Haya sasa

Valentina

JF-Expert Member
Oct 12, 2013
24,685
28,769
Pale unapozamia kwenye Dinner Party ya Jumuiya Fulani, sasa Lengo la Jumuiya hiyo ni kupata Fedha za kutunisha Mfuko wa Jumuiya...sasa unakakaa mbele kabisa ili Muda wa Msosi usichelewe na kukuta kwenye Buffee yamebaki maharage!

MC : "Papai zuri kabisa kutoka Newala, Papai Mwendokasi, hili ni Shilingi laki 1..jamani Papai,nipeni ofa!"

MOSHA : "Laki 3 hapaaa!"

"Jamani laki 3 pale kwa Mosha, Papai linaondoka jamani, papai hili ni self contained kabisa....papai jamani"

KIBOLIBO: "Milioni 1 hapaaa"

"Jamani Mambo yanazidi kunoga hapa!...Benedict Kibolibo anataka papai kwa milioni 1 jamani, linaondoka papai!"

RWEYEMAMU : "nitanunua Papai hilo kwa Milioni 5"

Haya sasa jamani Rweyemamu ametoa ofa ya Milioni 5 Jamani, nani mweingineee?"

Kimyaaa...

Haya jamani Papai kama hakuna Ofa basi Papai linakwenda kwa Rweyemamu!........haya sasa Kuna Kuku hapa Jogoo kabisa, bei yake ni laki 6 jamani Jogoo twitter huyu!"

WEWE "Milioni Mojaaa!"( hapa umejiwahi wa kwanza na wewe uonekane upo huku ukijua kabisa Wakina Mosha na Rweyemamu lazima watampandia Dau Jogoo, tena dau kubwa"

MC: ee sasa Kumekucha Jamani, Kabasele anamtaka Jogoo kwa Milioni 1 jamani!....ofa nyingineeee!"

Kimyaaa...

Jamani Jogoo anakwenda kwa Kabasele jamani!...ofa nyinginee!

Kimyaaa....

Kimyaaa....

....hapa sasa ndio mfukoni kuna Buku jero,..huko kwengineko NMB nill balance...sasa unageuza mimacho kumtazama Mosha kama atapanda dau kwa jogoo(mama wee Mosha anachezea Simu!).....unamtazama Rweyemamu (teh anatafuna Kuku).....mama weee

MC: Haya jamani kama hakuna Mwingine basi zoezi letu liishie hapa na limekwenda kwa Mafanikio, Mpatieni Kabasele Jogoo wake!

Hapa sasa unapokea jogoo wako wa MILIONI kwa Tabasamu la Maiti....kule nyumbani Jogoo wako Mkubwa unauza elfu 20 lakini sasa haka kajogoo kapya Mkononi kanakuwa kazito utadhani umembeba John Cena...Mama weee hapa sasa vidari ulivyotafuna unaviona kama vimerudi kwenye Ulimi....Chicken wings zinataka kutokea Masikioni.....Uuuuwiiiii,

Na hapa sasa kabla Dinner haijaisha ndipo unapojikuta Umebuni Cocktail ya Sparetta na Tomato
 
Ha ha ha ha
aiseee hapo naweza kusingizia nina tumbo la kuhara, naondoka kama naelekea chooni.

Nikifika mbele nakunja kona hawataniona tena
 
Ha ha ha ha
aiseee hapo naweza kusingizia nina tumbo la kuhara, naondoka kama naelekea chooni.

Nikifika mbele nakunja kona hawataniona tena

Hiyo nitawaachia wenyewe wajadili, shali yao. tena ninavyojua kuyumba watanionea huruma
Kwakweli mbinu ya haraka hapo muhimu kabla mtu mzima hujaumbuka
 
Hapo ni kuendelea kupanda dau mwenyewe mwenyewe inakuwa kamchezo flan hv endless watachoka tu wenyewe
 
Nimeshuhudia hii kanisani, maumini mmoja alidhani ni mchezo, kila kitu lazima alianzishe tena bei kubwa kuliko kawaida, aki bet wa pili yeye kimya ka hayupo kanisani. Likaletwwa jogoo jekunduu linameremeta kataja 80,000, hakuna mtu analiendeleza, kabaki anatambua macho mwendesha mnada ikabidi aanze upya.
 
Nimeshuhudia hii kanisani, maumini mmoja alidhani ni mchezo, kila kitu lazima alianzishe tena bei kubwa kuliko kawaida, aki bet wa pili yeye kimya ka hayupo kanisani. Likaletwwa jogoo jekunduu linameremeta kataja 80,000, hakuna mtu analiendeleza, kabaki anatambua macho mwendesha mnada ikabidi aanze upya.
Ha haa afu hao ambao wanazingua ndo wanakuaga viherehere kweli kupandisha dau
 
Back
Top Bottom