Haya madafu yetu Tz vipi?

Ufunuo wa Yohana

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
319
68
Mimi najiuliza shilingi yetu ya Tanzania imekuwaje tena? Mwishoni mwa mwezi wa pili exchange rate kwa dollar ilikuwa sh1150-1170, mwishoni mwa mwezi wa tatu especially tarehe 27/03/2008 ilikuwa 1210, wiki moja baadae yaani tarehe 3/04/2008 ikawa 1165 na leo tena ni 1200. jamani fractuations kama hizi kubwa kubwa zinasababiswa na nini hasa? na hizi fractuations si kwa dollar pekee hata ktk paund. Je kuna kiini macho gani hapa? Jamani hii haitumiki kunufaisha kundi furani? mathalani mtu amenunua dolla 1000 leo kwa bei ya sh 1170 ni sawa na sh 1,170,000 baada ya wiki moja akaziuza kwa sh 1210 ni sawa na sh 1,210,000 amegain sh 40,000 ktk dollar hizo 1000 tu. Je ingekuwa dollar 1,000,000 anagain sh 40,000,000 ktk week tu.
 
To be honest sijui exactly the cause of that, ila nahisi kitu kama Balance Of Payment (BOT), inapokuwa ianelemea upande mmoja then inaweza kuwa the factor of such fluctuations.

Lakini pamoja na hayo nahisi pia BOT should take an upper hand ktk kusimamia fluctuations ya Shiling yetu versus foreign currencies, private firms in most cases ends up benefiting themselves wakiachwa waamue rate.

Naamini kama kuna mtaalam wa mambo haya humu JF then naomba atupe more lights on that.
 
Dola na pound ziki fractuate shilingi yetu ita-respond. Dola ya marekani imekuwa ikiyumba kwa kipindi kirefu sasa, kuyumba kunakochochewa na fununu za kuwapo kwa depression America na dunia mzima kwa ujumla.

Kupanda kwa bei za vyakula na mafuta ulimwenguni nako kutayumbisha thamani za currencies. Kinachotegemewa kutokea sasa ni ongezeko la ela lisilo wiana na upatikanaji/uzalishaji wa chakula(demand pull-inflation); ongezeko la kiasi cha shilingi kwenye uchumi wetu likiambatana na kupanda kwa bei za mafuta katika soko la kimataifa litapandisha thamani ya dola. Kwa kuwa tayari dola nayo imekuwa ikiyumba, kunatokea vuta nikuvute dhidi ya shilingi na dola, na hivyo kusababisha hizo abrupt fractuations ambazo tunaziongelea.

Tuombe dola iendelee kuyumba, kwasababu ikiwa imara manake athari za njaa na kupanda kwa bei za mafuta katika thamani ya shilingi zitakosa upinzani, na hivyo kuizika shilingi yetu. Kadhalika tuombe bei ya mafuta iteremke mapema kabla BoT haijaporomosha shilingi yetu katika jitihada za kuzitega dola.
 
Back
Top Bottom