Ab-Titchaz
JF-Expert Member
- Jan 30, 2008
- 14,630
- 4,267
Hisani ya Maggid Mjengwa
![]()
Udenda unanitoka Mkuu Ab-Titchaz Nifungulie mlango ninakuja sasa hivi.Sikupigii simu naoan utamaliza haraka peke yako.
Mkuu Ab-Titchaz kaugali kenyewe mbona kadogo kadogo 🙂🙂🙂 si kataishia tu kwenye meno 🙂🙂
Mbona wantamanisha weye!.
lol! Sasa ukipiga tonge tatu za mtu mzima mwenye akili timamu 🙂 🙂 kaugali kamekatika!!!! inabidi iwekwe sufuria nyingine jikoni unasubiri hadi appetite inapotea! 🙂
narudi Tz aisee
....Siku hizi Mkuu huhitaji kuwa Bongo ili kupata msosi kama huu...hata bamia na nyanya chungu zimejaa tele kwenye masupermarkets ila inategema unaishi wapi. Miaka michache iliyopita vyakula vya kwetu ilikuwa ni nadra sana kuvipata siku hizi vinapatikana kwa wingi tu hata kwenye masupermarkets...na kuna wengine wanaagiza Bongo vile vyakula wavitakavyo kila baada ya muda fulani.Mambo kama haya yanakufanya utamani home to say the least. Chakula kina vutia kisha kina mswano!!!!
Menu imekaa vizuri ingawa si ya kula mwanamme wa shoka kwa upande wa matunda lol ....hayavutii AB...
...Umesikia harufu ya kuvutia ya samaki wa kukaangwa kisha kuungwa hadi umeamka lol! 🙂🙂 Mzima FL1?
hahahah si unajua sisi na samaki
Nilikuwa napiga kitabu kidogo,ndo nikaona nichungulie JF ..mara ugali na samaki limao na pilipili mbuzi kwa pembeni..
Hivi BAK unaweza kupata ,menu hii asubuhi?
Hahahahah lol! Kama appetite yako inaruhusu kuanza na ugali asubuhi basi sioni tatizo 🙂🙂...lakini mie pamoja na kuwa mpenzi mkubwa sana wa ugali lakini si wa asubuhi subuhi lol!
Kijini kwetu tunaanza na ugali asubuhi wa motooo uko kwenye chungu na nyama ya ng'ombe unashushia na maziwa ya mgando kwa afya.. ni ngumu lakini ,,
Hapa unakula healthy/quality na sio quantity mazee!...:biggrin: