Haya ndio mambo ninayoyaona huku Ughaibuni

ESCORT 1

JF-Expert Member
Dec 7, 2015
1,267
2,519
Wakuu naendelea na ziara ya kuzuru maeneo mbalimbali ya Dunia, na sasa nipo nchini Bolivia.
Wenyeji wa hapa ni wakarimu sana. Ila kwenye pitapita nikasikia sakata linaloendelea la gavana wa jimbo la La Paz.
Gavana huyu anakaribia kuondolewa katika wadhifa wake huo, kutokana na kashfa mbalimbali zinazomkabili toka kipindi cha miaka ya nyuma.

Ila cha kufurahisha ni mbinu inayotumika kumuondoa Gavana huyo wa jiji la La Paz.Wenyeji wananiambia kuwa mbinu hizo zinafanana sana na mbinu zilizowahi kutumiwa na Kiongozi wa Bolivia kumuondoa Waziri mlevi.

Gavana ataondolewa katika wadhifa huo ni baada ya kuondolewa kwa Naibu Sheriff ambaye alikuwa anamsapoti sana Gavana.

Wenyeji " wananiuma sikio " kuwa, Kiongozi ameamua kumuondoa gavana kwa mbinu ya " pwani ya bahari " na makasha.

Basi nikaona niwa " tonye " na nyinyi wa huko nyumbani Tanzania. Bado naendelea kukata mitaa huku, kesho nina safari ya kwenda mjini Forte, nikajionee vivutio vya asili vinavyopatikana huko.

Nisalimieni sana huko Nyumbani!!
 
karibu nyumbani tena sa hivi tuna viwanda zaidi ya 3500+ ndani ya miaka 3 ya magufuli nahisi hao bolivia tumisha wapita mwezi ujao tutaanza kuwauzia bidhaa kutoka TZ
 
Wenyeji " wananiuma sikio " kuwa, Kiongozi ameamua kumuondoa gavana kwa mbinu ya " pwani ya bahari " na makasha.
Kwani wenyeji hawajakujulisha hayo makasha yalikuwa yamejaza nini? Ila hiyo mbinu mbona ya kishamba sana!!
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom