Haya ndio matokeo yangu kidato cha VI&DIPLOMA.

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
8,817
17,612
Amani iwe kwenu wapendwa,

nilikuwa na malengo ya kuanza masomo yangu ya elimu ya chuo kikuu mwaka huu lakini kutokana na matokeo yangu na kuongezwa kwa alama za kujiunga na chuo kikuu nimekosa cha kufanya wapendwa naomba mnipanue mawazo kwa hili

Kidato cha sita nina daraja la tatu pointi 14 yaani nina DEE Masomo ya sanaa na wakati huo chuo kikuu wanataka D mbili

Diploma yangu ya sheria nina GPA ya 2.9 ambapo ili ujiunge na chuo wanataka GPA Ya 3, ikumbukwe kuwa waziri wa katiba na sheria ametupa muda wa miaka mitano mahakimu wote wenye diploma tuwe tumejiendeleza,je nifanyeje wapendwa, naona kama kazi yangu inaenda kunikimbia
 
Duuh sasa mnatupa Kazi ngumu nyie jamaa
Hizo GPA tunajua sio ishara ya uelewa ila linapokuja suala la kitaaluma aisee ulitakiwa kutusua hata 3.8 tu sasa ona unataka tushiriki kukushauri kitu ambacho hakiwezekani

Labda nenda urudie paper la six upate principal pass moja wanayotaka ili ziwe D mbili

Ila six msuli wake sina hamu nao kabisa
 
Duuh sasa mnatupa Kazi ngumu nyie jamaa
Hizo GPA tunajua sio ishara ya uelewa ila linapokuja suala la kitaaluma aisee ulitakiwa kutusua hata 3.8 tu sasa ona unataka tushiriki kukushauri kitu ambacho hakiwezekani
Hapana Mkuu usichoke kutenda wema ,ushaur wako kwangu ni muhimu ndugu
 
Labda kurudia paper la six au uende chuo cha nje mkuu sasa hata ukienda kusoma nje ukija bongo TCU watakwambia degree yako sio valid maana hukua na sifa, kumbuka wale wanaokimbilia Uganda ilihali Form four wamefeli, wakitoka huko na One zao za form six wanakataliwa hapa Tz maana hawakua na sifa za kusoma advance
 
Vipi nikisema nirudie somo moja hapo kutafuta D moja naweza sajiriwa chuo kikuu?
 
Kwa miaka 5 bado unaweza kusoma diploma na degree (2+3),credit zako zinaruhusu kusoma diploma tafuta chuo apply diploma tofauti na hiyo uliyonayo.

Ukirudi shule soma kwa bidii na ufanye discussion na wenzako utafaulu na kupata degree yako
 
Mkuu ngoja nikuweke sawa,mitayari nina diploma ya sheria ya GPA Ya 2.9 na kidato cha sita nina dvn 3 ya 14 hivo naomba namna ya kwenda chuo kikuu ndugu
 
Nafahamu ndio maana nimekwambia soma diploma nyingine tofauti na uliyo nayo jitahidi upate GPA itakayokuwezesha kufanya degree
 
Asante sana Mkuu, vipi nikisema kurudia mtihani wa kidato cha sita?
 
Back
Top Bottom