Haya ni mambo 8 ambayo huwezi kufundishwa shuleni

Showio

JF-Expert Member
May 16, 2019
255
481
Haya ni mambo 8 ambayo huwezi kufundishwa shuleni:

1. Maisha hayako fair. Yazoee. Unaweza kufanya kazi sana ila ukakosea kidogo tu usifanikiwe lakini mwingine ukaona hafanyi sana ila anafanikiwa. Usinung'unike, hayo ndiyo maisha.
2. Hutakaa upate kazi ya mshahara wa kukutosheleza mara tu baada ya kuhitimu elimu yako. Anza na kilichopo.
3. Kama unadhani walimu au malekchara hawako fair, subiri ukutane na maboss kwenye kazi halafu tafakari upya.
4. Ukikosea wewe usilaumu wengine. Sijui wazazi, sijui ndugu, sijui waalimu. Ni maisha yako. Jisimamie. Pambana.
5. Watu unaokutana nao wanajua vitu ambavyo wewe hujui. Heshimu watu. Jifunze. Kaa na watu uvae viatu. Usijione graduate ukakute mzee wa darasa la nne mlinzi getini ukaanza dharau. Utapotea.
6. Shuleni unaweza kuwa wa mwisho lakini maisha hayaamuliwi hivyo peke yake. Bado una nafasi.
7. Maisha hayajagawanywa kwa mihula (semesters). Jipangie mihula ya maisha mwenyewe, kuwa na sheria na mipango ya maisha yako na itekeleze. Hakuna atakayekupangia wala kukuhimiza kufanikiwa.
8. Unayoyaona kwenye TV ni maigizo, sio maisha halisi. Hata habari wakati mwingine huwa ni za kupikwa, sio uhalisia. Amka! Kwenye maisha ya kawaida watu wanafanya kazi na sio mapenzi muda wote kama tamthilia za Kimexico au Kifilipino
 
Hiyo namba 4 ukiiwezea itapunguza sana stress zako
 
Hiyo #6 kwa sisi tuliokimbia ku-download ma-file kwenye majengo ya serikali tukaingia mtaani umetufariji kweli mkuu.

Otherwise,bandiko ni zuri vijana mkipita hapa okoteni mawili matatu yatawaongezea mwanga huko mbeleni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom