Haya si mane no yangu............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya si mane no yangu.............

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kimatire, Mar 25, 2012.

 1. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  " cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa Nchi yetu unataka yasemwe. (Ukurasa 61)

  Mwalimu hakuishia hapo, bali aliongezea namna hii:

  Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona Chama makini cha upinzani; na wala dalili zo zote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasi wasi! (Ukurasa 66)"Yetu Macho tu!
   
 2. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,904
  Likes Received: 2,332
  Trophy Points: 280
  How prophetic Mwalimu was!
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  Leo ndio unasoma maneno haya ya hayati mwl?!anyway,mda wa ccm kutawala umeshakwisha.
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  ccm wanapumlia ICU.
   
 5. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,920
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Kimatire, I salute you, hazina kama hizi ndo tunatamani watu tuzipate. Bless U
   
Loading...