Hivi uhuru na lile la mzalendo liko wapi kweli jamani
Haya ni magazeti kongwe...yapo sana tu...Ila naona siku hizi wasomaji baadhi yao wengi wanabadilika..wanataka magazeti yale yanayotia chumvi yanayoiandika serikali.Uhuru na Mzalendo nayo wakati mwingine huwa 'yanaboa' kwa kuandika habari nyingi za kusifia CCM tu kama ilivyo kwa Tanzania Daima linalosifia CHADEMA tu...lakini siku hizi ukitaka gazeti lako linuniliwe andika stori za mipasho..kama hivi: fulani aliamsha dhidi ya serikali, Fulani atumbuliwa...Marekani ipo tayari kuja kufanya uchunguzi wa kupigwa risasi fulani..IMF yaikandia TZ...na kadhalika...hizi ni habari kwa mlengo au angle ya nchi za ulaya na Marekani..na magazeti yetu yanadaka hivyo hivyo...eti hiyo ndiyo transparency na objective reporting...dah..hovyo kabisa...Habariza ujenzi wa reli ya standard gauge hazitakiwi...