Matege
JF-Expert Member
- Dec 7, 2013
- 1,476
- 648
Naishi mkoa fulani hapa Tanganyika. Sehemu ninapofanyia kibarua kuna binti niko nae ofisi moja.. Ni mtu wa karibu kiasi cha kushea mawazo mara nyingi. Mwenzangu huyu aliolewa na kufanikiwa kupata mtoto mmoja na jamaa ambaye tuko nae pia kazini miaka miwili iliyopita.
Mwaka juzi mwishoni bibie alienda kwao kwa ajili ya kujifungua. Alipomaliza likizo ya uzazi alikuja na kumkuta mwanamke mwenzie ndani anapika na kupakua na mumewe. Waliyaongea yakaisha na wakaendelea kuishi ingawa maelewano hayakua mazuri sana.
Waliendelea kuishi ila hawakukaa sana mwanaume akahama nyumbani na kwenda kupanga. akiwa kule aliendelea kuishi na mwanamke aliekuwa nae baada ya mkewe kwenda kwao kula uzazi. Mwaka huu mwezi June mwanaume alifunga ndoa na yule mchepuko na kuanza kuishi nae rasmi kama mke wa ndoa.
Baada ya ndoa bibie aliumia sanaaa. alikua anatia huruma mpaka time zingine hakuwa anaweza kuja kazini. alikonda akabaki kama miss kwani mwanaume alikua hatoi huduma zozote kwa mtoto wake. alizoea na hatimae maisha yakaendelea.
Hivi leo jamaa amerudi kwa mdada na kuja kulia shida kuwa hana hela, anadaiwa kodi ya nyumba hivyo mdada amkppeshe na atamrudishia mwisho wa.mwezi mshahara ukitoka. bibie bila hiyana akampa.. alikuja kunipa taarifa tu nami sikuongeza neno maana kama.ni.kuongea nishamaliza maneno yoote. hivi sasa ndo amerudisha majeshi kwa jamaa. Mi siwezi kumshauri tena ila amenikera mnoo.. pamoja na kudhalilishwa kote huko lakini bado kalamba matapishi.. aisee mapenzi ya hivi hata shetani anayaogopa