Haya magroup ya shule mmlishamaliza shule miaka yapata 12. mnachangishana Hivi mimi ndiye nawaza negative?

Jamii yetu iko judgemental sana hususan kwenye baadhi ya mambo kama haya ya michango.

Mtu kama mimi napenda kusaidia watu wanapohitaji msaada lakini napenda kufanya hivyo kimya kimya bila kujulikana.

Ukilazimisha niweke jina, nasepa.

Si ajabu wapo watu wengine kama mimi ambao labda wangependa kuwa wachangiaji lakini hawachangii kutokana na kutokuweza kubakia anonymous.
Halafu wabongo wengi wana herd mentality ukichanganya na kuwa inconsiderate, watakushangaa tu wewe vipi? Sasa kwa nini hutaki kuonekana jina, kwani unaiba hapa?

Wengi wao usipo fit kwenye mifumo yao na thinking zao wanakuona ni tatizo, ni mtata, hawana hata consideration kwamba huyu ana concerns ambazo hatuzielewi, labda jambo tunaloliona dogo yeye linaweza kuwa kubwa kwake.

Yani unaweza kuwa vegetarian ukalazimishwa kula nyama tu, ukaambiwa "wee viiipi, huli nyama?"
 
🤣.

I’m not sure if I’m weird, selfish, different, or a little bit of everything, ila mimi sipo kwenye group hata moja!
And that's how it should be.

Whoever is supposed to be in touch with you, will always have a way to reach you without the groups.

Magroup ni mwanzo wa majungu na kuchunguzana tu.

Chochote kinachotolewa kwa jina la msaada pakiwa na matangazo basi dhana yote ya msaada hupotea. Desturi ya msaada ni ibaki baina yako na anaesaidiwa.

Kupitia kuweka mambo halaiki, kunapelekea hata walio na dhamira ya kuchangia kusita ama kutochangia kwa hofu ya kuonekana duni ikitokea wengine wakatoa zaidi.
Baada ya yote binadamu tumeumbwa na unafiki wa kulinganisha kwa kuangalia nani katoa zaidi na wa zaidi kuonekana bora.

Ikiwa mtu anapaswa kuchangiwa harusi/shughuli/msiba wake nina amini naweza mfikia muhusika directly na anonymously. Hapo mchango wangu utakuwa na impact zaidi kuliko matangazo ya ma group.
 
Hata kama si fraud.

Mimi labda naamini sana watu kwenye misiba, sasa fraud inakujaje?.

Mtu anamuua mzazi ili mumchangie? Watu wanaenda kumkabidhi mfiwa rambirambi kwenye msiba, ina maana mfiwa ana fake msiba ili apewe rambirambi au fraud inakuwaje hapo?

Kwangu suala la fraud silioni sana.

Ila, hata kama si fraud, tujitengenezee utamaduni mwingine wa kujiwekea akiba na kujitosheleza wenyewe bila kuchangishanachangishana kila inapotokea msiba.

Kuna watu wengine sio big deal, kuna watu wengine mnawaumiza kwa michango ya kila mara. Hata ikiwa michango ni ya hiyari, kwenye macho ya wengi watu wanaona haya.

Pia, mimi nina allergy na vimichangomichango ya kila mara, inabidi watu wawe na fund ya kutoa pesa haraka hata kama inahitajika kwa dharula. Sasa hivi vimichango mpaka watu watafutane, wafukuzane, wahimizane, tarehe zikiwa mbaya mpaka wasubiri mwisho wa mwezi, karaha tupu.

Afadhali hata kuchanga kwenye mfuko kwa mwaka mzima. Halafu misiba ikitokea mna fixed amount mnaweza kutoa kwa kila member.

Mfuko kama huu utaondoa matatizo kama ya mtu kuchangia wengine na kutochangia wengine, jambo ambalo mara nyingine linaleta mgawanyiko.

Hivi kwa nini watu kama wa bima wasichangamkie watu kukata bima ya maisha? Kuna bima mpaka za vikundi, hivi vikundi vya shule havijui hii bima? Au hizi bima zina matatizo ambayo mimi ndiye siyajui?

Au ndiyo utamaduni wetu kuchangishana watu wajione wako pamoja? Maana kuna jamaa yangu mmoja alikataa kuchangiwa harusi, akasema kama kuna mtu anataka kuchangia harusi yake achangie kijiji cha Wamasai wapate maji, kwa ni nzuri tu asiwape watu mzigo wa kuchanga.

Lakini, kikichotokea ni kwamba, kuna watu walimsema kuwa anaringa na anajiona anaweza kumaliza gharama za harusi yake peke yake bila ya kuwapa watu nafasi ya kuchangia.

Wamakonde walisema "Ukichimama.nchale, ukikimbia nchale".

Ukichangisha lawama. Usipochangisha lawama.
Best option kwa sasa ni M-koba. Mnatupiamo humo kila MTU anaona, mnatengeza katiba ya kipi kinakuwa covered na Kipi kinapotezewa. Thenlikitokea Jambo pesa itatolewa kila.mtu anaona, so inaepusha kuweka mikeka kila Jambo likitokea. Noma Zipo sema wengi hakuna trust nazo kutokana na milolongo Yao hasa pale Jambo linapotokea.
 
Inategemea na mahusiano yenu mlipokuwa shule. Wengine tunazaidi ya 20M kwa ajili ya lolote litakalompata yeyote na familia yake.
Mimi changamoto ya haya makundi ni kwa nini hakuna makundi kwa ajili ya maendeleo? Yani yote ni kwa ajili ya kujihami wakati wa kufa au kufiwa tu.
 
Tuliomaliza shule wakati magroup ya whatsapp hayajaanza tulibadilishana mawasiliano tu..baadae teknolojia ikatukutanisha kwa sura zetu pichani na wengine hawaweki nyuso zao isipokuwa avatar au picha za wanawe nakadhalika. Kazi inakuwa na maswali pale lnapokuwa hamuonani na mnaanzisha group la malengo ya kusaidiana katika shida....

Michango inaanzishwa na mmoja anampoteza mazazi mnachangia kwa masikitiko makubwa japo hamujui ni kwa moyo wa kibinaadam na kuwiwa tu mnachangia 30k kila mmoja wengine hadi 50k

Kuna kitu nakiwaza tofauti japo si kwa nia mbaya kwamba baada ya miaka zaidi ya 10 mnauhakika gani hiyo.michango sio fraud? N muda mrefu na pesa ni mwanaharamu
Tena wengine huandaa na vikao kabisa eti mkeo anakuaga kwenda kwenye kikao cha classmates ambapo wengi wao huishia kuliwa tu huko na vijamaa vyao walivyosoma navyo
 
Ikiwa upo well financial stable
Usiogope kutoa doesn't matter ni Fraud au real.

In this life people is an everything.
Tupo hapa na tutakuwa pale yote hii ni kwa ajili ya nguvu ya watu.
 
Tena wengine huandaa na vikao kabisa eti mkeo anakuaga kwenda kwenye kikao cha classmates ambapo wengi wao huishia kuliwa tu huko na vijamaa vyao walivyosoma navyo
Mkuu,

Sasa hapo huoni kwamba mtihani unao kwa mke wako, si kwa hivyo vijamaa?

Maana hata ukipiga stop kwa hivyo vijamaa, bado unaweza kupigiwa kwenye vikao vya kanisani/ msikitini, vya ususi, vya kwenda kilioni, vya safari za kazi, kwenye safari za hospitali, , za kuchukua watoto shule, za birthday za watoto, za kutembelea rafiki...

Yani ikiwa anaweza kukufanyia uhuni huko, anaweza kukufanyia uhuninsehemu nyingi sana.

Huoni kwamba hapo unatakiwa ku deal na mkeo tu, si kuziba sehemu atakazoenda ambazo huwezi kuzimaliza?
 
Mkuu,

Hakuna hiyari ikiwa kuna kiranja ana ki Excel spreadsheet anahesabu nani kachangia mara ngapi. Huo ni mfumo wa nipe nikupe tu.

Yani hata ukisema mimi sichangi, we have to do better, unakuwa unahesabiwa mchawi hutaki kuchangia watu. You become a social outcast.

Sasa hapo hiyari iko wapi?

Hiyari yenye social cost si hiyari hiyo.

Mimi bora hata uniambie kuna mfuko wa kuchangia kwa mwaka naweza kuwa mwepesi kuliko hivi vimichango vya ad hoc naviona viko kushoto kweli. Ingawa nachangia kwa kiasi changu bado.

Yani naona ni kama alama ya umasikini najiingiza humo.
Mtaani kwangu kuna utaratibu kila nyumba sh 1000 anspotutoka kwana mtaa awe mtoto nk.

Book sio ishu sana. Ila wanaume wanakitabu tsh 20000 sasa hapa naona kuna upigaji.

Mtaa una nyumba 1000 kila kichwa sh 20000 huu sio mradi kweli? Sh 20.000.000/= tu assume wametoa wanaume 500 bado 10M ni pesa nyingi sana

Bora hata ingekuwa kila mwanaume sh 500 kwa wanaume 100 ni 50.000/=
 
Mambo ya Life Insurance ndiyo tushaona uchuro au watu wa Insurance wanakosea sehemu? Nasikia kuna mpaka group life insurance siku hizi.
 
Tuliomaliza shule wakati magroup ya whatsapp hayajaanza tulibadilishana mawasiliano tu..baadae teknolojia ikatukutanisha kwa sura zetu pichani na wengine hawaweki nyuso zao isipokuwa avatar au picha za wanawe nakadhalika. Kazi inakuwa na maswali pale lnapokuwa hamuonani na mnaanzisha group la malengo ya kusaidiana katika shida....

Michango inaanzishwa na mmoja anampoteza mazazi mnachangia kwa masikitiko makubwa japo hamujui ni kwa moyo wa kibinaadam na kuwiwa tu mnachangia 30k kila mmoja wengine hadi 50k

Kuna kitu nakiwaza tofauti japo si kwa nia mbaya kwamba baada ya miaka zaidi ya 10 mnauhakika gani hiyo.michango sio fraud? N muda mrefu na pesa ni mwanaharamu
Mawazo ya kimaskini... Mostly, mtu mwenye unafuu wa kipato huwa hawezi lalama akifanya CHARITY ACTIVITIES..
 
Hayo magroup ya Whatsapp ni majungu, umbeya, kufanya familia kugombana, wanaume kutaka tongoza wake za watu, mradi, watu kutokuwa na shughuli za kufanya, ujinga ujinga....
Sitojiunga wala kufikiria...
 
Nina group tulimaliza shule late 90s aisee liko Active Hadi unaogopa yaani...tuko 105......tunatoaga 10 tu Kila Mtu likitokea jambo yaani mkeka ukiwekwa aibu unasikia wewe usiyetoa
 
Tuliomaliza shule wakati magroup ya whatsapp hayajaanza tulibadilishana mawasiliano tu..baadae teknolojia ikatukutanisha kwa sura zetu pichani na wengine hawaweki nyuso zao isipokuwa avatar au picha za wanawe nakadhalika. Kazi inakuwa na maswali pale lnapokuwa hamuonani na mnaanzisha group la malengo ya kusaidiana katika shida....

Michango inaanzishwa na mmoja anampoteza mazazi mnachangia kwa masikitiko makubwa japo hamujui ni kwa moyo wa kibinaadam na kuwiwa tu mnachangia 30k kila mmoja wengine hadi 50k

Kuna kitu nakiwaza tofauti japo si kwa nia mbaya kwamba baada ya miaka zaidi ya 10 mnauhakika gani hiyo.michango sio fraud? N muda mrefu na pesa ni mwanaharamu
Wengine wapigaji, wengine sio wapigaji

ila kuchangisha rambirambi kwa kifo fake aisee hiyo laana itakayokupata, GOD knows
 
Back
Top Bottom