Haya TANZANIA simama na useme CHINA ni msema kweli na MMAREKANI ni muongo.

Aaron

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,019
4,693
Wana jukwaa tangu juzi tumekuwa tumeshuhudia ubalozi wa china kutembelea visiwani zanzibar na kusema uchaguzi ulifanyika ulikuwa wa huru na haki..
wakati huo huo marekani kupitia MCC pamoja na mengine wamesema uchaguzi wa zanzibar haukuwa wa kidemokrasia..
serikali yetu imepokea kauli zote mbili za mchina na mmarekani lakini za mchina zimeonekana za ukweli kuliko za mmarekani...
sasa serikali yetu simameni na mseme marekani anapotosha ulimwengu.
 
Sasa Marekani wanapotoshaje Ulimwengu wakati kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana walituma waangalizi wao kwenye uchaguzi huo na wakapeleka mrejesho kwao kwa kuandika taarifa zao kuwa uchaguzi huo ulikuwa HURU na HAKI?

Kwa maana hiyo uchaguzi wa marejeo wa jecha ulikuwa wake binafsi na chama chake cha CCM ambapo walikuwa wanafanya uchaguzi wao wa kuchagua viongozi wao wa chama na haukuwa na hadhi na uhalali wa kuitwa kuwa ni uchaguzi mkuu.

Hao wachina wamejifanya 'vipofu' na kudai uchaguzi wa marejeo wa Jecha wa tarehe 20/03/2016 kuwa ulikuwa huru na haki, kwa kuwa nao wanabembeleza mikataba yao ya 'magumashi' ya gesi waliyowekeana na JK isije ikabumbuluka.
 
Back
Top Bottom