Ya "Forum on china-africa cooperation-focaf, fikra pana za balozi mbelwa kairuki, 4 r's za rais samia na usafirishaji wa kahawa yetu nchini china

Mkunazi Njiwa

JF-Expert Member
Apr 22, 2023
7,449
6,574
Ada ya wastaarabu ni kupongeza mazuri na kwa wafanyao mazuri.

Nimewiwa kumpongeza sana Balozi wetu wa zamani nchini China ,mh.Mbelwa Kairuki- 2017-2023 (sasa balozi Uingereza) kwa maono yake makubwa , ya mbali na uzalendo wake adhimu juu ya taifa letu.

Sababu za kumpongeza Mh.Mbelwa Kairuki:
-----------------------------------

Alipokuwa mwakilishi wetu huko China alikuwa anapambania sana soko la kahawa yetu ,iko siku alihojiwa na idhaa ya kiswahili ya Ujerumani(DW) akafafanua yaliyojiri katika "EXHIBITION" yetu ya kahawa nchini China kupata wahitaji wengi ,miongoni mwao wafanyabiashara na wamiliki wa hoteli.

Kahawa yetu Robusta na Arabica ni ya kiwango kizuri na bora mno.Wadau hao walikosoa baadhi ya mambo yetu mathalani wakisema UHITAJI umekuwa mkubwa mno kuzidi upatikanaji wa kahawa yetu.

Kwa kutafuta tiba ya hilo ,mh.Balozi Mbelwa Kairuki akaiambia "DW" kuwa Tanzania kama nchi tutaendelea kutengeneza MAZINGIRA mazuri katika kilimo ili kuongeza uzalishaji wake na usafirishaji wake.

Kwa maneno haya ,watoto wa mjini tunasema kuwa balozi "aliupiga Mwingi "kazi yake aliifanya ipasavyo na kilichopo ni wizara ya kilimo na washika dau wa mnyororo wa thamani ya kahawa kuendelea kuyafanyia kazi mawazo hayo tunduizi.

Ukiachana na zao la kahawa ,kwa ujumla mh.Balozi Kairuki ametengeneza mazingira bora sana ya uhusiano wetu huko China na leo ushiriki wetu katika "FOCAC" una mchango wake wa kutukuka na AHONGEREKE kwa hayo

Taifa letu ni la 26 kwa kuzalisha kahawa duniani .

Mchaganuo wa bei ya kahawa ya Robusta na Arabica katika mabaraza tofauti :
---------------------------------

AUCTION

Arabica safi - dola 5.5/kg, tarehe3/9/24
Robusta safi -dola 4.9/kg ,tarehe 3/9/24.

MASOKONI

Marekani ,New York dola 5.5 /kg

Uingereza ,London dola 4.7/kg

NYUMBANI FARM GATE (TZS/Kg).

H/Arabica na maganda 4,227
Robusta na maganda. 4,886
Arabica HP 7,129
Arabica (CPU) 8,911

Data za COMTRADE zinaonyesha kuwa tunasafirisha kahawa ya dola milioni 2.8 (takwimu za 2023).


4R's za mh.Rais Samia Suluhu Hassan
------------------------------------
Tumekwenda katika "FOCAC" kifua mbele kwa kutegemea makubwa juu ya mahusiano yetu na nchi hiyo ,yako mambo mengi tunategemea wawakilishi wetu watayasimamia kwa lengo la kuzidi kulithubutisha taifa letu KIUCHUMI kwa mwamko wa maendeleo ya viwanda (aliyoasisi hayati Rais Magufuli),uboreshaji wa miundombinu ya kisasa,kutafuta wawekezaji bora katika biashara na tasnia ya kilimo kwa ujumla.

Mh.Rais Samia Suluhu ana malengo bora na makubwa ya kuiendeleza nchi yetu pale alipoiacha mwanamwema wa Tanzania El Commandante JPM....kwa yale maono makubwa ya Magufuli na hima aliyonayo amiri jeshi wetu pamoja na Rais wa Zanzibar ,Dr.Hussein Mwinyi ni matarajio yetu tutapiga HATUA KUBWA ya kimaendeleo kuliko vile tulivyofikiri pale alipoapishwa na kuanza kazi MAGOGONI na CHAMWINO.

Nimalizie kwa kuwatakia kila la heri washiriki wote wa baraza hilo la "FOCAF" nasi tukiwakilishwa na watu walioaminiwa na katiba yetu adhimu ya JMT na umma wa watanzania.

Mwenyezi Mungu ambariki na kumhifadhi Rais wetu Dr.Samia Suluhu Hassan yeye na watendaji wake ,aaaamin aaaamin

#Nchi Kwanza
#Serikali mbili za JMT milele dumu ,aamin
View attachment 3085946View attachment 3085947View attachment 3085948View attachment 3085950View attachment 3085951
 
"Preliminary meeting" hushirikisha wanachama wote kupanga AGENDA za mkutano mkuu wa "forum" hiyo....

Ni tofauti na wengine ambao AGENDA zinapangwa na "wakubwa" na wengine kazi yao ni "kuziingia tu".....

#FOCAC na usawa kwa wote
 
Back
Top Bottom