Haya si matumizi ya mali za serikali kwa manufaa ya chama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya si matumizi ya mali za serikali kwa manufaa ya chama?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Mar 23, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nimefuatilia kwa karibu sana Tangazo linalorushwa na REDIO CLOUDS linalowahamasisha wapenzi wa CHADEMA kukichangia chama hicho nami nikiwa miongoni mwa wakereketwa wa kuchangia chama hiki ambacho kinaonekana kuja juu sana katika medani ya kisiasa. Lakini kilichonishangaza Kipande cha wimbo wa Taifa ndani ya tangazo hili.

  Je ni sahihi chama cha siasa kutumia wimbo wa Taifa kujitangaza wakati wimbo wa Taifa ni chombo cha mali serikali na kwa maana hiyo ni mali ya vyama vyote vya siasa? Haya si matumizi ya mali za serikali kwa ajili chama kujipatia umaarufu?

  Watanzania tunajua na tumezoea kuusikia wimbo wa Taifa Wkati Kiongozi mkuu wa Nchi akihutubia, wakati kuna sherehe za kitaifa, wakati kuna taarifa mbaya inatolewa na Mkuu wa nchi kama ilivyokuwa wakati tunaarifiwa kifo cha baba wa Taifa na vile vile wakati nchi inatangaziwa hali ya hatari kama vita n.k

  Iweje leo wimbo wa Taifa uchezewe na vyama vya siasa kujitafutia umaarufu tena kwa kuwahadaa wananchi kuwa wananchangisha pesa za kuendeleza chama wakati pesa hizo zinapotelea kwenye matumbo ya wachache.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Serikali ni nini? Anza hapo kwanza kujibu
   
 3. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mi ndio ringtone ya simu yangu
   
 4. S

  Saas JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Matumizi mabaya ya mali za Serikali kwanza anza na chama kilichoko madarakani otherwise akili yako inaonekana tu kama nazi za pale magogoni
   
 5. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,767
  Trophy Points: 280
  Hujui usemalo, wimbo wa taifa hutumiwa na yeyote
   
 6. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kwa tafsiri yako hii, wimbo wa taifa ni mali ya matukio makubwa ya taifa, kama kifo tena cha viongozi wakuu, sherehe za uhuuru, hotuba ya raisi. Naamini tafsiri hii umeipata kutokana na mazoea tu. Huu umekuwa ni utamaduni. Nikupe mfano: Kuna mama mmoja, kila mwaka wakati wa sikukuu ya Krismasi alikuwa hupika nyama ya kuku kwenye sufuria mbili.

  Mtoto wake wa kike alizaliwa na akakua akimwona mama yake akifanya hivyo. Na yeye alioolewa alitafuta sufuria za ukubwa ule ule kwa ajili ya kupikia nyama wakati wa Krismas. Siku moja mama yake alimtembelea wakati wa sikukuu ya Krismas. Baada ya kumwona mtoto wake akihangaika kuwasha majiko mawili kwa ajili ya kupika nyama ya kuku, alimuuliza kwa nini unapika nyama kwenye sufuria mbili?

  Yule mtoto alijibu, nilikuona wewe ukifanya hivyo katika maisha yangu yote nikiwa nyumbani. Mama yake akamwambia, "Mwanangu, mimi nilifanya hivyo kwa kuwa sikuwa na sufuria kubwa na uweza wa kununua sufuria kubwa sikuwa nao. Sasa wewe unasufuria kubwa nyingi usihangaike."

  Stori hii inafanana sana na tafsiri yako ya wimbo wa taifa. Wimbo wa taifa si wa raisi,si ishara ya kifo cha kiongozi wa ngazi ya juu. Wimbo wa taifa ni sala ya taifa, ni wa kila mwanataifa la Tanzania. Ndiyo hasa, kitambulisho chetu, ndiyo unaoweza kuonesha umoja wetu, ndiyo unaoshuhudia utu wetu wa kitaifa, na mshikamano wetu.
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mungu akusamehe hujui usemalo
   
 8. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Serikali ni nani? Au hiyo Tz ni ya nani? Tumia akili
   
 9. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 493
  Trophy Points: 180
  ****!!
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hata maana ya serikali unauliza?
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kwamba wimbo wa Taifa ni mali ya watanzania lakini mbona hujasema kwa upande wa vyama vya siasa, je vinaruhusiwa kutumia? Kwa upande wangu ninatambua kuwa wimbo wa taifa ni moja ya alama za kitafa (National symbols) zingine zikiwa ni Nembo (Court of arms) na Bendera (National flag). Kama ambavyo huwezi kuona bendera ya taifa ikipepea katika ofisi za vyama vya siasa hasa ambavyo havijaunda serikali ndiyo inavyotakiwa kuwa hata kwa wimbo wa taifa.
   
 12. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Kumbe wimbo amabao unahimiza umuhimu wa umoja na amani kwa africa na nchi yetu? wewe hushangai mali za serikali kama magari, ofisi,nk zinavotumiwa na mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na wakurugenzi kufanyia kampeni za CCM???mawaziri ambao kisheria ni watumishi wa umma na wanalipwa na serikali kutokana na kodi zetu wameacha ofisi za umma na kwenda kufanya kampeni za CCM Arumeru muda ambao wanatakiwa wawe ofisini wanafanya kazi za umma??Hizi ndizo rasilimali za serikali zinazotumika vibaya!!
   
 13. m

  mzizi dawa Senior Member

  #13
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ongera sana kwakutoa elimu ya bure,atakua amekuelewa yule mweu.
   
 14. v

  vngenge JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45

  Bendera ya taifa mbona matrja wanavaa kichwani, afterall wimbo wa taifa xaxa vyama vya siasa si sehemu ya Taifa?. Well ni mali ya serikali, serikali ni nani sasa kama sio wananchi na Rais ni kiongozi mkuu
   
 15. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Je vyama vya siasa ni vya nani? Je ni vya wamarekani? Kama vyama vya siasa ni vya Watanzania, je havimilikiwi na serikali ya Tanzania? Kwa nini basi vinapewa ruzuku na serikali ya Tanzania? Acha kujichanganya. Kama dhumuni lako ni kutaka kujua kwa nini chadema wanatumia wimbo wa taifa nimeshakupa jibu. Ukiendelea wenyewe wapo, utaona.
   
 16. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mtoa mada umepotelea wapi..? Jibu hoja hizo au kama umekubaliana nao pia useme, halafu swala la matumizi ya fedha za michango kwa matumbo ya viongozi hilo unapaswa kulitolea ufafanuzi ni lini na wapi na kiasi gani kilitumika kwenye matumbo na si kazi za chama kama inavyokusudiwa.
   
 17. BJEVI

  BJEVI JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 1,360
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mtoa mada naomba ukajipange upyaaaaaaaaaaaaaaaaaaa....huna dira wala mwelekeo wa mada yako hiiiiiii ya KIJIMA...

  KWAHERI
   
 18. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  mimi kila nikiaamka lazma niimbe mwimbo wa taifa langu kama wewe unauogopa inaonekana wewe sio mtz
   
 19. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Hili la kutumia wimbo wa Taifa kwenye vyama vya siasa naona kuna haja ya kuliangalia..
   
 20. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuacheni ushabiki wa kisiasa; kwa kuzingatia elimu tulonazo matumizi ya wimbo wa Taifa sina shaka kila mmoja anayafaham; sidan kama chama binafsi kinaruhusiwa kutumia wimbo wa Taifa kwa sababu zao tofauti si CCM wala CDM labda uwe ni utaratibu mpya na kama ndivyo basi tunakoelekea tutaanza kuutumia hadi kwenye kumbi za starehe na kama haitoshi ataibuka mtu atataka aufanyie remix na kuachia single yake; na mwingine (Njeree) ataibuka na bendera ya taifa ajifunge rubega akate kitaa la hasha tunapotoka"
   
Loading...