Habari zenu wana MMU!,I hope mko ok!. Nionavyo mimi michepuko hasa kwa wanandoa husababishwa na 1.MSULULU WA WAPENZI KABLA YA NDOA.Hii ni kwa wote ke na me,kuwa na msululu wa wapenzi kabla ya ndoa huchangia michepuko kwa kiasi kikubwa hasa pale ambapo kwa namna moja au nyingine mke/mume anapojaribiwa kumlinganisha mume/mke wake na ex wake na anapobaini kasoro fulani hujaribiwa kuichukulia kasoro hiyo/hizo kama guarantee ya kuchepuka!. 2.KUOA/KUOLEWA NA KE/ME ASIYEKIDHI MATAKWA YA MOYO(NAFSI).Ni wazi kwamba katika hali ya kawaida ni vigumu kumpata Mwenzi anayekidhi vigezo na matakwa ya Moyo(Nafsi) kwa kiwango tarajiwa,hali hii inapoendelea hupelekea wengi kuamua kuoa/ kuolewa na ke/me yeyote kwa kupunguza au kupuuza vigezo na matakwa asilia ya Moyo(Nafsi) yake.Ikitokea ktk pitapita akakutana na ke/me ambaye anakidhi vigezo au matakwa ya nafsi yake huanza kujishutumu kuwa alifanya "wrong choice".Huyu asipochepuka ni jambo la kumshukuru Mungu!