Haya ndio maisha halisi ya wengi

bongo dili

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
12,371
24,600
MDOGO WAKO:Kaka naomba 600,000/= Kwa ajiri ya ada . Walisema nisipolipa hawatanipokea kabisa.

BABA MWENYE NYUMBA:Missed Calls 83 na Ujumbe: Leo nakupatia Nafasi ya Mwisho

BINTI WA JIRANI: Nafikiri Nina Ujauzito wako.

RAFIKI YAKO: Kaka ,fedha yangu lini unanipa? Ni mwisho wa mwezi Sasa ulioniahidi mara ya Mwisho.

WAZAZI: Tunakufa Kwa Njaa kijana wetu.

Hatuna chochote , Tusaidie .

MCHUMBA: Sawa tu,naona umeanza kunionyesha dharau kabla hata hatujaoana. Endelea tu na Hao Malaya wako. Usinitafute mimi. Pepo wewe!

EX: Ulinitumia tu Mbwa wewe. Utakufa Kifo kibaya sana.

M PESA:Unakumbushwa kulipa Mkopo wako wa SONGESHA kiasi Cha Tsh. 93,200/=

TALA: Tunajua unapoishi , Wewe ni Mdaiwa sugu Sasa na tutakukamata tu.

MSHAHARA :Kiasi Cha Tsh. 187,000 kimewekwa kwenye akaunti Yako inayoishia 3214.
 
MDOGO WAKO:Kaka naomba 600,000/= Kwa ajiri ya ada . Walisema nisipolipa hawatanipokea kabisa .

BABA MWENYE NYUMBA:Missed Calls 83 na Ujumbe: Leo nakupatia Nafasi ya Mwisho

BINTI WA JIRANI: Nafikiri Nina Ujauzito wako .

RAFIKI YAKO: Kaka ,fedha yangu lini unanipa? Ni mwisho wa mwezi Sasa ulioniahidi mara ya Mwisho.

WAZAZI: Tunakufa Kwa Njaa kijana wetu .
Hatuna chochote , Tusaidie .

MCHUMBA: Sawa tu,naona umeanza kunionyesha dharau kabla hata hatujaoana. Endelea tu na Hao Malaya wako. Usinitafute mimi. Pepo wewe!

EX: Ulinitumia tu ,Mbwa wewe. Utakufa Kifo kibaya sana.

M PESA:Unakumbushwa kulipa Mkopo wako wa SONGESHA kiasi Cha Tsh. 93,200/=

TALA: Tunajua unapoishi , Wewe ni Mdaiwa sugu Sasa na tutakukamata tu.

MSHAHARA :Kiasi Cha Tsh. 187,000 kimewekwa kwenye akaunti Yako inayoishia 3214.
Maisha ya vijana wengi below 35
 
Kupanga ni kuchagua.

Wakati mwingine kubali lawama mpaka pale utakaposimama vizuri. Dhamira yako ikiwa safi mengine yote ni madogo na usijali lawama, kuchekwa wala kusemwa na watu. Na umakinikie mambo ya muhimu tu kipindi hiki (hayo ya wachumba, wapenzi na ma ex hayana nafasi kipindi hiki)

Tuliotoka familia za kawaida wengi wetu tumekipitia kipindi hiki. Hatimaye kitapita na siku moja Ma mkubwa anakupigia anahitaji 50K unatabasamu tu huyo unamrushia 200K. Mibaraka kama yote unaihisi mpaka kwenye simu....

Kutokata tamaa, kujikubali, kutojilinganisha na wengine, kuwa karibu na Mungu (kwa waaminio) na kuacha shobo zisizo na maana ni baadhi ya mambo ya muhimu sana kuzingatia katika kipindi hiki.
 
Bongo unatuma message ya kupiga mizinga usogezee siku baada ya kutuma tu nawe unapokea message ya kupigwa mzinga
 
Kupanga ni kuchagua.

Wakati mwingine kubali lawama mpaka pale utakaposimama vizuri. Dhamira yako ikiwa safi mengine yote ni madogo na usijali lawama, kuchekwa wala kusemwa na watu. Na umakinikie mambo ya muhimu tu kipindi hiki (hayo ya wachumba na ma ex hayana nafasi kipindi hiki)

Vinginevyo utachanganyikiwa!
Hii inatosha kuufunga huu mjadala
 
Dogo unataka na wazazi nao wanataka,Swali hawa wazazi mbona wanazaa watoto baadae wanawacha na kujifanya wamemaliza majukumu yao?

Hizi familia zilizo separated ni mtihani mama atumiwe na baba bado kuna madogo uwasomeshe, wakati huo wazazi wanajifanya kama Wamejitoa katika kusomesha watoto wao ,wewe ndo upambanie mwanzo mwisho.
 
Kupanga ni kuchagua.

Wakati mwingine kubali lawama mpaka pale utakaposimama vizuri. Dhamira yako ikiwa safi mengine yote ni madogo na usijali lawama, kuchekwa wala kusemwa na watu. Na umakinikie mambo ya muhimu tu kipindi hiki (hayo ya wachumba, wapenzi na ma ex hayana nafasi kipindi hiki)

Tuliotoka familia za kawaida wengi wetu tumekipitia kipindi hiki. Hatimaye kitapita na siku moja Ma mkubwa anakupigia anahitaji 50K unatabasamu tu huyo unamrushia 200K. Mibaraka kama yote unaihisi mpaka kwenye simu....

Kutokata tamaa, kujikubali, kutojilinganisha na wengine, kuwa karibu na Mungu (kwa waaminio) na kuacha shobo zisizo na maana ni baadhi ya mambo ya muhimu sana kuzingatia katika kipindi hiki.
Ahsante Sana Mkuu kwa Mwongozo mzuri barikiwa
 
Back
Top Bottom