Haya ndiyo maisha ya tembo

Haya ndiyo maisha ya tembo

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,852
tembo.jpg

TEMBO NI NANI ?
kwa wanaomfahamu au kutokumfahamu,tembo ni mnyama mkubwa kuliko wote duniani aishie nchi kavu.
Bila ya kusahau kuwa nyangumi ndie mnyama mkubwa kuliko wote hali ya kuwa wao wanaishi baharini.

AINA ZA TEMBO (species).
duniani tuna aina kuu mbili za tembo.
>african elephant.
>asian elephant.
Tembo wa asia (ASIAN ELEPHANT) tembo anaeweza kufugika,ni tembo mwenye ukaribu kabisa na binadamu na zamani alitumika pia katika masuala ya vita.

Huyu ni tembo mwenye pembe (tusk)nyepesi zaidi kuliko ya tembo wa afrika.
Tembo wa afrika na mkubwa zaidi na mkali kuliko wa asia.
Kawaida tembo wa afrika wanatabia ya kulipiza visasi (VIGAROUS ATTACK) hivyo kuwa katika mnyama wa kundi la BIG FIVE.

PEMBE ZAKE (TUSK).
pembe zake humsaidi katika mambo mengi kama wakati wa kupigana pia wakati wa kuchimba chini kutafuta maji au chumvi.
Pembe hizo ndio chanzo cha majangili wengi kuwaua.
Pembe hizo pia hutumika katika kubandualia magome ya miti hata kuangusha miti pia.

MKONGA WAKE (TRUNK).
Kwanza kwa kifupi,NI PUA NDEFU ILOYOREFUKA mdomo wa tembo upo chini ya mkonga huo.
Mkonga hutumika katika kukatia nyasi wakati akila na kufutia maji wakati wa kunywa.
Kwa kuwa mkonga ni pua ndefu,wakati wakipata tiba madaktari wanapaswa kuwa makini ili tembe asije kulali mkonga wake na hivyo huweza kusababisha kifo kwa kukosa hewa.

Kundi la tembo huongozwa na tembo jike aitwae MATRIARCHY.
Mkonga hutumika pia katika mawasiliano yao kama wanyama.

MIMBA.
Tembo ni mnyama mwenye kubeba mimba kwa muda mrefu zaidi.
Hubeba mimba kwa miezi 18 hadi 22 sawa na miaka miaka miwili.

UJANGILI.
=tembo hufanyiwa ujangili sana huku ujangili mkuu ukiwa ni wa kusaka pembe zake.
Jumuia za kimataifa na taifa kiujumla zinapaswa kusimama ili kulinda maisha ya wanyama hawa na vizazi vyao.
Ujangili wa tembo ni hasara kwa taifa.

JE UNAMFAHAMU TARZAN WA KWENYE FILM ?
Wengi wanamjua mtu huyu kwa kumuona katika filam yake,lakini huwezi amini yupo mtu katika nchi hii anaeshika tembo akiwa mzima kabisa na kucheza nae.

Ngumu kuamini lakini usijaribu kwani tembo ni hatari kama utamletea mzaha.
Tuwalinde tembo wetu ili watunufaishe.
 
Asante' hapo kwa Tarzan wa Tz hebu dadavua vizuri.
 
Mi nasubiria ulete simulizi ya Chatu na Mamba ingawa napenda kufahamu historia za wanyama vile vile.
 
JJ10 usiogope ipo siku atajulikana ingawa wachache wanamfahamu,ondoka shaka kwa hilo.
MASTER PLAN,pamoja sana,tutaendelea kuhabarishana kuhusu mamba na chatu.
 
Ngumu kuamini lakini usijaribu kwani tembo ni hatari kama utamletea mzaha.
Tuwalinde tembo wetu ili watunufaishe.

ujumbe huu uwafikie majangili wote waliopo ndani na nje ya nchi...
 
duh hapo kwenye mimba pamenishangaza miaka miwili duh?????
 
Mkuu asante ungemalizia pia kwa kusema Tembo ana uwezo wa kunusa maji kwa umbali wa kati ya kilometa 15 mpaka 20.
Pia Tembo ana kumbukumbu ya adaui (poacher) kwa miaka mingi. Ni wanyama wanaowasilia kwa umbali mrefu sana kati ya kilometa 4 na huongezeka mpaka kufikia 20.
 
Kama kuuliza si ujinga ngoja leo niulize,Hivi nn kazi kubwa ya pembe za ndovu?

Pembe za ndovu zinatumika duniani kote. Soko kubwa lipo East Asian countries hasa China. Wachina hutumia kutengeneza carvings, pipes, images of deities, daggers, chopsticks, jewelry, ornaments, souvenirs and hair accessories. Some Asian nations also highly value elephant tusks for their apparent medicinal properties. Even though science has verified the lack of medicinal properties in ivory, there is still a high demand.

Nimekumegea kidogo mkuu. Need more?
 
pembe za ndovu meno ya tembo

inanipa sheeda sana sijui ni kiswahili au uelewa wangu
 
Nashukuru sana mdau kwa uzi huu. Mimi kwa ujumla ndo fani yangu niliyosomea i.e Utalii, so wakiisha no job. dah walaaniwe majangiri wote wa rasilimali zetu za nchi hii, baba wa taifa alituachia.
 
Huyu tarzan wa tanzania kama namjua vileee!!?? Naskia ukikatiza mikumi ukitaja tu jina lake tembo wanatoka nduki balaaa!
 
Muhudumu, hebu leta KINANA baridi!!
 
Back
Top Bottom