Haya ndio yaliyo wasibu wana wa Arusha

mwobho

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
808
352
Arusha. Wabunge wanne wa
Chadema, Said Arfi (Mpanda Mjini),
Tundu Lissu (Singida Mashariki),
Mustapha Akunaay (Mbulu) na
Joyce Mukya (Viti Maalumu)
wamekamatwa wakituhumiwa
kuhusika na mkusanyiko usio halali
kwenye Uwanja wa Soweto jana.
Mkuu wa Operesheni wa Polisi,
Kamishna Paul Chagonja alisema
jana kwamba pamoja na wabunge
hao pia wamewakamata watu
wapatao 60 kutokana na vurugu
zilizozuka jana baada ya Polisi
kuwatawanya kwenye uwanja huo
waliokuwa wamekusanyika
kuomboleza vifo vya watu watatu;
Judith Moshi, Ramadhan Juma na
Amir Ally waliofariki kwenye
mlipuko wa bomu uliotokea kwenye
uwanja huohuo, Jumamosi iliyopita.
Mbali ya viongozi hao, alisema
wanawasaka Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe na
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema.
“Tunawasaka wabunge ili
tuwajumuishe na watu hawa kwa
kosa la kuhusika na mkusanyiko
usiokuwa halali. Hadi sasa
tumefanikiwa kulinasa gari la
Mbowe,” alisema Chagonja.
Pia kamatakamata hiyo imemkumba
Mpigapicha wa Kituo cha
Televisheni cha Channel Ten, Ashraf
Bakari. Polisi walilazimika kutumia
nguvu kuwatawanya waombolezaji
hao.
Awali, Kamishna Chagonja alisema
jana asubuhi kuwa wamelazimika
kuzuia viwanja hivyo kutumika
baada ya wamiliki wake, AICC
kuzuia shughuli za Chadema
kwenye eneo lao.
Kamishna Chagonja aliwaonyesha
waandishi wa habari barua
aliyosema imeandikwa na uongozi
wa AICC kuzua Chadema kuendelea
kuutumia Uwanja wa Soweto.
Mabomu yarindima
Dalili za kuzuka kwa vurugu
zilianza kuonekana asubuhi baada
ya polisi kuzingira uwanja huo na
kuzuia watu waliokuwa wameanza
kufurika katika eneo hilo kuanzia
saa moja kuingia kwa ajili ya
maombolezo.
Wakati Polisi wakiwa uwanjani,
wananchi walijaa nje ya uwanja na
kuonekana kama wamewazingira.
Viongozi wa Chadema wakiongozwa
na Mbowe waliwasili uwanja hapo
yapata saa nane mchana na kukuta
zuio hilo na kuanza kuzungumza na
wananchi ingawa FFU walikuwa
wakiwataka watu kutawanyika.
Mabomu yalianza kurindima wakati
Arfi aliposimama na kuwahimiza
wananchi kuelekea Hospitali ya
Mount Meru kwa ajili ya kuaga miili
ya marehemu.
“Tuna muda mfupi sana wa
kuzungumza hapa, tunaomba wote
tuelekee Hospitali ya Mount Meru
kuaga miili ya marehemu kwa
sababu uwanja huu umezuiwa na
polisi,” alisema Arfi kabla ya
kukatishwa na milipuko ya
mabomu.
source:gazeti la mwananchi.
 
Wee habari hii imewekwa tangu asubuhi hapa, na wewe unakurupuka usiku huu, kukamua band-with tu..
 
Back
Top Bottom