Haya Ndo Mapenzi

Filipo Lubua

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2011
Posts
339
Reaction score
578
Nyingine si ndoa, ni ndoano
Mengine si mapenzi, ni ushenzi
Pengine, ni wizi, ubezi, ubazazi
Yakache, ya siku chache yasikuchache

Mwingine si upendo, ni utando
Mengine si asali, ni ajali
Ni utweza, poteza, lemeza
Tulia, pana nia pana njia

Mengine si furaha, ni karaha
Mengine si utamu, ni udamu
Ni fweza, uweza, uoza
Jikubali, usikubali kukubali

Sidhani yatuliza, yanaliza
Sidhani ni mapendo, ni uvundo
Si uhondo, ni ugando, kimondo
Usilie, yakimbie ujitue

© Filipo Lubua
23 Feb. 2013
 
mujini musingi kiuno ,
ya msondo muachie ngurumo,
endelea hapo ni mavoko huyo mtafute mfanye kazi
 
Anatangaza single yake wajamenu
 
Shule imekuwa ngumu hadi umeamua kutirirka na mistari! UE imekaba au fm 6 mock inakumbamba? Maana hapo ndiyo huwa chujio linatenganisha pure na impurity

 
Shule imekuwa ngumu hadi umeamua kutirirka na mistari! UE imekaba au fm 6 mock inakumbamba? Maana hapo ndiyo huwa chujio linatenganisha pure na impurity
Nduguye, yote uliyoyataja nilishayamaliza zamani sana. Kama wewe ndo bado uko huko pole sana na kazana. Mie niko ngazi nyingine za juu zaidi, na uandishi wa mashairi ndo fani yangu.
 
nasubiria huo ubeti unaoongelea hasa, 'haya ndo mapenzi'.

Mentor naungojea kwa hamu mana nmeyatafuta muda mrefu.


ni mimi wenu PM Moderator,
Mentor.
 
Last edited by a moderator:

siku nyingine ukipesti vitu kama hivi, uwe unapeleka kwanza kwenye microsoft word, una edit, unafanya analysis.. then ndo unaleta hapa!

umechangia sana katika kuumiza macho yangu leo!
 
Wamarekani kwao maisha ni chochote muziki unaweza ukamfanya akaacha shule haya waige tu baadaye ukikumbuka muda hautakuwa rafiki tena.

Nduguye, yote uliyoyataja nilishayamaliza zamani sana. Kama wewe ndo bado uko huko pole sana na kazana. Mie niko ngazi nyingine za juu zaidi, na uandishi wa mashairi ndo fani yangu.
 
Kamua! wewe ni Fulbrighter wa kwelikweli hata usingeweka email hapo chini. By the way, wa mwaka gani na uko wapi? Embu ni PM.



 
Yote tisa kumi ngono tu, utafanya kila kitu kama kunako 6×6 uko under perfomance Hakuna mapenzi hapo

Ukilipata bumunda lifanyie kweli, litifue kwelikweli mpaka liwe jekunduuu, utapendwa hadi kero
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…