ikiwezekana kumfanyia booking
upya Samatta ili atue nchini Asubuhi, Mchana
au jioni muda ambao watu wengi wanaweza
kujitokeza kumpokea.
Lakini viongozi wa TFF wanakaa na vitambi
vyao vya "Castle lite" wanakubaliana tu na
CAF bila hata kureason kidogo. Huu ni ujinga
ambao hata Mwenyekiti wa "wajinga duniani"
hawezi kufanya.
Ingekua Samatta ni MKenya; kwanza
wangekataa hiyo ticket ya CAF ya saa 8 usiku.

Then wangemfanyia booking upya Samatta
kwa pesa zao ili aweze kutua kwa muda
wanaotaka wao. Na ingewezekana
wangemtumia hata ndege maalumu ya
kwenda kumchukua.
Lakini hapa bongo TFF wamekaa tu kama
"mazuzu" wanakimbilia kuandika Tweeter bila
aibu eti Samatta atatua kesho saa 8 usiku.
Nani akampokee saa 8 usiku?? Labda Malinzi
na familia yake.



MY TAKE.!
Natoa wito kwa watumiaji wote wa mitandao
Tushikamane kwa umoja wetu bila kujali
vyama vyetu, dini, kabila au timu
tunazoshabikia, tupige kelele mitandaoni
kuhakikisha Samatta anatua nchini muda
ambao watanzania tunaweza kwenda
kumpokea.

Kama itakosekana ndege ya kesho mchana
bora aje Jumapili asubuhi kuliko kuja hiyo
kesho saa 8 usiku. Share ujumbe huu, mtag
kiongozi yeyote wa Serikali au wa TFF. Kama
una namba zao wapigie au watumie sms
kuonesha kulaani hujuma inayotaka
kufanywa dhidi ya Sammata ya kumpokea saa
8 za usiku. Natoa wito pia kwa Serikali
iingilie kati suala hili. Mpigieni # Nappe
mwambieni hatuko tayari kumpokea Samatta
saa 8 za usiku.


Tunamtaka Sammata muda ambao tunaweza
kumpokea sio saa 8 za usiku.
 
umenena mantiki tupu. malinzi unalo hilo, hukwepi. chukua hatua mara moja kuyatendea kazi haya kuhusu samatta. kwa tukio hili la kumpokea shujaa wetu samatta, lifanyike asubuhi au mchana au jioni na si usiku mnene saa 8. hizo ni saa za wanga kufanya vitu vyao na sisi ni mashabiki wa soka, muda huo hautufai. ok?
 
Niliwahi kusema nyakati flani wakati Malinzi anagombea urais TFF kuwa hafai, tutamkumbuka Nyamlani.
 
Hujuma za CAF ndio hujuma za TFF wote hawajapenda Mafanikio ya Samatta,ndiyo maana baada ya kumbana Malinzi ameishia ku edit kutoka saa 8 usiku to saa 8 alfajiri..ukiangalia sana hata Ushiriki wa Samatta kwenye tuzo haujawa promoted sana na vyombo vya habari vya ndani ya nchi yetu.
 
Leo ndiyo unajua kuwa malinzi ni kanjanja katika soka letu.
 
Hoja yako imeshiba kweli kweli lakini sasa tatizo ni hao waliopewa dhamana ya kusimamia soka letu wanaoitwa TFF kama wana utashi nalo.Hii ni miongoni mwa taasisi bomu kabisa Tanzania.Sasa kwenye hili la Samatta tunashuhudia TFF walivyoshindwa kujiongeza hususani kulitazama kiuzalendo zaidi.Lakini haishangazi sana kwani hata FIFA na CAF siasa zipo,lakini ni SIASA MASLAHI.
 
Tunakesha bar tunashindwa nini kwenda kukesha airport kumpokea Sammatta ili tuwakate vilimi wenye husuda na mafanikio yake.
 
Back
Top Bottom