mahirtwahir
JF-Expert Member
- Jan 12, 2013
- 614
- 322
Historia ya kweli
Kijana mmoja anaitwa J miaka yake 18 ilitokea kumpenda mtoto wa miaka 17 ambaye ni mtoto wa mama ake mdogo (mamdogo) waliishi kimya kimya ila hazira na wazazi wao hawakujua kua kuna mahusiano kwani ni familia ilionekana kama kawaida.
Kwa vile baba ake msichana alikua na pesa na mwanawe alifeli form 2 aliamua kumpeleka shule ya bodingi Dar baada ya miezi 3 mtoto alibainika kua ni mja mzito kwa hio alirudishwa kwao baba wa mtoto wa kike akafungua kesi na kusema atahakikisha kua yule kijana anafungwa.
Suluhu za kifamilia na majirani hadi viongozi wenzake wa baba wa mtoto wa kike aliombwa suala hili kulimaliza kifamilia ambako ni kuwaozesha wawili hao ila baba huyo alikataa kwa nguvu zote.
Baada ya kesi kuanza kwa muda wa miezi 2 kijana J alikua akipanda kizimbani na kurudi rumande hadi familia ilipopata ruhusa ya kumchukulia zamana ambapo mzamana wa kwanza alikua mama ake.
Baada ya zamana ikafika wakati wa hukumu siku ya kuamuliwa hukumu kijana akakimbia hakupenda mahakamani mama yake akapanda kizimbani na kupelekwa rumande yeye ili amlete mwanawe ilipishindikana jaji aliamua kumhukumu kijana huyo kifungo cha miaka 7 akipatikana na mama ake aliachiliwa huru baada ya kuvua zamana hio.
Baada ya kujifungua mtoto wa kike kalenda tena Dar kusoma kapelekwa shule nyengine bodingi bila ya kujua mawasiliano yametoka wapi wakawa wanawasiliana na kijana huyo aliyempa mimba akamtorosha tena shule kwa muda wa siku 3 na shule ikabidi kutoa taarifa kwa wazazi wa msichana huyo.
Familia ya msichana wakaanza kumsaka kwa juhudi hatimaye wamemuona akiwa na kijana huyo wakamchukua na kumpeleka polisi kutoa maelezo kua kakimbia mahakama na kumfungulia jalada jengine la kutorosha
Kijana akasafirishwa kutoka Dar hadi kwao Pemba na kupandishwa kizimbani kusomewa tena mashtaka mawili la kukimbia mahakama na la kutorosha mtoto alie chini ya uangalizi kijana akahukumiwa kifungo bila kuchelewa na kwa sasa 7/2/2019 hata week hajamaliza toka aanze kutumikia
Binafsi naona ni ujinga pili ni kua watoto hawana huruma na wazee wao tatu nahisi ulezi jamani ni mgumu Mungu akikupa mtihani akikunyima mtihani
Kiupande wako unasemaje?